Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Umejuaje moyo kudunda na kusukuma damu ni Mungu hufanya hivyo?
Moyo unadunda kwa nguvu ya roho ambayo ndio chanzo cha uhai wa mtu. Roho haionekani ndio maana mpaka sasa wanasayansi hawajaweza kufahamu chanzo.
 
Kusema tu hewa ninayo vuta ni ya Mungu bila uthibitisho, Hata mimi naweza kusema hewa unayo vuta ni ya Aliens 👽 bila uthibitisho.
Mungu ametuambia katika neno lake kwamba yeye ndio chanzo cha uhai. Pia amesema alimpa mwanadamu pumzi ya uhai hivyo hewa ni yakwake.
 
Unaposema angalia uumbaji, niangalie wapi?

Labda huko kwako ulipo ndio huo uumbaji unaonekana

Huko nilipo mimi siuoni labda unipe maana ya uumbaji ni nini
Nenda hapo nje uangalie kuku, mbuzi, ndege, wadudu, mimea nk utauona ulandano katika uumbaji. Halafu inua macho usiku utazame angani na mchana ukaiangalie milima na mabonde.
 
Nenda hapo nje uangalie kuku, mbuzi, ndege, wadudu, mimea nk utauona ulandano katika uumbaji. Halafu inua macho usiku utazame angani na mchana ukaiangalie milima na mabonde.
Kuku kila siku nawaona ila huo uumbaji ndio sijawahi kuuona.
 
Huyu jamaa ni mtu wa dua na maombi lakini anasema hakuna Mungu. Ninaamini alipitia changamoto za kimaisha hadi akamchukia Mungu lakini deep down anafahamu uwepo wake.
Scars
Dua si lazima iombwe kwa Mungu. Kuna Polytheistic religions ambapo ndani yake kuna Mystical traditions, Kuna na non-religious perspective kama vile Psychotherapeutic view, Secular humanist view n.k hao wote haya makundi yote yana dua zao lakini hayazielekezi kwa Mungu.
So Scars yupo sawa kuomba Dua bila kumuelekea Mungu.
 
Mungu ametuambia katika neno lake kwamba yeye ndio chanzo cha uhai.
Neno lake lipi?

Kuna maandiko mengi sana yanayo daiwa ni maneno ya huyo Mungu yanayo tofautiana maelezo ya chanzo cha uhai.

Kuna Biblia ya wakristo, Quran ya waislamu, Veda ya wahindu,Tiptaka ya wabudha, Kojik ya washinto n.k

Hakuna neno la Mungu zaidi ya hadithi za kutungwa na kusadikika sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
Pia amesema alimpa mwanadamu pumzi ya uhai hivyo hewa ni yakwake.
Haiwezekani Mungu huyo awe na maandiko mengi mengi yanayo daiwa ni maneno yake.

Mara wakristo wadai biblia ndio neno la Mungu na waislamu wadai Quran ndio neno la Mungu huyo.

Automatically Mungu huyo Hayupo katika uhalisia ila ni dhana ya kufikirika katika mawazo na imani za watu mbalimbali.

Hakuna neno la Mungu.

Kuna hadithi za kutungwa na kusadikika za kuelezea fictional character Mungu asiye kuwepo.

Biblia, Quran na maandiko yote ya kidini ni sawa na Hekaya za Abunuwasi au riwaya za Alfu Lela ulela.
 
Dua si lazima iombwe kwa Mungu. Kuna Polytheistic religions ambapo ndani yake kuna Mystical traditions, Kuna na non-religious perspective kama vile Psychotherapeutic view, Secular humanist view n.k hao wote haya makundi yote yana dua zao lakini hayazielekezi kwa Mungu.
So Scars yupo sawa kuomba Dua bila kumuelekea Mungu.
Na sio neno dua tu

Hata katika surprise naweza kusema "oh my god"

Just kama wewe unavyokuwa comfortable kutumia neno Thursday bila kujali kuwa umetaja jina la Mungu wa Thor.

Sidhani kama kwa kutaja kwako neno hilo unakuwa ni muumini wa huyo Mungu
 
Penye uhakika, hakuna imani

Penye imani, hakuna uhakika
Penye uhakika matokeo hayawezi kubadilika? Kwamba ukiwa na uhakika kwenye jambo ni kwamba lazima iwe hivyo hivyo?
 
