Serikali isirudi nyuma: Mfumo wa kukata pointi kwenye leseni usisistishwe, migomo isitumike kuchezea maisha ya abiria barabarani

Serikali isirudi nyuma: Mfumo wa kukata pointi kwenye leseni usisistishwe, migomo isitumike kuchezea maisha ya abiria barabarani

Hatuwezi kuwa na taifa la watu wasiokubali kufata sheria na kanuni bila ya shuruti.

Tumezika wapendwa wetu wengi kutokana na uzembe wa madereva. Familia kibao zimebaki mayatima na wengine wanepata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali zinazoletwa na uzembe wa madereva
Oktoba 29, 2025 tumepoteza wapendwa wengi zaidi kwa mara moja. Familia zimenaki yatima kutokana na uroho wa madaraka na uzembe uliosababishwa na executive kama anavyoitafsiri wakili Katuga. Nguvu hii ya kupinga mgomo wa madereva kwa kuwa ni wasababishi wa vifo vya wapendwa wetu, iongezeke zaidi kupinga executive kwa mauaji ya Oktoba 29
 
Itapendeza zaidi huu mfumo wa points ukiwa kwenye kada zote.usiishie tu kada usalama barabarani.

Ikipendeza hata jeshi la polisi kwa mfano,kila askari akifanya kosa naye akatwe points kwenye kazi yake.ili points zikiisha automatically anakua amejifukuza kazi.

Kila kada ikiwekewa mfumo huu itakua safi sana.

Maana ni kweli madereva wanahatarisha maisha ya watu barabarani na ajali zinakua nyingi.

Lakini twende mbali zaidi hadi kwa askari wanaokula rushwa,kusingizia watu kesi na kuwakamata bila utaratibu.

Na mfumo huu wa points twende nao hadi kwa madaktari wasioshinda kwenye vituo vyao vya kazi na kufanya kazi kufanya kazi kwenye vituo vya watu binafsi,waoficha na kuiba dawa muhimu na kuuza kwenye famasi zao.

Naungana na mfumo wa points lakini usiishie kwenye kada moja tu.ikiwezekana ufike hadi kwa wanasiasa.
Mkuu una hoja nzito lakini wala urefu kwa kamba watakushukia kama mwewe!😀
 
Sijapanic siwezi kufundishwa mambo ya road na mtoto asiee ambae haujui hata aina za magari yaliyopo na sheria za bara barani Duniani mimi nikufundshe wewe braza sehemu nazopita inatakiwa uwe dereva kweli sio msukuma gari..
unaji brag sio...mi nafikiri kutikana na experience yako ya kuendesha malori kutoka huko SA ndio ungekuwa balozi mzuri kuhamasisha madereva wenzako kufata taratibu za kimataifa ila ndio kwanza upo kupinga maendeleo ya usalama wa barabarani
 
Nimepita barabara ya moro to dodoma ina mashimo kama yote yani kama wewe ni mgeni unaweza pasua ring inabidi uhame upande urudi kushoto kulia
Waliosababisha barabara ijengwe chini ya kiwango hawawajibishi wapo maofisini wanaendelea kupanga mipango ya kujenga barabara nyingine chini ya viwango, badala yake, wanawajibishwa madereva wanaohama upande kushoto au kulia kukwepa mashimo.
 
Oktoba 29, 2025 tumepoteza wapendwa wengi zaidi kwa mara moja. Familia zimenaki yatima kutokana na uroho wa madaraka na uzembe uliosababishwa na executive kama anavyoitafsiri wakili Katuga. Nguvu hii ya kupinga mgomo wa madereva kwa kuwa ni wasababishi wa vifo vya wapendwa wetu, iongezeke zaidi kupinga executive kwa mauaji ya Oktoba 29
Sijaja kuanzisha mijadala ya vyama vya kisiasa..nimekuja hapa kama mdau wa usalama wa barabarani. Unataka mada hizo kaanzishe uzi kwenye jukwaa la siasa...Upo?
 
