EMMYGUY
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 11,099
- 25,347
Mkuu Mpwayungu Village, njoo na Walimu wenzako mtusaidie hili.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hao wenye D shule za Kata Form four wanapiga division 4 wanaingie ile chuo kikuu kipo Moshi kina wakurya wengi sijui kinaitwa sisipii .
Na mie nahisi hivyo pia.nimewaza labda wanaangalia wastani;
mwenye 50,50,50,40,40(atachukuliwa ana A tatu, B mbili) ana wastani mkubwa kuliko mwenye 41,41,41,41,41(atachukuliwa ana A tano)
ni mfano tu, ila inaonesha inawezekana.
Hayo ni matumizi mabaya ya resources.Mwanafunzi akiwa na alama nzuri kwenye mitihani yake asahau kwamba kuna siku atakuja kuwa askari.Akiwa na four mbaya njia nyeupe kwani anafaa kulinda BankSilabasi yao "hairuhusu rizoningi" !
Wakikukamata wanakwambia "utajieleza huko huko Mbele"
Unachoma mafuta toka Dar kwenda Arusha kumkamata Lema, wakati ukimpigia Simu anakuja mwenye kituoni.
Serikali haina akiliMkuu Mpwayungu Village, njoo na Walimu wenzako mtusaidie hili.
Hapa Tunachotakiwa kuilaumu serikali Ni kutokuboresha mazingira mazur gov schoolsMkuu labda hujanielewa vizuri. Hapa tunaongelea slection ya wanafunzi na hii haihitaji mtu kuwa tajiri, mbinafsi au mchoyo ili mtoto wake achaguliwe. Wanafunzi inafaa wachaguliwe based on MERIT. Hiki ndicho kigezo cha kitaalua kinachotakiwa kufuatwa. Lakini sasa serikali imeacha kuchagua wanafunzi kwa kigezo cha UFAULU badala yake wanaangalia MAZINGIRA ya kufundisha. Hii ni mentality ya kipumbavu sana.
Hili ni jibu lenye kueleweka.Hizo shule teule ni chache mpendwa! Ukisema utumie vigezo unavyovisema wewe maanake kwanza hazitatosha kwa hiyo uwiano ni mhimu ili kila upande upate! Kinachofanyika shule za private zina nafasi zao za kwenda huko hivyo hivyo na shule za umma zina idadi yao! Kutokana shule za private ni wengi wanafaulu ndo maan wanagawana wawili wawili mkuu! Shule za umma wanaofaulu kwa ufaulu wa juu ni wachache ndo maana wale wanaofaulu kwa kiwango hata cha B wanabahatika maana nafasi zao wengi hawafaulu kwaviwango vya juu!!
Sio kila kitu kuilaumu serikali mambo mengine tunapaswa kuipongeza
Huwa wanachukua 60 bora ya wilaya, ke 30 na me 30 wanapelekwa hizo shule, wakati wangu ndo tuliambiwa utaratibu huo, sijui kwa sasa.Kivipi mkuu? Hebu fafanua zaidi.
Wanaochaguliwa hawaend,nafas znabak vacant wanaanza kuokoteza wabovu,wanaohamia na watovu wa nidhamu wanaohamia toka shule mbalimbali ilimradi tu shule zisikose wanafunziHuwa hawaendi kwan, ndo maana serikali imeamua kuwachukua wahitaji
Mi nmesoma pia technical schoolKumbe kusoma shule ya bweni, ufundi, special kwa o level ni bonge LA deal? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuanzia leo natembea kifua mbelee, nimesoma bweni O level.
Weuweeeeee!!!
Kwenda special schools ni swala la bahati tuSerikali hii ya CCM ina mambo ya ajabu sana. Ni aibu kwa serikali inayojinasibu kuzingatia usawa kufanya uhuni wa kiwango hiki. Sijawahi kuona serikali yenye ubaguzi mkubwa kwa wananchi wake hapa ulimwenguni kama serikali ya CCM.
Katika uchaguzi wa wanafunzi watakaojiunga kidato cha kwanza mwaka 2024, serikali imeonyesha ubaguzi wa waziwazi kati ya wanafunzi wa shule za kata na shule binafsi. Hii tabia ya kibaguzi haifai hata kidogo. Tukumbuke kwamba kuna wazazi wa watoto wanaosoma shule binafsi ambao wangependa watoto wao waendelee na masomo katika shule za umma. Inasikitisha serikali imeamua kukatisha ndoto hizo kwa makusudi.
