Sehemu za kazi ni sehemu hatari sana ingawa tunapokea chochote kitu

Moja ya mambo niliwaeleza Niliwaambia wazazi wote walifariki nilisomeshwa na wasamaria wema na nikafanikiwa kuwa kwenye top 10 of form four students kwa mwaka wetu. Sasa hiyo story imekuwa ikijirudia hadi nakwazika yaani
Wanakuonea husda,so wanatumia karata ya uyatima na kusomeshwa na wasamaria wema,kukuumiza kisaikologia.
Chapa kazi,hiyo ilikuwa mipango ya Mungu,kumbuka kila mja ana story yake hapa duniani.
 
Kwenye hiyo 300M ya Consultant kulikuwa na ugali wa watu ndio maana uliona hayo majungu
 
Kiufupi sana, kazini hakuna rafiki
 
Mkuu nimesoma mara nyingi ila sijaelewa. Naomba fafanua kwanini umeacha kazi?
Mkuu mm siwez kufanya Kaz chini ya micro-manage. Mana tulikuwa tunafanya connect na watu tofauti.. na njia ya mawasiliano ni simu. Unampigia sim mtu siku nzima haipatikan siku ya pili unaandika report ya uliowasilian nao wote. Wengine hawapatikan, kesho anapigiwa anapatikana unaonekana hujamtafuta na inaibua mzozo.

Kuna watu maofisn kama madem tu. Kuna kijamaa ndo kikawa kinaleta maneno maneno mara ohh mkataba wako utaisha tu. Mm mkuu nafanya kazi masaa ya kazi tu, hata kama workload ya siku haijaisha muda ukiisha nasepa. Habari za kwa nn yondoke na kazi za Jan hujamaliza usiniulize. Nimewaashia popo na nikasepa bila kuwadai hata mia
 
Wanaume wengi wa Maofisini wana pigo za kike kike
 
Wakati mwingine huwa tunashindwa kuthubutu kufanya maamuzi kama hayo
Fear of tomorrow.... Mnaambizana kuwa mitaani kugumu! Usiache kazi kabla hujapata Kaz mana sijui kufanyaje... Kupata kazi nzuri ukiwa katika Kaz mbaya ni ngumu mana inakubana muda wako. Kama una ka mtaj ka kuzugia unajilipua tu
 
Nilipitia hayo hadi leo sitaki kuajiriwa tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…