Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 4,994
- 9,625
Wana-Jamii Forums salamu,
Kama mnavyofahamu, nchi imeshuhudia taharuki na usumbufu mkubwa kufuatia mgomo wa ghafla wa madereva wa mabasi ya mikoani na malori unaopinga utekelezaji wa mfumo mpya wa Jeshi la Polisi wa kukata pointi kwenye leseni za udereva kila wanapofanya makosa.
Binafsi nasema, Serikali isitii kabisa matakwa ya mgomo huu na isirudi nyuma kwenye msimamo wake. Kufanya hivyo ni kuzidi kuhalalisha uzembe na kuhatarisha maisha ya abiria na mali zao barabarani.
Hebu tuangalie ukweli bila kumung'unya maneno:
1. Uzembe uliokithiri na "Kamari" ya Ligi za Barabarani
Madereva wa mabasi ya mikoani wanaongoza kwa kufanya makosa ya kijinga na ya kizembe barabarani. Wengi wao wanafanya overtake za hovyo kwenye milima, kona, na maeneo yenye mstari mmoja ulionyooka bila kuzingatia sheria wala kanuni zozote za usalama.
Inasikitisha sana kuona pindi mabasi yanapotoka stendi kuu ya Mbezi Magufuli kwenda mikoani, au kutoka mikoani kuja Dar es Salaam, madereva hawa na wadau wao wanageuza maisha ya watu kuwa kamari. Kuna ujinga wa hovyo unaoitwa "Ligi za Barabarani / Ligi za wanazi " ambapo wanashindana mbele ya abiria kuona basi gani linakimbia zaidi au gari gani litawahi kufika. Huu ni upumbavu uliopitiliza na watanzania tumechoka kuzika ndugu zetu kila siku kwa sababu ya sifa za kijinga za watu wachache. Faini ya fedha pekee imeonekana kutofua dafu kwa sababu wamiliki wanazilipa, lakini mfumo huu wa pointi unamwajibisha dereva mmoja mmoja binafsi ili anyooshe nidhamu yake.
2. Kulinda Maisha ya Wananchi vs Maslahi ya Madereva
Kugoma kisa tu unalazimishwa kufuata sheria ni utovu wa nidhamu. Dereva anayejiamini kuwa anafuata sheria na kuheshimu alama za barabarani anaogopa nini kukatwa pointi? Ni wazi kuwa wanaogopa kwa sababu wanajua hawana nidhamu barabarani. Serikali isikubali kuwekwa mtu kati na kikundi cha watu wanaotaka kupewa leseni ya kuendelea kuua raia wetu kwa uzembe.
3. Mfumo wa Pointi ni Suluhisho la Kimataifa (Mifano ya Nchi Zilizofanikiwa)
Mifumo hii ya point-deduction inatumika duniani kote na imethibitika kisayansi kupunguza ajali kwa zaidi ya 21% na vifo kwa 10%.
Uingereza na Ujerumani: Zina mifumo madhubuti ya pointi ambapo dereva akifikisha kiwango fulani cha makosa, leseni inafungiwa kiotomatiki na anarudishwa chuo kusomea upya udereva. Hii imesaidia kuwa na madereva wenye nidhamu ya hali ya juu barabarani.
Italia
(Ukanda wa Veneto): Utafiti unaonyesha tangu kuanzishwa kwa mfumo huu, zaidi ya vifo 1,500 na majeraha ya barabarani zaidi ya 91,000 yaliepukwa kwa sababu madereva walianza kuogopa kupoteza leseni zao.
Ushauri wangu kwa Serikali: Leteni Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kwa Askari
Ili kuondoa malalamiko ya madereva kudai kuwa wanaonewa au kubambikiziwa makosa, na ili kudhibiti mianya ya rushwa barabarani, nashauri serikali iweke utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwa na Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kama wanavyofanya mataifa makubwa.
Teknolojia hii itarekodi mazungumzo na matukio yote kati ya askari na dereva papo hapo:
Mataifa kama Marekani na Uingereza: Matumizi ya kamera hizi yamesaidia kupunguza malalamiko dhidi ya askari kwa takriban 16% hadi 17%. Kamera iko wazi, hivyo dereva hawezi kutoa rushwa na askari hawezi kuomba rushwa wala kumbambikizia dereva kosa kwa sababu kila kitu kinakuwa na ushahidi wa video na sauti. Hii inaleta uwazi na haki kwa pande zote mbili.
Wito wangu kwa Serikali:
Kaeni chonjo na shinikizo la mgomo huu. Tukirudi nyuma sasa hivi, tutakuwa tumefungulia milango ya ajali zaidi, vifo, na ulemavu usio na lazima barabarani. Sheria ikazie hapo hapo, na yeyote anayeona hawezi kufuata sheria, aachie usukani akafanye kazi nyingine.
Usalama wa abiria na mali zao kwanza!
Pia soma:
~Dereva alalamika Askari wa barabarani kuwakatia Point kwenye leseni
~Mfumo wa Pointi Leseni: Usawa Wapi?
~Serikali isirudi nyuma: Mfumo wa kukata pointi kwenye leseni usisistishwe, migomo isitumike kuchezea maisha ya abiria barabarani
~Makosa ya barabarani na point zake zitakazowekwa kwenye leseni. Kila leseni itakuwa na jumla ya pointi 15