Serikali: Bei ya Mchele imefikia Tsh. 3,500, Maharage 3,500, Mahindi 1,500 kwa kilo

Serikali: Bei ya Mchele imefikia Tsh. 3,500, Maharage 3,500, Mahindi 1,500 kwa kilo

We ni mjinga sana nimeona ukiongea huu ujinga kwenye nyuzi nyingi nimeona nikujibu sio kila mtu lazima awe mkulima hizo kazi nyingine zitafanywa na nani unajua maana ya division of labour and specialization

Kwa kukusidia a modern agriculture inafanywa na watu wchache sana sababu ni machine extensive hiko kilimo Cha kufanywa na watu wengi kama wewe unavyo advocate ni Cha kizamani
Mbona umepewa ushauri mzuri Mkuu!.. kalime uuze buku jero acha kupanic
 
Mbona umepewa ushauri mzuri Mkuu!.. kalime uuze buku jero acha kupanic
Sasa kila mtu akilima nani atamuuzia mwenziwe?
Tuache majibu yasiyo na tija..

Yaani ni sawa na wale wanaosema kuikosoa serikali ni kulalamika, kwamba tuache kulalamika tutafute hela au tuhame nchi.
Hii si sawa.
Hatuwezi kuwa wote wakulima au wafanyabiashara! Tunategemeana
 
Kwani mimi nataka Samia afanyaje sasa [emoji38][emoji38]..

Hayo mapovu kamtolee bibi yako Ili akutumie maharage na mahindi..

Mtanyooka ngoja ifike wa 12 kuelekea wa 2 mtanunua elfu 5 tuone mtakachofanya fala wewe..

Mumevimba matumbo kama kitimoto kwa jasho la wakulima,this time mtajua hamjui..
Uzuri ni kwamba watakao kiona cha moto ni ukoo wako ambao ni masikini wa kutupwa
 
Ukifika uchaguzi utasikia ccm ni ile ile ooh ni ni ileile wanaimba mazuzu tena wengine ndio walalamikaji leo!
 
Wafunge mipaka na iundwe sheria ngumu atakayekamatwa akisafirisha nafaka nje apigwe kesi ya uhujumu uchumi
Kuzuia export ya mazao ya kilimo kama njia ya kutatua tatizo la mfumko wa bei, ni njia primitive ya kutatua tatizo. Ni njia zinazotumika na watu waliokosa maarifa.. Zinatakiwa kutafutwa njia ambazo ni sustainable.
 
Wameshaweka ban ya kuuza mazao nje ya nchi na hapo unasemaje
Aliyeweka hiyo ban amekosa maarifa. Hiyo ban itasababisha kutopata ongezeko sustainable la uzalishaji mazao ya kilimo.

Gharama za uzalishaji zipo juu sana. Masoko ya mazao ya kilimo ya ndani ya nchi kukiwa na chakula kingi kidogo tu, hayaeleweki. Nani mwenye akili timamu atakayepoteza mtaji wake aende akafanye shughuli za kilimo wakati anajua kuwa hana uhuru wa kuuza kwenye soko ambalo anaamini litalipa gjarama zake za uzalishaji? Nani atakubali kuwa mtumwa wa Serikali, yaani alime yeye, gharama zote ni zake, halafu Serikali ambayo haimsaidii chochote, ije kumpangia nna ya kuuza? Je, Serikali italipia pengo la tofauti kati ya gharama za uzalishaji na mapato, plus faida anayoitafuta mkulima?

Mkulima hana wajibu wa kitaifa wa kuwatunza Watanzania. Kama Serikali inataka kuhakikisha uwepo wa chakula cha kutosha, ilistahili kufanya ununuzi wa mazao kwa kwenda kushindana na wanunuzi wengine, na kisha kuhifadhi kwenye maghala yake.
 
Sijui ni makuzi tu.

Katika kukua kwangu, sijawai ona home vyakula vikinunuliwa kwa kilo, stoo ilikua inakua na kila kitu,mahindi,mpunga,maharage ,alizeti n.k ,nje mifugo na bustani za mboga . hii tabia nimeibeba mpaka kwenye familia yangu, sinunui vitu reja reja, nalima au kununua kwa wingi nafunga mwaka.

Sijisifii, ila nunue vitu in bulk kipindi cha mavuno
.
 
Sio kila mtu lazima awe mkulima Kuna viwanda vinahitaji wafanyakazi, serekalin wanahitaji wafanyakazi, utalii unahitaji wafanyakazi ukitaka kila mtu hiko kitu hakitakaa kitokee na inaonyesha ulivyokua na upeo mdogo

Hata bidhaa za viwandan vina Bei elekezi sio tu kwenye kilimo ni karibia sekta zote Wana Bei elekezi
Unatakiwa ufanye kazi unayoona inakulipa. Hakuna anayekulazimisha ufanye kiwandani, kwenye utalii au serikalini. Unakoona wewe kutakulipa vizuri, nenda kafanye huko.

Kufanya kilimo Tanzania ni aghali sana, ndiyo maana kilimo cha mazao ya chakula cha Tanzania kimeachwa kwa watu wasio na chaguo jingine la maisha.

