DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu hasira humuumiza anayeihifadhi.

Mahita na ugaidi wake anafikia 75 wewe unaweza usitoboe 40 sababu magonjwa ya moyo na hasira za kijinga.
 
Mkuu hasira humuumiza anayeihifadhi.

Mahita na ugaidi wake anafikia 75 wewe unaweza usitoboe 40 sababu magonjwa ya moyo na hasira za kijinga.
Kuna mahali nimesema "nitatoboa" miaka 40?

Umri wangu unaujua?

" Kutoboa" miaka 40 au 75 kuna uhusiano gani na maoni yangu.?

Kumbuka hata wajinga na washenzi huzeeka.
 
Huyu jamaa bado anadhani bado ni IGP.hata wakati yupo madarakani alikuwa na tabia ya hovyo sana na hakupaswa kumilikishwa silaha.hii nchi ya hovyo sana ni kama vile hatuna serikali na wakati jpm alikuwa mpole sana ila sasa wanachezea sana mama
Itifaki za polisi huyu ni mkubwa kuliko wambura😁😁.

Unasema wakati wa wapi alikuwa mpole!!!!kasikilize seherehe za miaka 60 ya polisi usikie alimwambia nini siro mbele ya jpm,ndio utajua hii kichwa hata BWM aliishi nayo kwa tabu sanaπŸ˜…πŸ˜…

Siungi mkono ubabe hasa wa silaha,lakini hakupiga mtu aivunja kufuli awahi kuondoka.
 
Kuna mahali nimesema "nitatoboa" miaka 40?

Umri wangu unaujua?

" Kutoboa" miaka 40 au 75 kuna uhusiano gani na maoni yangu.?

Kumbuka hata wajinga na washenzi huzeeka.
Sasa hubiri faida za kuonekana timamu mbele za watu,maana huyu dingi kakuzidi kila kitu japo unamwona mwehu.

Sijuo una umri gani but unasound 19yrs😁
 
JK mbali sana. akakamate gari hata ya Tibaijuka tu
Wakati wa Magufuli Kuna traffic alikamata gari ya mke wa waziri wa mambo ya nje na east Africa akapandishwa cheo. Ila kwa sasa serikali ya mama lazima wenye vyeo vyao wawanyanyase wenye vyeo vidogo na wasiokuwa na vyeo.
Kwenye serikali ya Magu hakuna aliyekuwa juu ya Sheria ila alivyokufa misimamo yake pia ikauawa.
 
Mkuu, sasa hapo habari za askofu mstaafu ziningiaje?
Ni kweli huduma aliyyokuwa akitoa ni kutukuka lakini inawezekana huyo kijana hakujua hilo. Yy alitekeleza kadri ya maagizo ya boss wake. Kwani huyo mkubwa mstaafu angejitambulisha kwake angelinyimwa hiyo favour? Kama alikuwa ameiacha garihiyo na mlinzi halafu mlinzi akamjulisha kwamba gari hiyo ni ya fulani halafu kijana akakaza shingo, basi huyo mkubwa angelichukua hatua nyingine ya kistaarabu zaidi e.g. kumwita na kujitambulisha kwake wakayamaliza kiungwana zaidi kuliko kutumia silaha.
Matumizi ya silaha haikuwa vizuri. Kijana angeliweza bado kumjulisha bosi wake ili apate maelekezo.
 
All animals are equal, but some animals are more equal than others.
 
Huu muda wote kwa IGP mstaafu unatoka wapi??

Mpaka anakata hiyo lock kwa vyovyote kijana aliyeyuka baada ya kuingia ubaridi,anatafutwa haonekani.

Angefunga kisha amsubiri mbona angefungua mwenyewe kawaida tu???
 
Ni yupi kati ya hao wawili atakuwa hana adabu kabisa- Aliyepaki gari mahali pasipostahili na bila hata kutoa taarifa ya kuomba exemption? au huyo kijana aliyetimiza wajibu wake kwa kuzingatia Taratibu alizopewa na boss wake?
Huyo dogo kazingua sana, kwa status ya utumishi aliyofikia Mahita katika taratibu za utumishi wa umma anakuwa immuned na priviledged to some regulations kama hizo.
Kufunga gari ya huyo Mzee ni kumfedhehesha na kutweza utu na status yake.
Achilia mbali status ya Mzee Mahita, inamaana huyo dogo ameshindwa hata kuheshimu tu umri wa huyo Mzee?
 
Wewe umetoa maoni ya kipumbavu sana. Nasema hivi kwa sababu USA hata uwe ex-president, na ukavunja sheria unashughulikiwa. Mahita kama ali-pack gari lake bila kufuata sheria ni kosa. Kama ana kibali cha kupaki bure alitakiwa akionyeshe baada ya kukuta gari limefungwa, as simple as that. Au kama anaruhusiwa kupaki lakini hatembei na kibali basi alitakiwa amwambie kiungwana yeye ni nani! Kuna tatizo gani kusema kuwa mimi ni fulani na naruhusiwa kupaki bila malipo? Hawezi kutumia silaha kwa mazingira kama haya. Ana bahati sana ingekuwa ni wakati wa Magufuli angekiona. Unakumbuka yule mke wa marehemu mahiga alimletea traffic police za kuleta Magufuli alichofanya? Eti ''amelika'' akili! Mawee! Haya manyang'au yaliyoharibu nchi ndiyo unasema yalilika akili? Alikuwa anafanya kazi ya kujitolea? Haya ni mawazo mgando sana.
 

Mkuu hii sukari kuipandisha hovyo sio salama kwa afya yako.maoni ni maoni tu hata uyaone ni ya kipumbavu yatabaki kuwa maoni tu.

Anyway dogo wa parking likuwa wapi mpaka mzee akatoa pistol??au unadhani alitaka kufunguliwa akagoma kisha akavunja kufuli??
 
Ila JPM aliweka nidhamu sana kwenye utawala wake. Mambo kama hayo ya kujifanya mimi Kingunge kwa kuvunja sheria za nchi na kujifanya doni alishayapoteza.
 
Narudia, hayo ni maombi ya kipumbavu. Huwezi kushabikia ex police officer kuvunja sheria kisa eti aliitumikia nchi. Hii siyo karne ya mawe. Aliyepaki gari ndiye mwenye makosa na huyo mkusanya ushuru alikuwa anatekeleza wajibu wake. Kama ana kibali cha free parking basi huwa vinawekwa ndani ya gari kwa mbele kwenye dashboard ili akija mkusanya ushuru akione. Kama anacho na hakuweka ni kosa lake. Kama hana basi anatakiwa kulipa kama raia wengine kwa sababu analipwa fedha nyingi sana kuliko raia wengi wanaolipa. Kilichonifanya niseme ni maoni ya kipumbavu ni wewe kusema eti mkusanya ushuru ana kosa kwa sababu alitakiwa ajue (sijui angeota) kuwa hilo ni gari la Mahita na aliache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…