Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Kwahiyo ndo unamuacha wa A kwenda shule maalumu unampeleka wa C kisa katoka kayumba ya serikali? Hao baadhi wanaokwenda huko, kwanini wasiwe wa A bila kujali anatoka private au kayumba?
 
Serikali imejenga shule nyingi, lakini watu hawaziamini wanapeleka watoto shule private. Sasa wanachofanya serikali .shule zoote private zinazopokea ada ya chini ya milioni ukipeleka mtoto wako umeliwa mana zinaminywa makusudi kuanzia ufauru nk.

Labda umpeleke private ya kuanzia milioni 3 kwenda juu kwa levo ya og hadi advance. Na mtu anaeweza kumudu ada ya hivyo anaweza pia kumudu hadi galama za chuo kwa kulipia bila ya mkopo. Hivyo watu wachini tuwe makini juu ya hili.a
 
Opinions za watu wote hawa kama hujapata kitu kwenye hizi selections basi ww ni 'mbishi kufa'
Wewe umeelewa nini? Hebu weka hapa ili twende sawa. Inaonekana hata wewe hujapata kitu. Mimi ninachofahamu ni kwamba selection is and should be based on MERIT and nothing else. Kufanya vinginevyo, huo ni UBAGUZI. Wewe unataka nikubaliane na ushauri wa watu wanaoshabikia ubaguzi wa waziwazi? Mimi sio kilaza wa kiwango hicho.
 
Utafiti hukosolewa kwa utafiti. Kama unaona utafiti haujakamilika, basi wewe nenda kafanye utafiti wako makini utuletee majibu hapa mkuu. Vinginevyo ukae kimya. Huna hoja,
Mkuu utafiti wako hautoshelezi.

Kwanza- Mbele ya yote, huna uwezo wa kuninyamazisha, na hiyo ukae ukijua. Huna.

Pili, Hoja yangu ipo wazi kabisa.
  • huna weledi
  • huna elimu ya kufanya utafiti wa aina hiyo(correct me if i'm wrong)
  • huna ushahidi wowote ule, halali au hoja yeyote ile ya kuunga mkono madai yako kwamba serikali inawabagua wanafunzi wa shule za private.

Siwezi kukaa kimya kamwe kama kuna watu kama wewe mpo hapa kuulaghai Umma wa Watanzania.

Hatahivyo ukweli utabakia pale pale....kwamba...

Huu si utafiti. Ni kasfha..
 
No research, no right to speak. Mimi nimefanya utafiti wangu nime analyse matokeo ya utafiti na kutoa conclusion.

Sasa wewe kama unaona kuwa utafiti wangu haujitoshelezi, usipinge kwa maneno matupu bali pinga kwa kufanya utafiti mpya utakaotoa majibu kinzani kisha wanajukwaa wenyewe watafanya comparative analysis na kuchuja ukweli.

Usidhani kila mtu ni mjinga umuambie maneno matupu akuelewe wakati ukweli wote nimeuanika hapa. Utasubiri sana.
 
Somesha mtoto huko acha lialia kwani serikali ndoilimwaga ikakaza tako na vidole vyamiguu?? msituchoshee bhana aah!!
Nawe acha bangi zako mkuu. Changia mawazo kulingana na uzi, matusi sio mchango bali yatasababisha upigwe ban na mods.
 
Ukifuatilia haya mambo unaweza kulia kabisa, mtoto wangu alimaliza 2022, shule binafsi iko tabata- bonyokwa wanafunzi 93....ktk 93 waliokuwa na wastani wa B walikuwa watatu tu, lkn wanafunzi wote walipangwa Bonyokwa sekondari na mvuti sekondari shule za kata
 
Serikali ina mambo ya kipumbavu huwezi kuamini mkuu. Inauma sana.
 
Siasa nyingi sana,,,mitihani inanunuliwa sana ,,,unakumbuka ile shule imefutiwa matokeo kwa wanafunzi wote katika shule za halimashauri ya chemba ,mwanza jiji pia shule ya tumaini na little flower huu ndo uthibitisho wangu huko private hakuna lolote ni upupu tu bisha na hapa pia
 
Nilishangaa mwaka jana mwanangu kwenye mtihani wa drs la saba alipata alama A katika masomo yote,lakini cha ajabu alipangiwa shule ya kata tena ya kijijini ya kutwa!
Ulitaka aende wapi wakati huyo popoma tu,,,saizi huko sekondari ana A ngap?
 
Habari zenu jamani,Naomba kuuliza kuna dogo jirani yangu kamaliza mwaka jana darasa la 7 matokeo yake ana wastani wa D,Majibu ya kuchaguliwa kwenda sekondari jina lake halipo sijajua iyo D ni amefeli ama vipi,na kama amefeli kwa wastani wa D je chaguo la pili anaweza kupangiwa shule ya sekondari,uyo mtoto wazazi wake hawana kabisa uwezo wa kumpeleka shule ya private,
 
Sasa miaka hii kupata A si kawaida unataka mtoto apelekwe wapi wakati ana A nyepesi za 41 wenzie wana 50
Lete ushahidi, otherwise ukae kimya milele. Darasa zima la wanafunzi 98 wote wamepata A za 41? You must be lunatic!
 
Napenda utaratibu wa Kenya,wao wanaweka Marks sio huu utaratibu wa Grade,hiki wanachofanya baraza ni kuua ushindani madhara yake hayana tofauti na madhara ya ujamaa
Kenya inajulikana kabisa mwanafunzi mwenye marks fulani basi yeye atapangiwa Alliance
 
Napenda utaratibu wa Kenya,wao wanaweka Marks sio huu utaratibu wa Grade,hiki wanachofanya baraza ni kuua ushindani madhara yake hayana tofauti na madhara ya ujamaa
Kenya inajulikana kabisa mwanafunzi mwenye marks fulani basi yeye atapangiwa Alliance
Kweli kabisa mkuu. Zamani NECTA hawakuwa na grading system ya ovyo kama hii wanayofanya sasa hivi. Utaratibu huu wa MamaSamia2025 na chawa wake chawa wa mama umechangia mno kudidimiza elimu yetu; umepunguza morali ya kufundisha na kujisomea. Nchi ya kiqumer sana hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…