Tetesi: Serikali haina pesa. Hali ni mbaya ya kusua sua baadhi ya Donors waanza kulalamika

Tetesi: Serikali haina pesa. Hali ni mbaya ya kusua sua baadhi ya Donors waanza kulalamika

Wapuuzi nyie,kodi hamlipi mnashindana kupeleka pesa kwa manabii matapeli,na mafungu ya kumi huko makanisani kutajirisha wwavivu wa kazi hao

Tofautisha Kodi ya serikali ambayo ni lazima kisheria na fungu la kumi ambalo ni hiari. Ni Kama mtu anamaliza laki nzima bar hiyo ni hiari yake. Ndio maana TRA ipo kwaajili hiyo.
 
Kimsingi toka mwezi wa 9 hakuna Malipo yoyote yanayofanyika serikalimi. Kibubu hakina kitu. Miradi ya maendeleo yote imesimama ndio maana wale YASP wa SGRA wanapunguza wafanyakazi. Hakuna OC kwenye mataasisi au Halmashauri. Kimsingi, hakuna pesa yule ajuza wa Zanzibar ana kazi ya kuturembulia macho tu. Katika pogo amblo Mungu alitupiga watanzania ni lile la 17/3/2021. Hii takataka isingeingia madarakani.
Umenikumbusha 17 March siku ya sherehe kuu baada ya lile shetani lenu la Chato kutwaliwa na Muumba
 
Baadhi ya donors wameanza kulalamika kuwa wanachangia pesa lakini hazitumiki vizuri. Zinatumika katika kusafiria na kulipana posho.

Mnakumbuka pesa za kukubali uwepo wa Covid 19 na kupigwa chanjo? Tumezila sisi wakuu... Tumewana kwa namna mbalimbali. Inaumiza lakini unaona wenzako wanapiga... Ukisusa wao wala. Unaona nawe uchukue kwa shingo upande huku ukiona huruma.

HAPO TUKAWA TUNAANZISHA MIRADI BUBU YA WAZALENDO humo ndani ndo tunasosomola madollar. Nyie wananchi endeleeni kutudumisha tu. Tudumu cc , tudumu.

Serikali imeshindwa lipa Wakandarasi. Imeshindwa lipa wengi ambao walifanya huduma kwayo. Hakuna pesa. Donors wanasema wanatoa pesa zinaliwa tu na wachache. Hali ni mbaya.

Traffic sasa wamepewa hesabu kwa siku ukiwa barabarani unahakikisha unakusanya kiwango ulichowekewa. Hali imekuwa tete. Makosa yanatafutwa hata usipochomekea unaweza pigwa faini kuwa unaendesha gari bila kuchomekea ni hatari shati linaweza nasa kwenye pedal ya accelerator ukashindwa hamisha mguu kuja kwenye brake.
VC akiwa kama mchumi mbobevu alilazimika kwenda huko majuu kwa kazi maalum kwa siku zaidi ya 30 huku ukimya ukiwa umetamalaki.
 
Miradi Kama SGR haiendeshwi kwa pesa za Donors. Hizo ni pesa za MIKOPO.

Magufuli alikuwa anakopa KINUHA kwenye mabenki ya kibiashara, mikopo yenye riba kubwa halafu ya muda mfupi.

Sasa SGR haijaisha na madeni yameiva yanatakiwa kulipwa.

Wanachofanya Bibi too na Mwigulu ni kukopa sehemu nyingine na kulipa.madeni yaliyoiva.

Mzungu alishajua mitawala ya Africa ni mijuha na Ina tamaa Kali sanaa.

Kwahiyo, Mzungu akitoa pesa yake iwe msaada au mkopo nafuu anaiwekea masharti, hasa itumike kwenye Afya, demokrasia, utawala Bora, haki za binadamu au Mazingira na Mzungu anakagua pesa zake hataki ujinga.

Pesa unazoona Wanasiasa wanafanyia anasa za posho, mishahara, kulipa wake wa viongozi, kununua magoli ya mpira ni pesa za TRA na makusanyo mengine.
Mwafa
 
Back
Top Bottom