Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

hata hao wa kwenu ni vilaza waliokaririshwa majibu, wajinga ndio waliwao. Hao watoto wenu wakifika vyuoni wanapigwa mbaya sana na hao wa shule za serikali, mnajilisha upupo tu na kuliwa mapesa kwa ulimbukeni wenu
 
Sasa povu lote hili la nini wewe bwege? Shule za serikali sio zza CCM pekee bali ni za watu wote. Mbona kama unataka kunipangia maisha. Kwa hiyo wanafunzi wanaosoma shule binafsi sio raia hawapaswi kutendewa haki kama watanzania? Mijitu yenye akili za kipuuzi kama wewe ndio mnasababisha serikali isiboreshe huduma za jamii. Ningekuwa na uwezo majitu kama wewe ningewanywesha sumu; bora mfe tu!.
 
Na serikali sikivu itaendelea na huu utaratibu hadi akili ziwakae sawa. Mwaka 2000 pale Ilboru kulijaa watoto wa Green Acres na shule nyingine za kishua hadi ikashangaza. Naona serikali imeshtuka. Utaratibu huu ni mzuri kama wanavyofanya HESLB. Mtoto wa St Kayumba apewe kipaumbele. Nyie wa private pelekeni watoto wenu sekondari za private acheni kulialia.
 
Mkuu usichanganye mada. Hapa tunaongelea selection ya form one 2024 lakini wewe umekimbia hadi HSLB. Unatafuta nini huko? Kuwa muelewa.

Wanafunzi huchaguliwa kwenda sekondari bora kulingana na ufaulu bora. Wewe unataka serikali yako ya kusadikika iendelee kuwachukua wanafunzi bora kutoka shule binafsi na kuwapeleka shule za kutwa za Kayumba badala ya kuwapeleka shule teule? Una akili kweli au akili zako umezisahau nyumbani?
 
Mkuu tumekuelewa na tumekufikia. Tunaomba sasa ujikite kwenye mada. Mbona unakuwa kama kuku anayetaka kutaga? Hutulii. Jikite kwenye hoja usizunguke tu kama kipepeo bila muelekeo.
 
SI mna Hela wapelekeni private
Rudia kusoma uzi uelewe hoja. Usikurupuke tu kama panya aliyekurupuliwa kutoka kwenye kibuyu. Majitu kama wewe mnaosapoti ujinga ndio mnasababisha serikali igome kuboresha huduma za jamii.
 
Acha kunililia mimi sio babako.
 
Watasubiri sana. Wapambane na hali zao. Wasitegemee ubwete wa kuandaliwa wanafunzi halafu waje kuchukua ujiko wa bwerere hapo baadaye.
 
Nimeshangaa sana hawa jamaa. Kuna dogo kijijini kwetu amepata wastani wa C mbovu kabisa eti amepangiwa korogwe girls alafu wale madogo waliopiga A wamepangiwa shule za kata. Duh
EQUITY!!!
 
Mara nyingi Wanafunzi waliosoma Private huwa hawaripoti kwenye shule walizochaguliwa hivyo inafanya shule kongwe kuwa na wanafunzi wachache,hivyo kwa muktadha huo serikali imeona ni bora tuwapeleke wanaohitaji na watasoma huko.!
 
Mara nyingi Wanafunzi waliosoma Private huwa hawaripoti kwenye shule walizochaguliwa hivyo inafanya shule kongwe kuwa na wanafunzi wachache,hivyo kwa muktadha huo serikali imeona ni bora tuwapeleke wanaohitaji na watasoma huko.!
Huu ni upumbavu..

Iko hivi, watoto wanajengewa foundation, vile sekondari ni lugha mpya kwa masomo yote.
 
Unajua ni kigezo gani kilitumika kufanya selection? pengine kigezo kilichotumika ni average ya marks na sio A zote
 
Binafsi sio muumini sana wa kukosoa wengine lakini, katika hili naomba niweke Sawa baadhi ya mambo machache kuhusu selection (kwa uelewa kiasi nilionao).
1. Si kweli kwamba kuna mwanafunzi kapata wastani wa B kaenda shule teule.( kama una ushahidi tuoneshe tafadhari)
2. Mwanafunzi apelekwi shule teule eti kwa sababu kapata wastani wa A, badala yake kuna factors nyingi sana mfano, A ya ngapi? Mtu kapata wastani wa A lakini A ya 98, lakini kuna mwengine kapata A ya 100, kama wapo kwenye kapu moja la uchaguzi, mwenye A ya 100 lazima achaguliwe.
Au watoto wamegongana wastani wote wana A ya 98 na wenye 99 na 100 wote wamechaguliwa kulingana na makundi yao, mwenye ufaulu mzuri zaidi katika somo la hisabati au Sayansi ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa shule teule kwa kigezo hiki.
Kwahiyo, shule X inaweza kuwa na A moja tu, lakini mwanafunzi akachaguliwa shule teule, na shule ikawa Z wakawa na A zote na wasipelekwe shule teule kulingana na uzito wa hiyo A. Tafadhari mtoa mada naomba ujiridhishe katika hili.
3. Uwiano ni jambo la msingi ndio maana hata jinsia huzingatiwa, walemavu n.k hivyo basi, hakuna namna utakayokwepa kuweka some standards kulingana na makundi mbalimbali. Ubaya ni pale tu unapoweka double standards kwa watu wa kundi moja.
Hivyo basi, nionavyo mimi unapoamua kuilamu Serikali au viongozi kutokana na maamuzi wanayoyafanya katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku, ni vyema tukawa na ushahidi usiokua na chembe ya mashaka hasa katika hili la selections.

Ahsante.
 
Hapa Tunachotakiwa kuilaumu serikali Ni kutokuboresha mazingira mazur gov schools
Lakini serikali ikishindwa kuboresha mazingira ya kusomea badala yake ikaboresha mazingira ya selection ya wanafunzi wa shule ya kata wewe unaona ni haki mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…