Wamezingatia EQUITY !!!Huwezi kulinganisha ufaulu wa Kagera na Mtwara au Lindi na Mbeya au Katavi na Kilimanjaro.
Huwezi kuweka mizani sawa hata siku moja. Kata ya Umasaini iwe sawa na kata ya Dsm! Nooo!!
Mimi si mmoja wao. Ni fikra zangu zinanifikirisha hivyo
Mkuu umetoa ushuhuda na ushauri mujarab! 👍👏🙏Na mimi nitaelezea uzoefu wangu katika swala hili la selection kwa kidato cha kwanza. Jambo hili naweza kusema kwamba halijaanza leo, linaweza kuwa limeanzia tangu miaka ya 2008 na litaendelea. Kwanini nasema hivi? Sababu ni hii mimi mwenyewe nilikumbwa na kadhia hii hii japo nilisoma shule ya serikali. Matokeo yetu ya shule ya msingi yalikuwa mazuri mno kwani shule yetu ilikuwa inafahamika kwa kufaulisha vizuri. Lakini lilipokuja swala la selection za kidato cha kwanza hadi waalimu pale shuleni walibaki kushangaa. Kwani kwa ufaulu nilioupata na kupelekwa shule ya kata nilipofika kule nilishangaa. Nilitegemea kupelekwa shule ya mkoa kama si wilaya. Kwani kuna wanafunzi waliokuwa na ufaulu kama wangu wa shule nyingine na walipelekwa shule za mkoa au wilaya. Na kibaya zaidi aliyefaulu kwa ufaulu wa juu zaidi pale shuleni kwetu aliishia kupelekwa Azania wakati mdada aliyemfuata ndiye aliyepelekwa Shule ya Vipaji yaani Kilakala. Kwa kweli ilikuwa ni sintofahamu sanaa. Kwahiyo nataka kusema hili swala kwa sasa hv ndo linaanza kuonekana ukubwa wake. Lakini lilianzia miaka ya nyuma kabisa. Kuwa na amani, muhimize kijana wako asome kwa bidii katika shule aliyochaguliwa atafaulu, au laa ukiona haujaridhika baadae umuhamishie shule nyingine ya serikali utakayoona ina uhafadhali kuliko hiyo. Shule za Kata zimekuwa zikitazamika vibaya katika jamii zetu kutokana na miundombino pamoja na vitendea kazi vya kufundishia lakini pia na aina ya wanafunzi wapelekwao huko. Wengi wao wanakuwa ni wale wasindikizaji hili linazidi kuzifanya shule hizi kuzidi kudharaulika lakini, wewe kama mzazi lisikuvunje moyo mpambanie mwanao na atafanikiwa. Mimi nilifaulu vizuri kuliko hata baadhi ya waliopelekwaga shule za mkoa na wilaya sijisifii lakini natoa ushuhuda.
Mkuu unapaswa kuzingatia pia mazingira ya usomaji Kati ya private na kayumbaKwa hiyo kumbe selection haifuati ufaulu bali inafuata uwiano kama vile Tanganyika inavyowiana na Zanzibar? Hii kali aisee!
Hebu tufafanulie kidogo mkuu huenda unakuwemo kwenye selection board. Huwa mnachagua kwa kutumia muongozo kutoka juu bila kuzingatia ufaulu?
Mkuu sio analilia ni anadai haki yake kwa sababu hizo shule teule zimejengwa kwa kodi za wananchi wote na ya kwake ikiwemo, wewe vipi mkuu???Hao wa Private si waende shule za Private.. mbona Unalilia shule teule za Serikali..? Huwezi kumpangia Mmiliki
Halafu matokeo yake hawahawa wenye uwezo mdogo ndio wanaokuwa watumishi wa serekali, hii ndio inapekelekea mambo ya serekali kuendeshwa kwa maguvu na akili kidogo, huku kukiwa na ufanisi duni.Kuna mdau aliandika humu, hakuna kitu hata kimoja ambacho serikali inafanya kwa ufasaha na usahihi. Ni kuunga unga tu mradi pakuche
Inawakatisha sana tamaa, Tunazalisha wakandarasi wanaojenga kituo cha mwendokasi katika ya Jangwani na wanaona sawa maana walibebwa na hawajui kitu.Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.
Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.
Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.
Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392
Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!
Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Hao wenye D shule za Kata Form four wanapiga division 4 wanaingie ile chuo kikuu kipo Moshi kina wakurya wengi sijui kinaitwa sisipii .Halafu matokeo yake hawahawa wenye uwezo mdogo ndio wanaokuwa watumishi wa serekali, hii ndio inapekelekea mambo ya serekali kuendeshwa kwa maguvu na akili kidogo, huku kukiwa na ufanisi duni.
Na wengi wa hao vilaza hutokea kuwa makada wa ccm, Hadi uzee wao unakuta wanategemea Hila tu maana wamelelewa kwa njia ya mbeleko. Wengi wa watu wenye akili huru ni adui waccm, ndio sababu ya huo upendeleo kwa vilaza.
Halafu matokeo yake hawahawa wenye uwezo mdogo ndio wanaokuwa watumishi wa serekali, hii ndio inapekelekea mambo ya serekali kuendeshwa kwa maguvu na akili kidogo, huku kukiwa na ufanisi duni.
Na wengi wa hao vilaza hutokea kuwa makada wa ccm, Hadi uzee wao unakuta wanategemea Hila tu maana wamelelewa kwa njia ya mbeleko. Wengi wa watu wenye akili huru ni adui waccm, ndio sababu ya huo upendeleo kwa vilaza.
nimewaza labda wanaangalia wastani;
Marks Grade 00 - 10 F 11 - 20 D 21 - 30 C 31 - 40 B 41 - 50 A
CCM inahofia uwekezaji makini kwenye elimu kwamba watakuja kuanguka kwenye chaguzi.Serikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.
Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.
Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.
Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392
Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!
Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Selection ipo SawaKwa hiyo unataka kusema nini kuhusu selection inayofanywa na serikali ya CCM?
Mkuu umekasirika sana...Mfumo wa elimu wa Tanzania ni outdated na elimu inayotolewa na mfumo huo ni ya dark ages ndo maana nchi haiendi mbele.Hakuna shule ya serikali inayotoa elimu bora bila kujali ikoje na ipo wapi,hata malalamiko yako nayaona hayana msingi kwa sababu anaesoma kata au hiyo spesho wote wapo chini ya mfumo uleule uliofeli. Shule za kata, bweni, teule, spesho kote ni full ujinga uleule,we unapelekeshwa na majina ya shule.
Uko sahihi lakini lazima serikali ifanye juhudi za kuboresha shule za umma ili kiwango cha ufaulu kilingine na wale wa private kwani kwa sasa tofauti ni kubwa mno.Waone private wanafanya investment gani mpaka wanafaulu kwa rate kama ileHizo shule teule ni chache mpendwa! Ukisema utumie vigezo unavyovisema wewe maanake kwanza hazitatosha kwa hiyo uwiano ni mhimu ili kila upande upate! Kinachofanyika shule za private zina nafasi zao za kwenda huko hivyo hivyo na shule za umma zina idadi yao! Kutokana shule za private ni wengi wanafaulu ndo maan wanagawana wawili wawili mkuu! Shule za umma wanaofaulu kwa ufaulu wa juu ni wachache ndo maana wale wanaofaulu kwa kiwango hata cha B wanabahatika maana nafasi zao wengi hawafaulu kwaviwango vya juu!!
Sio kila kitu kuilaumu serikali mambo mengine tunapaswa kuipongeza
Unadhani!?Nadhan serikali pia imezingatia hilo