DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

DOKEZO Serikali imuangalie IGP Mstaafu Omari Mahita, anatoa silaha yake ovyo hadharani anaweza kumjeruhi mtu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ila dingi ni kama ana tatizo la akili la kukasirika hovyo😂 nasikia wakati wake alikuwa jambazi
 
Inaonekana kijana aliwaaminisha wenzake ngoja kwa niifunge gari ya mahita ... Nyie sini mnamuogopa.😁 Arafu kijana mwenyewe ni huyu huyu muanzisha mada hii..

Halafu makosa mengi kama hayo ya kufunga gari unakuta hata vile vibango vya Katazo havipo au kukiwepo kimeanzishwa makusudi ili usikione au kimewekwa mazingira ambayo si rahisi kukiona

Sababu wanajua kabisa watakosa hela..

Labda kwa taarifa kijana ambazo hazijui Omar mahita ni mtu hatari sana na aina ya wafu wenye misimamo mikali sana enzi zake za utumishi
Hili walifahamu watu wote, na wasilichukulie poa. Mahita mtu mpole ila hatari sana, enzi zake za utumishi hata sasa.
 
Nanukuu: "Mtu yyte lazma uijue gari ya huyu bwana, else wise ni dharau. Na hiyo ndio kazi ya bastola."
Mkuu, Hiyo gari yake ina utambulisho(Identity) gani wa kipekee kiasi kwamba mtu yeyote ni lazma aijue? Mbona ss huku umasaini ndani ndani huku hatuijui au sisi sio watu?
Je, kazi ya bastola ni kufungua lock za magari? Tafakari.
Huyo mwamba mstaafu inabidi ajitambue(Kama bado akili iko vizuri) kwamba ni muda wake sasa wa kupumzika na kuyafurahia mema ya nchi na sio kuendeleza ubabe. Wahenga walitanabahisha "Dunia huwatiisha watu".
1. Hiyo gari yaweza kutofanya kazi muda wowote e.g. kuharibika au vinginevyo;
2. Hiyo bastola sio mali yake - amedhaminiwa tuu i.e. anaweza kutakiwa kisheria airudishe kwa waliompa.
3. Kadri umri wake unavyosogea, anaweza kufikia umri ambapo asiweze tena kuvitumia hivyo vitu hata kama bado atakuwa navyo.
Ushauri: IGP (Inspector General Police) Mstaafu, kwa heshima alokuwa nayo (kabla na baada ya kustaafu) ndani ya Jamii ingependeza zaidi akawa ni mfano wa kuigwa na sio kuwa ni mtu wa vitisho na kuonesha umwamba.
Mahita ni mfano wa kuigwa morogoro, ndio ujumbe umefika kama amefanya tendo hilo, hata wahusika watakua wamempigia simu tayari.
Kingine i don't entertain politics kwenye comment yangu, siasa kaa nazo.
Nasijaongelea mm nyie washamba wa umasaini, nimesema morogoro haswa eneo analopaki yy gari yake.
Unaleta maswala ya masai hapa, nimetaja masai mm hapa.
 
Baada ya kustaafu, mzee huyu kwasasa anaishi mkoani Morogoro. Moja ya madoido yake katika uzee wake ni kuchomoa hadharani silaha yake ya moto (bastola) kila anapokerwa na mtu.

Miongoni mwa matukio ya ajabu aliyofanya ni kupiga risasi lock iliyowekwa kwenye gari yake baada ya kupaki sehemu isiyo sahihi.

Mzee alipaki gari yake binafsi, akaingia sehemu, alivyotoka akakuta gari imepigwa lock, akauliza ni nani kaifunga? Kwa mamlaka gani? Inamaana hajui gari yangu? Akachomoa bastola akaitandika ile lock ikafunguka bila kuathiri tairi, akaitupa huko, akaondoka!

Mwamba aliyeifunga aliogopa hata kusogea eneo la tukio.

Nikweli mzee ulikuwa nafasi ya juu sana, ila hilo lisifanye uishi kibabe mzee, mbona ma CDF wastaafu tunaishi nao fresh tu na wana unyenyekevu mkubwa?

Badilika.
😂😂
 
Ulisema mtu yeyote ni lazma..... Pia umesahau Jf haisomwi hapo moro tu.
Kama huyo mwamba ni mtu wa kuigwa Je, itakuwaje kama kila mwenye bastola hapo kwenu Moro akawa hivyo patakalika? au unataka kuniambia kwamba ili umudu kuishi hapo Moro ni lazima uwe mbabe?
nI sehemu gani kwenye komenti yangu kunaonesha Siasa?
 