Tukitaka kilimo kiwe na tija, kama ambavyo wakulima walivyoachwa bila msaada wowote, vivyo hivyo, hata kwenye masoko, wauze popote watakapoona pana tija. Kilimo kitakapoonekana kina tija, kitawavuta watu wengi, kufanya kilimo, na hilo ndilo litakalosababisha kuwa na chakula kingi cha ziada.

Kama Serikali inataka kuwa na maamuzi juu ya wapi mkulima auze mazao yake, basi pia itoe ruzuku kwa wakulima kufidia pengo kati ya gharama za uzakishaji na kile anachokipata akiuza mazao yake, ongezea na faida anayoitafuta. Vinginevyo kumzuia mkulima kuuza mazao yake mahali anapoona kuna bei nzuri ni ujambazi wa hali ya juu. Anayeona mkulima anafaidi sana kwa bei zilizopo, aende na yeye akafanye shughuli za kilimo. Kudai eti haiwezekani kila mtu kuwa mkulima, ni utetezi wa kijinga, kwa sababu mtu yeyote ana uhuru wa kufanya kazi yenye tija. Kama wewe ni lawyer, unaona kilimo kina faida kubwa, acha kazi yako ya uanasheria, ukafanye kilimo, au endelea na kazi yako, lakini kawekeze kwenye kilimo, halafu baada ya muda utarudi na kuzungumza vitu sensible.
 
Sijui ni makuzi tu.

Katika kukua kwangu, sijawai ona home vyakula vikinunuliwa kwa kilo, stoo ilikua inakua na kila kitu,mahindi,mpunga,maharage ,alizeti n.k ,nje mifugo na bustani za mboga . hii tabia nimeibeba mpaka kwenye familia yangu, sinunui vitu reja reja, nalima au kununua kwa wingi nafunga mwaka.

Sijisifii, ila nunue vitu in bulk kipindi cha mavuno
.
Kwasababu huna uhakika wa Kula kesho.
 
Ban imeshawekwa tayari kama ulikua hujui
Kama ban unaamini kuwa ndiyo suluhisho, suburia uuziwe mchele kwa sh 500, na wala usilalamike ten. Ban ya uuzaji mazao ya kilimo nje kama njia ya kudhibiti mfumko wa bei, ni uwendawazimu, na mbinu kama hizo zinafanywa na viongozi waliokosa maarifa.

Kama ban huongeza uzalishaji, sahizi uzalishaji wa korosho ungekuwa umeongezeka maradufu. Ban siku zote hupunguza uzalishaji. Hakuna mtu mwenye uelewa mkubwa atafanya shugjuli ambayo, kukitokea kitu kidogo tu, anatokea kiongozi mjinga, na kuingilia mfumo wa biashara. Biashara na uwekezaji huangalia sana predictability.
 
Wakulima wanaombea ipande zaidi. Kufa kufaana
 
We ni mjinga sana nimeona ukiongea huu ujinga kwenye nyuzi nyingi nimeona nikujibu sio kila mtu lazima awe mkulima hizo kazi nyingine zitafanywa na nani unajua maana ya division of labour and specialization

Kwa kukusidia a modern agriculture inafanywa na watu wchache sana sababu ni machine extensive hiko kilimo Cha kufanywa na watu wengi kama wewe unavyo advocate ni Cha kizamani
Kila mtu ashinde mechi zake kilimo ni Biashara wakulima pia hawatoi huduma wanafanya biashara kama wengine tuu
 
Watu kila mtu awe mkulima hizo kazi nyingine watafanya nani tunashida sana kwenye kufikiri

Mfano developed countries watu wanaojihusisha na kilimo hawafiki hata asilimia 3 lakin ni nadra sana kusikia Kuna njaa, Ila Tanzania na nchi nyingi za afrika majority watu almost 30% ya watu wanashiriki kwenye kilimo lakin ni kawaida kusikia Kuna njaa

Mtu unalima heka mbili au moja alafu unajiweka kwenye kundi la wakulima si vichekesho alafu unataka ufanikiwe kupitia kilimo watu waache utani
Unaokoteza maneno ya hapa na pale.

Kwenye nchi hizo zilizoendelea:

1) umewahi kusikia kuna ban ya uuzaji mazao yao nje?

2) kweenye hizo nchi zilizoendelea unafahamu jinsi serikali zao zinavyofidia gharama zabuzalishaji na kumpa mkulima ruzuku ya kumwezesha apate faida ya 20% pale ambapo mkulima anapokuwa amepata hasara kutokana na kushuka kwa bei au mazao kukosa soko?

3) mkulima wa Tanzania hasaidiwi chochote na Serikali, hivyo ni haki kabisa afanye namna anavyotaka akishayavuna, ikiwa ni pamoja na kuuza popote patakapompa faida au kumpunguzia hasara.

