DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ndiyo mshike adabu sasa! Siyo kukaa mnatunyanyasa sisi wazee! Hata mimi nikistaafu nitakuwa natembea nacho hadharani, ukileta ujinga tu nakuvunjavunja huto tu milonjo twako! Kwa nini wafunge gari ya igp mstaafu? Ina maana wao hawamjui?
 
Hayo madhara ya serikali ya ccm kuwapa watu vyeo kwa vigezo vya itikadi ya kisiasa. Huyo Mhita hakufaa hata kuwa coporal. ila kwasababu alikuwa mpenzi wa ccm akapewa cheo kwa masirahi ya chama.
 
🤣🤣🙌
 
𝐾𝑎𝑘𝑎 𝑚𝑛𝑎𝑘𝑒𝑟𝑎𝑔𝑎 𝑚𝑘𝑖𝑓𝑢𝑛𝑔𝑎 𝑚𝑎𝑔𝑎𝑟𝑖...𝑛𝑒𝑥𝑡 𝑡𝑖𝑚𝑒 𝑎𝑡𝑎𝑘𝑢𝑠𝑢𝑏𝑖𝑟𝑖 𝑢𝑤𝑒 𝑗𝑖𝑟𝑎𝑛𝑖 𝑛𝑑𝑜 𝑎𝑙𝑖𝑏𝑢𝑡𝑢𝑒 ℎ𝑖𝑙𝑜 𝑐ℎ𝑢𝑚𝑎 𝑙𝑎 𝑀𝑟𝑢𝑠𝑖
 
Mtu alishasema ni IGP mstaafu alaf unataka kuleta ligi. 😂😂😂😂😂😂
Hata kukupoteza hashindwi na hata akiulizwa ana "watu" Wa kumfunika.

Kibongo bongo sheria tumewekewa Sisi maskini. Viongozi wa serikali na matajiri wakubwa hizi sheria ndogo ndogo ni kama hazipo na haziwahusu.
 
Mkuu kufuli imevunjwa na x IGP,unaweza fungua kesi mtoza ushuru alipwe,kama itashindikana tukupe namba ya mahita umueleze kwamba kafanya jambo la hovyo,kutufokea sisi hapa badala umfate mwenyewe ni dalili ya ugonjwa wa moyo.
 
Huyo kijana alikwendaje kufunga gari ya mahita hana adabu kabisa
Kwani hiyo gari aliiegesha eneo gani na alikwenda wapi.Au kijana alifanya makusudi kwa kufanya wivu na hapo anapoingia IGP mstaafu.
Yawezekana kama ni 2000 mzee alikuwa tayari kulipa, lakini kijana kwa jeuri yake akawa anamchungulia kwa mbali ili amharibie ratiba zake.
 
Je, kama alikuwa hajui ni ya nani angelifanyaje? Hata huyo mwamba inawezekana alipishana na huyo kijana alipokuwa anakuja kwenye gari yake. Si hamjui au hawajuani?
 
Mkuu kufuli imevunjwa na x IGP,unaweza fungua kesi mtoza ushuru alipwe,kama itashindikana tukupe namba ya mahita umueleze kwamba kafanya jambo la hovyo,kutufokea sisi hapa badala umfate mwenyewe ni dalili ya ugonjwa wa moyo.
Sijafoka bali nimejadili. Nimechukuwa hii nafasi kukuelimisha ni nini maana ya utawala wa sheria. Kama hutaki maoni yako yapingwe basi jiondoe kwenye JF au uwe unasoma tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…