Ulisema mtu yeyote ni lazma..... Pia umesahau Jf haisomwi hapo moro tu.
Kama huyo mwamba ni mtu wa kuigwa Je, itakuwaje kama kila mwenye bastola hapo kwenu Moro akawa hivyo patakalika? au unataka kuniambia kwamba ili umudu kuishi hapo Moro ni lazima uwe mbabe?
Soma tena , Mbwa wewe soma nilichoandika nimeandika morogoro, ukiona mtu yyte haina maana hadi ww uliyepo uliposoma huko, accha siasa mzee. Hujui ku think, hujui.
 
Miaka ya nyuma kidogo tulikuwa na mgonjwa pale hospital ya Taifa wakati tupo Tunasubiria muda ufike kuona wagonjwa kuna gari aina ya Prado ilifika na kupark eneo fulani akatoka mama mmoja wa makamo anaharaka kidogo akaondoka baada ya muda wakaja vijana wamevaa vile vizibao wakaja na minyororo wakafunga mwenzangu akauliza mbona mnafungia hii gari Katazo kipo wapi na mbona gari nyingine zipo hapa muda mrefu tangu asubuhi hamjazifunga wakajibu hili sio eneo la gari mwenye gari aje ofisini tukacheka na mwenzangu tukabaki Tunasubiria muda ufike ..
Baada ya dakika 30, mama yule akaja kuona gari yake imefungwa alichofanya ni kuchukua mkoba wake akatoa simu na kubonyeza namba fulani tukaona anaongea na simu kisha akakata simu akatoa simu nyingine akapiga tena .. baada ya dakika 10 zilikuja Gari 3 kwa speed kubwa sana . Gari 2 walishuka jamaa 4 waliopanda hewani wamevalia mavazi ya kijeshi na kijana mmoja ameshikilia zile mikasi mikubwa ya kukata makufuri/ minyororo

Wakakata kisha yule mama hakupanda ile gari akapanda gari nyingine ilioletwa ile aliokuja nayo akapanda mwingine zikaondoka..

Wale vijana waliofunga minyororo walipoona lile tukio walivua vizibao hawakusogelea lile eneo kwa Woga 😁

Vijana muwe makini katika kazi zenu mnaweza potezwa hivi hivi kwa kutengeneza mazingira ya rushwa na eneo lisilosahihi ao mnaowafungia ndio maboss wa. Maboss zenu

.. WEKA KATAZO ENEO LINALOONEKANA WEKA KAMBA ENEO LINALOKATAZWA Kujiepusha na aibu na kupoteza kazi . Hata huyo Boss wako atakukana kuwa na Lugha za kistaarabu unapomuelezea mtu kosa lake maana hujui unazungumza na nani ..
 
Jamaa amevurugwa
Nadhani sijavurugwa ila huyu analeta siasa.
Huwezi judge mtu kwa tendo la mara moja au mbili hiyo ni biasness. Unampaje mtu tabia ya hovyo.
Abood ana ubaya gani moro? Hana. Ila annaweza kuwa na matendo yasiyofaa yanayojulikana na mtu mmoja moja. We can't conclude his nature kwa hayo matendo.
 
M
Mkome kufungafunga magari ya watu, mimi natembea na ule mkasi mkubwa kwenye buti, nikiukiza wewe uliyefunga umefunga kwa mamlaka gani haujibu, nioneshe kitambulisho hauna, basi nakata loki yako natupa huko.
MZee ukizikata hizo lock usiwe unazitupa, weka kwenye buti zikifika kilo tano nitafute mkuu, nitaenda kuuza nitakupatia posho kidogo ya maji ya kunywa.
 
Baada ya kustaafu, mzee huyu kwasasa anaishi mkoani Morogoro. Moja ya madoido yake katika uzee wake ni kuchomoa hadharani silaha yake ya moto (bastola) kila anapokerwa na mtu.

Miongoni mwa matukio ya ajabu aliyofanya ni kupiga risasi lock iliyowekwa kwenye gari yake baada ya kupaki sehemu isiyo sahihi.

Mzee alipaki gari yake binafsi, akaingia sehemu, alivyotoka akakuta gari imepigwa lock, akauliza ni nani kaifunga? Kwa mamlaka gani? Inamaana hajui gari yangu? Akachomoa bastola akaitandika ile lock ikafunguka bila kuathiri tairi, akaitupa huko, akaondoka!

Mwamba aliyeifunga aliogopa hata kusogea eneo la tukio.

Nikweli mzee ulikuwa nafasi ya juu sana, ila hilo lisifanye uishi kibabe mzee, mbona ma CDF wastaafu tunaishi nao fresh tu na wana unyenyekevu mkubwa?

Badilika.
Kuna watu wanahitaji kutiwa adabu waheshimu wastaafu acha awape doscipline
 
Back
Top Bottom