Nimepita barabara ya moro to dodoma ina mashimo kama yote yani kama wewe ni mgeni unaweza pasua ring inabidi uhame upande urudi kushoto kulia
kama unaendesha mwendo mzuri sidhani kama utapasua rings. Pia JF inatoa wasaa wa kuwasilisha kero...ukiona sehemu ya barabara ina mashimo yanayoweza kuhatarisha usalama wa watumiaji wa barabara basi leta kero yako humu ifanyiwe kazi...wenye mamlaka wataona na kufanyia kazi
 
Nin
unaji brag sio...mi nafikiri kutikana na experience yako ya kuendesha malori kutoka huko SA ndio ungekuwa balozi mzuri kuhamasisha madereva wenzako kufata taratibu za kimataifa ila ndio kwanza upo kupinga maendeleo ya usalama wa barabarani
Mimi ni transpoter sio dereva tu magari Tanzania wanakimbia sana kwa safari fupi hiyo ndio changamoto yao unataka mimi niwaambie wasikimbie kutoka Tunduma mpaka Daslm gari inadondoka si utani huo wakitoka Lusaka mpaka Johannesburg watafika wangapi shida wanahsindana mbio kufika na abiria wengi wanataka mbio mimi nifanyeje..
 
Sasa Mkuu, si unabidi tuanze na sisi mdogo mdogo? Unadhani wao waliamka tu overnight wakajikita hawana rushwa? Initiatives kama hizi zikianza huwa zinapunguza rushwa taratibu with time, mifumo, transparency nk nk
Ni kweli
Lakini wange balance kote
Kamata wala rushwa kwa kuweka plain clothes kwenye mabasi na kuwakamata hao wanaodhani ni haki yao kula hela za madereva halafu wanawaachia wakafe mbele
Traffic anaachia lorry matairi yameisha kabisa kisa kapewa buku mbili
Anaenda kuuwa watu kumi mbele
Halafu ripoti inasema break zimefeli kumbe matairi yameisha kabisa

Mifumo ya rushwa imekuwa kawaida sana yaani dereva anaweka pembeni hela ya njiani kama sheria

Najua wazungu wametoka mbali lakini pia wamewekeza sana kwenye usalama barabarani kuanzia cameras mpaka points
Unajua Ulaya makampuni ya insurance yana access mpaka traffic department
Kama una points na insurance premium zinapanda kila mwaka mpaka licence itakapokuwa safi
Unaweza ukajikuta unalipa x 3 yake kisa ulivuka traffic lights
Na ukilewa unaweza kufungiwa miaka 10
 
Sasa Mkuu, si unabidi tuanze na sisi mdogo mdogo? Unadhani wao waliamka tu overnight wakajikita hawana rushwa? Initiatives kama hizi zikianza huwa zinapunguza rushwa taratibu with time, mifumo, transparency nk nk
Kwa maoni yangu naona serikali imeruka hatua, walitakiwa waweke camera za barabarani angalau miji yote mikubwa kwa kuanzia na polisi wote wavae bodycam, baaada ya hapo ndio hii sheria ianze kufanya kazi ili kupunguza mazingira ya rushwa, first world inafanyakazi kwa sababu misingi ilishawekwa tusifanye vitu nusunusu
 
Nin
Mimi ni transpoter sio dereva tu magari Tanzania wanakimbia sana kwa safari fupi hiyo ndio changamoto yao unataka mimi niwaambie wasikimbie kutoka Tunduma mpaka Daslm gari inadondoka si utani huo wakitoka Lusaka mpaka Johannesburg watafika wangapi shida wanahsindana mbio kufika na abiria wengi wanataka mbio mimi nifanyeje..
paza sauti naamini kuna madereva unaweza kuwanadilisha mindset zao. Kama ushapoteza ndugu, jamaa na marafiki kwenye ajali najua utakuwa unaelewa nini nahimiza.
 
Kwa maoni yangu naona serikali imeruka hatua, walitakiwa waweke camera za barabarani angalau miji yote mikubwa kwa kuanzia na polisi wote wavae bodycam, baaada ya ndio hii sheria ianze kufanya kazi ili kupunguza mazingira ya rushwa, first world inafanyakazi kwa sababu misingi ilishawekwa tusifanye vitu nusunusu
ushauri mzuri pia
 
Wana-Jamii Forums salamu,

Kama mnavyofahamu, nchi imeshuhudia taharuki na usumbufu mkubwa kufuatia mgomo wa ghafla wa madereva wa mabasi ya mikoani na malori unaopinga utekelezaji wa mfumo mpya wa Jeshi la Polisi wa kukata pointi kwenye leseni za udereva kila wanapofanya makosa.