Kwa mwaka huu:

Mbolea ilikuwa sh 120,000 kwa mfuko wa 50kg

Eka moja kulima siyo chini ya 100,000

Kupalilia mara mbili siyo chini ya 160,000

Kuvuna na kupukuchua siyo chini ya 100,000

Kusafirusha toka mashambani mpaka sokoni siyo chini ya 200,000

NB: eka moja hutumia mifuko 3 kupanda, na mitatu kukuzia = 720,000

Maeneo mengi kutokana na upungufu wa mvua, mavuno ya mahindi yalikuwa kati ya magunia 5 mpaka 10.

Bei ya gunia moja la kilo 100, anayopata mkulima ni kati ya 50,000 - 55,000. Kwa magunia 10, ina maana ni sh 500,000 - 550,000.

Halafu kuna mwendawazimu mmoja mjini utamsikia anasema kuwa bei zipo juu sana! Unajua gharama za uzalishaji? Kama kilimo kina faida sana kuliko kazi unayoifanya, acha hiyo kazi, nenda ukalime ukafaidi bei anayoipata mkulima. Hata kama umeaomea udaktari, lakini hakuna anayekulazimisha kufanya kazi ya utabibu. Wapo wengi wamesomea fani fulani, lakini siyo wanachokifanya. Kama huwezi, endelea na kazi yako, kalipe bei ya soko ya mazao ya chakula.

Mimi siyo mkulima, lakini nilijaribu kuwekeza kwenye kilimo, kwa kweli kwa gharama za uzalishaji ziluzopo, na kwa bai zilizopo, hakuna mwekezaji makini ataenda kuwekza kwenye kilimo. Mkulima wa Tanzania, kwa mazingira yaliyopo, na kukiwa na viongozi wajinga wanaoamini kuwa suluhisho la kushusha bei za vyakula ni kuzuia wakulima kuuza chakula nje, ataendelea kuwa duni kuliko makundi yote.
 
Sasa kila mtu akilima nani atamuuzia mwenziwe?
Tuache majibu yasiyo na tija..

Yaani ni sawa na wale wanaosema kuikosoa serikali ni kulalamika, kwamba tuache kulalamika tutafute hela au tuhame nchi.
Hii si sawa.
Hatuwezi kuwa wote wakulima au wafanyabiashara! Tunategemeana
Kalime wewe uwauzie wengine. Kwani wewe umelazimishwa usilime. Kafanye unachokiona kina tija.

Kuna waliosomea udaktari lakini hawatibu. Kuna watu wamesomea uwalimu lakini ni wanasiasa, n.k. Kafanye kile unachokiona kina tija kwako. Kama huko kwenye kilimo watu waanafaidi sana, nenda na wewe huko, la sivyo, nyamaza kaa kimya, nunua kwa bei ya soko, sawa na anavyonunua bei ya gari toka Japan, au dawa toka India au Uk.
 
"Najua mtanikumbuka kwa mazuri sababu nime sacrifice maisha yangu kwaajili ya Watanzania maskini" ..... Wanasiasa na mabwanyenye "huyu hapendi matajiri na ana roho ya kimaskini"

Kinachoendelea sasa .... wanasiasa na mabwanyenye "tunalamba asali na tujadili ianze Katiba au tume huru" ........Maskini "Tutakufa kwa njaa mchele na unga bei haikamatiki, tozo zinatuumiza na umeme unakatika ovyo" .... wanasiasa na mabwanyenye " Tozo tutaunda tume , bei ya vyakula ni sababu ya vita vya Ukraine tulisema kila kitu kitapanda ila tutafanya mchakato kuona bei ishuke vipi, kuhusu umeme ni matengenezo ya kawaida, mnajua hii mitambo imeendeshwa miaka mitano bila maintenance, serikali ipo kazini" [emoji1]
 
Tafuteni pesa wazee, hata kilo 1 ya mchele ikiuzwa elfu 10 kama pesa unazo wala uwezi lalamika.
Shida ya watanzania wengi wanaangalia leo tu wanachoamini maisha ni kula tu chakula kinavyopanda bei wao hawaoni kama ni fursa ya kuzalisha zaidi wanabaki wakilalama tu. Kitu kingine watu wapo siriazi Sana na kilimo wanawekeza mitaji yao shambani halafu anatokea mwanasiasa mmoja anampangia mkulima mahali pakuuza mazao
 
Shida ya watanzania wengi wanaangalia leo tu wanachoamini maisha ni kula tu chakula kinavyopanda bei wao hawaoni kama ni fursa ya kuzalisha zaidi wanabaki wakilalama tu. Kitu kingine watu wapo siriazi Sana na kilimo wanawekeza mitaji yao shambani halafu anatokea mwanasiasa mmoja anampangia mkulima mahali pakuuza mazao
Kwahiyo bei zipande tu ili watu waone fursa? Kwanini zisipande kwenye mazao ya biashara? Umeshiba wewe hukumbuki hali halisi ya watu maskini na yanayowazunguka.
 
Wali maharage ni msosi mmoja maharufu uswahilini, ila naona nao unaenda kuonekana ni kitu cha anasa.

Manake wali nyama mpaka sikukuu, ila tuendeko wali maharage nao kuliwa mpaka sikukuu ifike.
 
Back
Top Bottom