KERO Sehemu ya Kuabudia Airport izingatie Dini zote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wakristo wakitengewa sehemu Moja ndio itakuwa shida kubwa maana madhehebu mengine wataona wenzao wamependelewa
 
Katika karne hii serikali inakumbayia mambo ya kioumbavu kabisa halafu ndiyo watu watarajie nchi kuja kusonga mbele?

Waislam wanawekewa sehemu za kuswalia sehemu nyingi tu sio hapa Tanzania tu.

Mfano






Prayer Facilities
Terminal 4 has dedicated prayer rooms for major faiths. The Muslim Prayer room is well maintained with seperate areas for males and females. However for wudhu, you have to use the common washrooms which are not very wudhu friendly. From whatever terminal, you can take the inter-terminal train to Terminal 4, which only takes 5 minutes.

The prayer room is located near the Emirates check-in counter. It is located in the public area, if you are departing from JFK, then you should pray before going through the immigration control. Jumu'ah prayer is performed here as well.

Another prayer room is located in Terminal 1 Back left corner of 2nd floor(departures)



Hizo ni nchi za kimagharibi ambazo nadhani unakubali zimesonga mbele.

Saudi Airlines wameweka sehemu za kuswali kabisa katika ndege zao na Etihad Airways wameweka sehemu za kuswali katika baadhi ya ndege zao. Kama ni maendeleo kwa tafsiri yako hao wanayo kuliko nchi unayotokea.


Natumai wenzao wataiga hili katika ndege zao pia Akitaka Allah
 
Kwa sababu wanajidekeza na hawakawii kuzira na kutupa mawe.
 
Dini nyingine tumeanza lini kuabudu safarini, wenzetu walianza kitambo mpaka kwenye vituo vya mafuta
 
Uislamu ulikuta miundo hiyo ipo tayari inatumika kikalenda.Kama inakera,ombi liwekwe irekebishwe.
Uislam umeingia hapa Afrika Mashariki kabla ya ukristo kwa zaidi ya miaka 1000 nadhani unajua hili. Kalenda ya Miladia imeanza kutumika rasmi hapa kwetu lini?

Acheni ligi
 
Makanisa, Mahekalu, Misikiti n.k. hayatoshi ? Badala ya kuwaza kuongeza Bridges mnataka kuongeza Walls kwa Imani zenu ambazo hata mababu zenu hawakuzitambua....
 
Basi zisijengwe nyumba za ibada za dini yoyote Airport.
 
Narudia tena. Katika Uislam kuna Swala ambazo ni LAZIMA kuziswali.. Swala tano za Faradhi ni Lazima kuswali. Swala tano ni LAZIMA kuziswali.

Wakatoliki nao kwao hizo sala zao ni lazima? Ni nguzo katika nguzo za dini yao?

Tusilazimishe tu kulinganisha.
 
Ni sawa pia kama mapumziko yataondolewa siku za eid na maulid
 
Na sie waabudu mizimu sehemu yetu ya KUABUDU iwepo pia
 
Kwa hiyo unataka Jumapili ukasali Airport?
 
Uliwahi kua mkristo au kua wa dini nyingine zaidi ya uislamu?Kama haujawahi,nini kinakuelekeza kwamba kwenye uislamu ndiyo kuna ulazima zaidi wa kusali kuliko dini zingine?Acha upotofu.
 
Tufate maelekezo ya Mungu kuhusu Ibada

Siku 6 fanya kazi, lakini siku ya 7 ni Sabato
 
Unazijua sala za masfu na sala za saa sita mchana na za jioni?Jiboreshee ufahamu.
Nadhani acha ubishi mahitaji ya dini hizi ni tofauti kabisa sasa usilazimishe jambo ya kafanana. Mkristo hata akikosa misa haambiwi kwa imani kama katenda dhambi waislamu unaambiwa usikose swala na sio kukosa swala kwa muda wake ufanye ibada. Tusitake kila kitu kifanane kama ushindani wa Simba na Yanga.
 
Uislam umeingia hapa Afrika Mashariki kabla ya ukristo kwa zaidi ya miaka 1000 nadhani unajua hili. Kalenda ya Miladia imeanza kutumika rasmi hapa kwetu lini?

Acheni ligi
Uislamu kuingia E Africa hiyo miaka(kwa madai yako)ndiyo yamefuta ukweli kwamba Ukristo ulianza kabla ya Uislamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…