Juni 28, 2025, Rashid Kilua alikwenda kuchukua fomu kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Bumbuli akiwa katika ofisi za Wilaya alifanikisha zoezi la Fomu ila inasemekana watu waliotajwa ni wafuasi wa Januari Makamba hawakuondoka eneo hilo ingawa nao pia walishachukua Fomu.
Inasemekana Baadae Saa 8 Kilua Alifika ofisini akiwa na waandishi wa Habari wake na mpiga picha wake akaingia ndani akachukua fomu, kisha akatoka nje kwa ajili ya kupiga picha.
Wakati tukio la kupiga picha linaendelea alitokea January na watu wake na kumvamia Kilua na kumkataza asipige picha.
Chanzo: Matukionline