Serikali inawabagua wanafunzi wa shule binafsi; ushahidi huu hapa

Silabasi yao "hairuhusu rizoningi" !

Wakikukamata wanakwambia "utajieleza huko huko Mbele"

Unachoma mafuta toka Dar kwenda Arusha kumkamata Lema, wakati ukimpigia Simu anakuja mwenye kituoni.
Hayo ni matumizi mabaya ya resources.Mwanafunzi akiwa na alama nzuri kwenye mitihani yake asahau kwamba kuna siku atakuja kuwa askari.Akiwa na four mbaya njia nyeupe kwani anafaa kulinda Bank

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Hapa Tunachotakiwa kuilaumu serikali Ni kutokuboresha mazingira mazur gov schools
 
Hapa Tunachotakiwa kuilaumu serikali Ni kutokuboresha mazingira mazur gov schools
That is right. Kwa hiyo wakati huu ambao bado hawajaboresha shule za kata waendelee na huu mchezo wao wa ubaguzi kwenye selection?
 
Hili ni jibu lenye kueleweka.
Hata hivyo, serikali iongeze na kuboresha shule zote badala ya kuwepo teule chache.
Ifahamike kuwa, wazazi wanaosomesha watoto shule binafsi wanaisadia serikali kubeba gharama na kuboresha mfumo wa elimu.
Fikra kwamba ni matajiri na kwamba watoto Hao waonekane tofauti katika mfumo wa serikali ni potofu kabisa.
 
Kumbe kusoma shule ya bweni, ufundi, special kwa o level ni bonge LA deal? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuanzia leo natembea kifua mbelee, nimesoma bweni O level.
Weuweeeeee!!!
 
Huwa hawaendi kwan, ndo maana serikali imeamua kuwachukua wahitaji
Wanaochaguliwa hawaend,nafas znabak vacant wanaanza kuokoteza wabovu,wanaohamia na watovu wa nidhamu wanaohamia toka shule mbalimbali ilimradi tu shule zisikose wanafunzi

Ndo maana skuhz shule teule hazifanyi vzur sn Kama miaka ya zamani maana zinachanganyiwa Sana makapi
 
Kumbe kusoma shule ya bweni, ufundi, special kwa o level ni bonge LA deal? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuanzia leo natembea kifua mbelee, nimesoma bweni O level.
Weuweeeeee!!!
Mi nmesoma pia technical school
Pia ndoto yangu wanangu wote wapitie uko. Kule sio TU anapata shule, bali Mtoto anafundishwa kazi, maisha na kujitegemea kiujumla.
 
Kwenda special schools ni swala la bahati tu


Wanaopata A ni wengi mno hivyo hawawezi wote kuzingatiwa

Hata form four hivyo hivyo watu wanapiga one kali na wanapelekwa A level shule za kawaida
 
Huwa wanachukua 60 bora ya wilaya, ke 30 na me 30 wanapelekwa hizo shule, wakati wangu ndo tuliambiwa utaratibu huo, sijui kwa sasa.
Du! Hii ni mbaya sana. Wanavyofanya utadhani kila wilaya inatunga mtihani tofauti. Serikali hii ina mambo ya kijinga sana.
 
Serikali inapaswa kuwa ya wananchi na itekeleze matakwa au mahitaji ya wananchi.
Habari ya huduma kama elimu, maji, afya, umeme,... inatakiwa iamuliwe na wananchi wenyewe na serikali itekeleze.
Tuendelee kuwaelimisha wananchi ili waweze kujiamulia mambo yao wenyewe na kuidhibiti au kuiondoa serikali isipotekeleza.
 
Iko hivi katika uchaguzi wanaangalia vigezo kadhaa

1,masomo matatu ambayo ni hisabati, English na sayansi awe amepata daraja A positive yaani 46+

2, Continue assessment tangu akiwa darasa la 4

3,Tabia na mienendo ya mwanafunzi mfano kama amejaziwa tabia ni wastani imekinzana na A zake
 
Nimekuelewa sana ulichomaanisha na mimi nasupport serikali kwa hicho walichoamua nadhani hata kuna miaka fulani nyuma wanafunzi toka private ilikuwa ngumu sana kupewa mikopo ya elimu ya juu japo nami nili apply na niikanyimwa cha ajabu mzee wangu alifurahi sisi kutokupewa mikopo naweza kuwa sikumwelewa kipindi kile lakini kadri miaka ilivyokuwa inakwenda nikawa namuelewa mzee wangu

Kuna vijana wengi sana wa kimaskini wamekosa nafasi za kwenda shule bora na hata shule za vipaji kuendeleza vipaji vyao kwa kubase kwenye marks/matokeo au kwasababu hakusoma shule bora.

Nimekulia maisha ya kati lakini kuna vijana zaidi ya watatu ambao nimekua nao ambao nikiri kuwa walikuwa wanasoma shule X shule ambayo ilikuwa haina hata madawati na walikuwa kwa mwaka mzma wanavaa shati moja daftari zmejaa jasho.

Lakini kipindi hicho kulikuwa kuna walimu katika shule nuing ambao walikuwa wanafanya kazi za ualimu lakini walikuwa ni watu wa system sjui kama siku hizi bado ipo hivyo au la.

Basi maisha yakaendelea wakaenda tabora boys hivi sasa wawili ni captain wa jeshi na hawa watatu ni marubani wa air Tanzania.

Kilichonisukuma kuandika haya yote ni kwa sababu hiyo shule ya msingi niliyosoma miaka hyo ninavyozungumza mpaka leo hii hali ya ile shule iko vile vile,kuanzia mazngira magumu ya kufundishia na hata hali ngum za maisha ya watu wa maeneo hayo.

Je serikali ikisema ifate results/au ubora wa elimu kwa shule fulani je hawa maskini ambao hela tu ya kula au kununua madaftari wataweza kuwekwa fungu moja na wenzao wanaolipiwa 10m+ kwa mwaka?

Na hapo tutakuwa tunatengeneza gape gani kwa walionao na wasio nacho?

Au ndo tutegemee hawa wachini kuona wao ni watengwa na kuacha kuamini kuwa elimu si ufunguo wa maisha na kuamua kuachana nayo je unajua what will happen after 20 years later?
 
Yani kifupi ni kwamba CCM mtaji wao ni wajinga..makapuku...masikini...walala hoi..mahohehahe...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…