Nyerere nae anasingiziwaga mengi nyie, khaa. Yule mzee hadi anakufa aliliamini azimio la Arusha, leo lipo? Ni yule mzee ndio aliasisi muungano wa serikali 2 na nchi 1 inaitwa Tanzania, leo iko hivo kweli? Same mzee aliamini katika mashirika ya umma, leo ipo namna hiyo? Mzee yule alishauri ccm kuukubali mfumo wa vyama vingi, Augustin Mrema hadi alikua anaambiwa na wafuasi wake azime gari lake na wao wanamsukuma, aliyekua waziri wa mambo ya ndani those years bwana Nyanda from Mwanza, aliamuru Mrema kupigwa mabomu ya machozi wakati wa kampeni, Nyerere alikemea jambo hilo; leo hali ikoje? Lissu si anakusudiwa kunyongwa? Ni mambo ya Nyerere hayo kweli? Njoo kwenye rushwa, mzee Mchonga aliwahi hadi kukata majina ya wagombea fulani na baada ya kumpata mgombea aliyedhania yeye kwamba ni Mr. Clean, mzee alitamka kabisa kwamba, "tumezishinda fedha za Bangi" leo hali ikoje? Msimsingizie Nyerere, alikua na madhaifu yake lakini kwa hapa tulipo yeye hahusiki; kwa ujumla ccm ya Nyerere na ccm hi ni ccm mbili tofauti, yake ilikua ya jembe na nyundo, hi hapana.