Binafsi nasema, Serikali isitii kabisa matakwa ya mgomo huu na isirudi nyuma kwenye msimamo wake. Kufanya hivyo ni kuzidi kuhalalisha uzembe na kuhatarisha maisha ya abiria na mali zao barabarani.
Hebu tuangalie ukweli bila kumung'unya maneno:

1. Uzembe uliokithiri na "Kamari" ya Ligi za Barabarani

Madereva wa mabasi ya mikoani wanaongoza kwa kufanya makosa ya kijinga na ya kizembe barabarani. Wengi wao wanafanya overtake za hovyo kwenye milima, kona, na maeneo yenye mstari mmoja ulionyooka bila kuzingatia sheria wala kanuni zozote za usalama.

Inasikitisha sana kuona pindi mabasi yanapotoka stendi kuu ya Mbezi Magufuli kwenda mikoani, au kutoka mikoani kuja Dar es Salaam, madereva hawa na wadau wao wanageuza maisha ya watu kuwa kamari. Kuna ujinga wa hovyo unaoitwa "Ligi za Barabarani / Ligi za wanazi " ambapo wanashindana mbele ya abiria kuona basi gani linakimbia zaidi au gari gani litawahi kufika. Huu ni upumbavu uliopitiliza na watanzania tumechoka kuzika ndugu zetu kila siku kwa sababu ya sifa za kijinga za watu wachache. Faini ya fedha pekee imeonekana kutofua dafu kwa sababu wamiliki wanazilipa, lakini mfumo huu wa pointi unamwajibisha dereva mmoja mmoja binafsi ili anyooshe nidhamu yake.

2. Kulinda Maisha ya Wananchi vs Maslahi ya Madereva
Kugoma kisa tu unalazimishwa kufuata sheria ni utovu wa nidhamu. Dereva anayejiamini kuwa anafuata sheria na kuheshimu alama za barabarani anaogopa nini kukatwa pointi? Ni wazi kuwa wanaogopa kwa sababu wanajua hawana nidhamu barabarani. Serikali isikubali kuwekwa mtu kati na kikundi cha watu wanaotaka kupewa leseni ya kuendelea kuua raia wetu kwa uzembe.

3. Mfumo wa Pointi ni Suluhisho la Kimataifa (Mifano ya Nchi Zilizofanikiwa)

Mifumo hii ya point-deduction inatumika duniani kote na imethibitika kisayansi kupunguza ajali kwa zaidi ya 21% na vifo kwa 10%.

Uingereza na Ujerumani: Zina mifumo madhubuti ya pointi ambapo dereva akifikisha kiwango fulani cha makosa, leseni inafungiwa kiotomatiki na anarudishwa chuo kusomea upya udereva. Hii imesaidia kuwa na madereva wenye nidhamu ya hali ya juu barabarani.

Italia

(Ukanda wa Veneto): Utafiti unaonyesha tangu kuanzishwa kwa mfumo huu, zaidi ya vifo 1,500 na majeraha ya barabarani zaidi ya 91,000 yaliepukwa kwa sababu madereva walianza kuogopa kupoteza leseni zao.

Ushauri wangu kwa Serikali: Leteni Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kwa Askari
Ili kuondoa malalamiko ya madereva kudai kuwa wanaonewa au kubambikiziwa makosa, na ili kudhibiti mianya ya rushwa barabarani, nashauri serikali iweke utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwa na Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kama wanavyofanya mataifa makubwa.

Teknolojia hii itarekodi mazungumzo na matukio yote kati ya askari na dereva papo hapo:

Mataifa kama Marekani na Uingereza: Matumizi ya kamera hizi yamesaidia kupunguza malalamiko dhidi ya askari kwa takriban 16% hadi 17%. Kamera iko wazi, hivyo dereva hawezi kutoa rushwa na askari hawezi kuomba rushwa wala kumbambikizia dereva kosa kwa sababu kila kitu kinakuwa na ushahidi wa video na sauti. Hii inaleta uwazi na haki kwa pande zote mbili.