Nitatoa mifano hai ili kuthibitisha hili ninalosema hapa. Nimechukua sampuli ya shule mbili kutoka kata moja (moja ya serikali na nyingine ya binafsi) ili kuuonyesha umma wa watanzania jinsi serikali ya CCM ilivyojaa ubaguzi wa kipuuzi uliopindukia. Lengo la kuchukua shule kutoka kata moja ni la kitafiti zaidi…..kwamba wanafunzi wote wanatoka eneo moja lenye mazingira yanayofanana; hivyo hakuna sababu ya kuwabagua.
Tazama matokeo ya shule hii binafsi jinsi wanafunzi wake walivyofanya vizuri: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206131.htm
View attachment 2848392
Linganisha matokeo hayo na haya ya shule ya kata: https://matokeo.necta.go.tz/results/2023/psle/results/shl_ps0206125.htm
View attachment 2848390
Utaona idadi ya A kwenye shule binafsi ni 58 huku shule ya kata wakiambulia 9 tu!
Sasa njoo kwenyye uchaguzi wa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule za sekondari mwaka 2024. Serikali imechagua wanafunzi 2 waliopata A tu kutoka shule binafsi kwenda shule teule. Wengine wote waliosalia wamerundikwa kwenye shule za kata za kutwa kama mnavyoona.
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Na pia wamechaguliwa wanafunzi 2 tu kutoka shule ya serikali iliyofanya vibaya na wanafunzi hao wamepata B mbili katika masomo yao. Haki iko wapi?
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, 2024
Kama serikali ingekuwa inafuata haki, wanafunzi wote 58 kutoka shule binafsi wangechaguliwa kwenda shule teule. Lakini kwa kuwa ubinafsi na upendeleo umetawala ndani ya roho zao za kutu, wameamua kuchagua wanafunzi 2 tu ili kufunika kombe mwanaharamu apite. Serikali hii ina mambo ya kijinga sijapata kuona.
Du! Hii ni mbaya sana. Wanavyofanya utadhani kila wilaya inatunga mtihani tofauti. Serikali hii ina mambo ya kijinga sana.Huwa wanachukua 60 bora ya wilaya, ke 30 na me 30 wanapelekwa hizo shule, wakati wangu ndo tuliambiwa utaratibu huo, sijui kwa sasa.
Serikali inapaswa kuwa ya wananchi na itekeleze matakwa au mahitaji ya wananchi.Mkuu acha uvivu....pitia hayo matokeo uone uovu wa serikali yako. Wanafunzi waliopata B wa shule za kata wameenda shule teule huku wanafunzi waliopata A wa shule binafsi wamepelekwa sjule ya kata Changanyikeni. Huu ni ujinga usiovumilika. Acha kutetea uhuni na upuuzi wa serikali ya CCM.
Nimekuelewa sana ulichomaanisha na mimi nasupport serikali kwa hicho walichoamua nadhani hata kuna miaka fulani nyuma wanafunzi toka private ilikuwa ngumu sana kupewa mikopo ya elimu ya juu japo nami nili apply na niikanyimwa cha ajabu mzee wangu alifurahi sisi kutokupewa mikopo naweza kuwa sikumwelewa kipindi kile lakini kadri miaka ilivyokuwa inakwenda nikawa namuelewa mzee wanguMkuu labda hujanielewa vizuri. Hapa tunaongelea slection ya wanafunzi na hii haihitaji mtu kuwa tajiri, mbinafsi au mchoyo ili mtoto wake achaguliwe. Wanafunzi inafaa wachaguliwe based on MERIT. Hiki ndicho kigezo cha kitaalua kinachotakiwa kufuatwa. Lakini sasa serikali imeacha kuchagua wanafunzi kwa kigezo cha UFAULU badala yake wanaangalia MAZINGIRA ya kufundisha. Hii ni mentality ya kipumbavu sana.
Ni vile ambavo unabehave ...Yametoka wapi yote Ayo mkuu?
Nadhan Tungejikita Kwny kujibu hoja za mtoa mada bila jazba badala ya kushambuliana sisi kwa sisi personally.
Yani kifupi ni kwamba CCM mtaji wao ni wajinga..makapuku...masikini...walala hoi..mahohehahe...Serikali hii inaamini kwamba, watoto wanaosoma shule za private wazazi wao Ni wafuasi na wanachama wa chadema na wanaosoma shule za kanumba wazazi wao Ni wafuasi na wanachama wa CCM.
Wanahisi wakiwachagua waliotoka shule za kulipia wanawapa ujiko chadema.