RIP mzee Moi, pamoja na mambo mengine lakini ulionesha njia kwa viongozi wa Africa ambavyo wanatakiwa kuwa baada ya kishindwa uchaguzi, nakumbuka uliposhindwa uchaguzi na kuulizwa kwanini hujakataa matokeo, ulijibu jibu rahisi kwamba 'hiyo ndiyo demokrasia '
Hakushindwa 2002 ila chama chake kiligombea kikiwakilishwa Uhuru Kenuyatta ambaye alishindwa na kukubali matokeo.
Ukiacha Kenyatta ambaye alihodhi ardhi kubwa ya Kenya, Mzee Moi naye si haba kwa hilo. Na ameacha ukwasi wa kutosha kupitia familia yake. Tusisahau kashfa ya Goldenberg ambayo ilitikisa uchumi wa Kenya miaka ya 90, kila mkubwa akijichukulia chake. Mauaji na mateso kwa Wanasiasa na Wanaharakati, kupendelea kabila lake nk.
Ila angalau alijaribu kutafuta umoja wa Wakenya japo waliokuwa wanamzunguka walimzidi nguvu. Program ya kutoa maziwa bure kwa Wanafunzi nk.
Namsifu kwa kutokubali kuchakachua matokeo chama chake cha Kanu kiliposhindwa uchaguzi mwaka 2002. Taarifa zinasema kabla ya hapo matokeo yalipokuwa yanakuja ndivyo sivyo mwishoni wakijua wanashindwa, viongozi wakubwa wa karibu wakiongozwa na Lee Njiru wakamfuata na kumwambia wapindue matokeo tena mmoja alimwambia 'the matter is quantity and not quality'. Akawasikiliza halafu akaenda chumba kingine, akamwita Uhuru. Kilichofuata ni Uhuru Kenyatta kutangaza kukubali kushindwa. Mwamba Kanu ukaanguka.
Ni vyema kukumbuka mpaka 2002 Kanu hakikuwa Chama cha siasa kwa maana ya chama hasa bali kundi la Watu lililokuwa linafaidika na uwepo wa Kanu madarakani.
Nakumbuka kichekesho cha uchaguzi wa nani awe mgombea Urais, wakati huo Raila Odinga amehamia Kanu kwa ahadi ya kupewa kijiti! Chini kwa chini Moi kabadili mawazo anamtaka Uhuru kanuni zikapinduliwa. Kwamba wajumbe wapige kura kwa kunyoosha mkono au mlolongo!! Hahaaaa...nani angethubutu kwenda kinyume na Mzee Nyayo???!!
Nimekumbuka mengi sana enzi hizo.
Kbc na akina Khadija Ally, Mambotela, Jack Oyoo Sylivester nk. Jina linaanza na Mtukufu Rais.
Rip Moi
Sent using
Jamii Forums mobile app