Watu kila mtu awe mkulima hizo kazi nyingine watafanya nani tunashida sana kwenye kufikiri
Mfano developed countries watu wanaojihusisha na kilimo hawafiki hata asilimia 3 lakin ni nadra sana kusikia Kuna njaa, Ila Tanzania na nchi nyingi za afrika majority watu almost 30% ya watu wanashiriki kwenye kilimo lakin ni kawaida kusikia Kuna njaa
Mtu unalima heka mbili au moja alafu unajiweka kwenye kundi la wakulima si vichekesho alafu unataka ufanikiwe kupitia kilimo watu waache utani
Unaokoteza maneno ya hapa na pale.
Kwenye nchi hizo zilizoendelea:
1) umewahi kusikia kuna ban ya uuzaji mazao yao nje?
2) kweenye hizo nchi zilizoendelea unafahamu jinsi serikali zao zinavyofidia gharama zabuzalishaji na kumpa mkulima ruzuku ya kumwezesha apate faida ya 20% pale ambapo mkulima anapokuwa amepata hasara kutokana na kushuka kwa bei au mazao kukosa soko?
3) mkulima wa Tanzania hasaidiwi chochote na Serikali, hivyo ni haki kabisa afanye namna anavyotaka akishayavuna, ikiwa ni pamoja na kuuza popote patakapompa faida au kumpunguzia hasara.
Kwa mwaka huu:
Mbolea ilikuwa sh 120,000 kwa mfuko wa 50kg
Eka moja kulima siyo chini ya 100,000
Kupalilia mara mbili siyo chini ya 160,000
Kuvuna na kupukuchua siyo chini ya 100,000
Kusafirusha toka mashambani mpaka sokoni siyo chini ya 200,000
NB: eka moja hutumia mifuko 3 kupanda, na mitatu kukuzia = 720,000
Maeneo mengi kutokana na upungufu wa mvua, mavuno ya mahindi yalikuwa kati ya magunia 5 mpaka 10.
Bei ya gunia moja la kilo 100, anayopata mkulima ni kati ya 50,000 - 55,000. Kwa magunia 10, ina maana ni sh 500,000 - 550,000.
Halafu kuna mwendawazimu mmoja mjini utamsikia anasema kuwa bei zipo juu sana! Unajua gharama za uzalishaji? Kama kilimo kina faida sana kuliko kazi unayoifanya, acha hiyo kazi, nenda ukalime ukafaidi bei anayoipata mkulima. Hata kama umeaomea udaktari, lakini hakuna anayekulazimisha kufanya kazi ya utabibu. Wapo wengi wamesomea fani fulani, lakini siyo wanachokifanya. Kama huwezi, endelea na kazi yako, kalipe bei ya soko ya mazao ya chakula.
Mimi siyo mkulima, lakini nilijaribu kuwekeza kwenye kilimo, kwa kweli kwa gharama za uzalishaji ziluzopo, na kwa bai zilizopo, hakuna mwekezaji makini ataenda kuwekza kwenye kilimo. Mkulima wa Tanzania, kwa mazingira yaliyopo, na kukiwa na viongozi wajinga wanaoamini kuwa suluhisho la kushusha bei za vyakula ni kuzuia wakulima kuuza chakula nje, ataendelea kuwa duni kuliko makundi yote.