Wito wangu kwa Serikali:
Kaeni chonjo na shinikizo la mgomo huu. Tukirudi nyuma sasa hivi, tutakuwa tumefungulia milango ya ajali zaidi, vifo, na ulemavu usio na lazima barabarani. Sheria ikazie hapo hapo, na yeyote anayeona hawezi kufuata sheria, aachie usukani akafanye kazi nyingine.

 Usalama wa abiria na mali zao kwanza!
Mkuu mfumo huu sio mbaya, tatizo ni je wasimamizi wa sheria (traffic) wana maadili?
So far so good, mambo ya kubambikiwa makosa na kutafutiwa sababu utoe chochote ni mengi sana huko barabarani, kwa hivo kabla ya kuleta mfumo huu ni lazima kwanza huko barabani kusafishwe na watu waone kumesafishika. Kisha ukileta haya hamna atakayelaumu maana kunakuwa na fairness.
Bodycam itapunguza kidogo sana tatizo maana hawa police wetu tunawajua, wataanzisha mfumo wa ukisogea mbele yupo shoe shine mwachie mzigo wangu.

Nchi hii Traffic wanaongoza kwa kula rushwa na hapa ndo mzizi wa matatizo mengi ya usalama barabani.
 
Mmoja alikuwa anasema kuwa Eti ukianza kutoka Stendi magari ni mengi na njia n ndogo sasa inabidi u overtake Sana ili uende na muda, nilichoka kusikia hiyo hoja...Halafu Kingine hawa Traffic ni watu wapuuzi Sana wanapenda Sana chochote kitu yani lazima uache Hela ya soda, madereva wameshazoea hiyo Hali huwa Pembeni wanakuwa na posho za matrafki kabisa.
 
Mkuu mfumo huu sio mbaya, tatizo ni je wasimamizi wa sheria (traffic) wana maadili?
So far so good, mambo ya kubambikiwa makosa na kutafutiwa sababu utoe chochote ni mengi sana huko barabarani, kwa hivo kabla ya kuleta mfumo huu ni lazima kwanza huko barabani kusafishwe na watu waone kumesafishika. Kisha ukileta haya hamna atakayelaumu maana kunakuwa na fairness.
Bodycam itapunguza kidogo sana tatizo maana hawa police wetu tunawajua, wataanzisha mfumo wa ukisogea mbele yupo shoe shine mwachie mzigo wangu.

Nchi hii Traffic wanaongoza kwa kula rushwa na hapa ndo mzizi wa matatizo mengi ya usalama barabani.
polisi wanakula rushwa kwasababu ya madereva kutoa rushwa
 
paza sauti naamini kuna madereva unaweza kuwanadilisha mindset zao. Kama ushapoteza ndugu, jamaa na marafiki kwenye ajali najua utakuwa unaelewa nini nahimiza.
Sauti Tanzania aisee niliwahi kushuka kwenye bus Iringa nikiwa na Ticket ya Daslm Sauli mimi ndio naonekana mshamba kwa ule mwendo nikawaambia niacheni kituoni nimefika nikapanda bus lingine wafanyabiashara wanapenda ile speed ukiwa mgeni kwenye bus zao unawaamulia mambo wanakasirika hizo bus zinaruka sio kukimbia..
 
Sijaja kuanzisha mijadala ya vyama vya kisiasa..nimekuja hapa kama mdau wa usalama wa barabarani. Unataka mada hizo kaanzishe uzi kwenye jukwaa la siasa...Upo?
Serikali sio chama. Vifo haviangalii chama, sababu ya hoja yako ni vifo vya wapendwa waliokuwa safarini, vivyo hivyo majibu yangu yanahosu vifo vya waliokufa wakiwa safarini tarehe 29/10, wakienda makazini, wakiwa wanarudi majumbani mwao, wakienda sokoni nk, hakuna mahala pametajwa vyama vya siasa. Pinga hivyo vifo, la, acha watu waendelee na mgomo wao. Jukwaa la Siasa nenda wewe mkuu, mimi najibu hoja yako jukwaa hilihili
 
Back
Top Bottom