Penye uhakika matokeo hayawezi kubadilika? Kwamba ukiwa na uhakika kwenye jambo ni kwamba lazima iwe hivyo hivyo?
Matokeo ya mwisho ambayo yanabadilika ndio uhakika wenyewe. Kabla ya hapo ulikuwa na mtazamo haukuwa na uhakika.

Kuwa na uhakika na jambo sio uhakika wa jambo

Mpaka kitu kiwe na uhakika ni mpaka kipitie misingi ya uthibitisho na kuwa verified.

Unaweza ukawa wewe unasema una uhakika wa jambo ambalo bado hujalifanyia uchunguzi baadaye matokeo yakaja tofauti

Na hiyo sio uhakika ni imani
 
Moyo unadunda kwa nguvu ya roho ambayo ndio chanzo cha uhai wa mtu. Roho haionekani ndio maana mpaka sasa wanasayansi hawajaweza kufahamu chanzo.
Kama roho haionekani, Wewe uli iona wapi ukajua ipo?

Roho isiyo onekana, ilifahamikaje ipo?

Aliyesema roho ipo, Ali iona wapi akajua ipo?

Mtu huyo aliwezaje kuiona roho isiyo onekana?
 
Dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mkamilifu, mwenye huruma na upendo kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya ya kila aina ni uthibitisho tosha kwamba Mungu huyo anaye daiwa kwamba ni mwema, mwenye upendo na huruma Hayupo.

Kama Mungu huyo yupo Basi ni mkatili na Muovu sana.
Nilikusudia kumjibu jamaa anayesema kwamba kisichokuwepo hakihitaji uthibitisho.

Nikamjibu kwa kjmpa mfano wa kitabu alichokiandika stephen akithibitisha kwamba Mungu hayupo.

Hivyo hata wanaokataa Mungu nao wanatakiwa wathibitishe kwamba Mungu hayupo.

Hiyo ndio ilikuwa point yangu.
 
Imani nyingi na dini nyingi humtafsiri na ku uelezea uwepo wa Mungu huyo kama mwema na mwenye Upendo.

Sasa kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya automatically Mungu huyo mwema na mwenye Upendo kwa mujibu imani hizi na dini hizi hayupo.

Otherwise Mungu huyo ni mkatili na muovu sana.

Hakuna ulazima wa Mungu kuwepo.

Mungu huyo Hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Bado haujajibu nilichouliza.

Unajadili uwepo wa huyo Mungu au unajadili hizo sifa za upendo na wema wa Mungu?

Jaribu kulielewa swali vizuri na kuona tofauti ya hivyo vitu viwili hapo.
 
Matokeo ya mwisho ambayo yanabadilika ndio uhakika wenyewe. Kabla ya hapo ulikuwa na mtazamo haukuwa na uhakika.

Kuwa na uhakika na jambo sio uhakika wa jambo

Mpaka kitu kiwe na uhakika ni mpaka kipitie misingi ya uthibitisho na kuwa verified.

Unaweza ukawa wewe unasema una uhakika wa jambo ambalo bado hujalifanyia uchunguzi baadaye matokeo yakaja tofauti

Na hiyo sio uhakika ni imani
Kwahiyo kitu kikipitia misingi ya uthibitisho na kikawa verified ndipo ukasema una uhakika je hicho kitu hakiwezi kubadilika?
Kwa sababu huko mwanzo ulisema unaamini Simba atamfunga Wydad hauna uhakika kwa sababu matokeo yanaweza kubadilika.
 
Kubadilika kuwaje?
 
Weka mfano
Mie tena nitoe mfano wakati mie ndio nataka kuelewa kutoka kwako! Tukitumia mfano wa Simba na Wydad ambapo umesema unaamini Simba atashinda kumfunga Wydad na unaamini kwa sababu hauna uhakika, kwa maana kuna chance matokeo yanaweza yasiwe hivyo kwa maana Wydad anaweza ndio akamfunga simba.

Sasa ndio nauliza je kwa jambo ambalo una uhakika hilo hakuna chance kuweza kubadilika?
 
Jambo ambalo nauhakika nalo ni Simba kushinda 3-0 dhidi ya Kagera sugar

Kuna chansi katika hilo ya matokeo kubadilika kuja tofauti?
 
Back
Top Bottom