Serikali isirudi nyuma: Mfumo wa kukata pointi kwenye leseni usisistishwe, migomo isitumike kuchezea maisha ya abiria barabarani

Wana-Jamii Forums salamu,

Kama mnavyofahamu, nchi imeshuhudia taharuki na usumbufu mkubwa kufuatia mgomo wa ghafla wa madereva wa mabasi ya mikoani na malori unaopinga utekelezaji wa mfumo mpya wa Jeshi la Polisi wa kukata pointi kwenye leseni za udereva kila wanapofanya makosa.

Binafsi nasema, Serikali isitii kabisa matakwa ya mgomo huu na isirudi nyuma kwenye msimamo wake. Kufanya hivyo ni kuzidi kuhalalisha uzembe na kuhatarisha maisha ya abiria na mali zao barabarani.
Hebu tuangalie ukweli bila kumung'unya maneno:

1. Uzembe uliokithiri na "Kamari" ya Ligi za Barabarani

Madereva wa mabasi ya mikoani wanaongoza kwa kufanya makosa ya kijinga na ya kizembe barabarani. Wengi wao wanafanya overtake za hovyo kwenye milima, kona, na maeneo yenye mstari mmoja ulionyooka bila kuzingatia sheria wala kanuni zozote za usalama.

Inasikitisha sana kuona pindi mabasi yanapotoka stendi kuu ya Mbezi Magufuli kwenda mikoani, au kutoka mikoani kuja Dar es Salaam, madereva hawa na wadau wao wanageuza maisha ya watu kuwa kamari. Kuna ujinga wa hovyo unaoitwa "Ligi za Barabarani / Ligi za wanazi " ambapo wanashindana mbele ya abiria kuona basi gani linakimbia zaidi au gari gani litawahi kufika. Huu ni upumbavu uliopitiliza na watanzania tumechoka kuzika ndugu zetu kila siku kwa sababu ya sifa za kijinga za watu wachache. Faini ya fedha pekee imeonekana kutofua dafu kwa sababu wamiliki wanazilipa, lakini mfumo huu wa pointi unamwajibisha dereva mmoja mmoja binafsi ili anyooshe nidhamu yake.

2. Kulinda Maisha ya Wananchi vs Maslahi ya Madereva
Kugoma kisa tu unalazimishwa kufuata sheria ni utovu wa nidhamu. Dereva anayejiamini kuwa anafuata sheria na kuheshimu alama za barabarani anaogopa nini kukatwa pointi? Ni wazi kuwa wanaogopa kwa sababu wanajua hawana nidhamu barabarani. Serikali isikubali kuwekwa mtu kati na kikundi cha watu wanaotaka kupewa leseni ya kuendelea kuua raia wetu kwa uzembe.

3. Mfumo wa Pointi ni Suluhisho la Kimataifa (Mifano ya Nchi Zilizofanikiwa)

Mifumo hii ya point-deduction inatumika duniani kote na imethibitika kisayansi kupunguza ajali kwa zaidi ya 21% na vifo kwa 10%.

Uingereza na Ujerumani: Zina mifumo madhubuti ya pointi ambapo dereva akifikisha kiwango fulani cha makosa, leseni inafungiwa kiotomatiki na anarudishwa chuo kusomea upya udereva. Hii imesaidia kuwa na madereva wenye nidhamu ya hali ya juu barabarani.

Italia

(Ukanda wa Veneto): Utafiti unaonyesha tangu kuanzishwa kwa mfumo huu, zaidi ya vifo 1,500 na majeraha ya barabarani zaidi ya 91,000 yaliepukwa kwa sababu madereva walianza kuogopa kupoteza leseni zao.

Ushauri wangu kwa Serikali: Leteni Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kwa Askari
Ili kuondoa malalamiko ya madereva kudai kuwa wanaonewa au kubambikiziwa makosa, na ili kudhibiti mianya ya rushwa barabarani, nashauri serikali iweke utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwa na Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kama wanavyofanya mataifa makubwa.

Teknolojia hii itarekodi mazungumzo na matukio yote kati ya askari na dereva papo hapo:

Mataifa kama Marekani na Uingereza: Matumizi ya kamera hizi yamesaidia kupunguza malalamiko dhidi ya askari kwa takriban 16% hadi 17%. Kamera iko wazi, hivyo dereva hawezi kutoa rushwa na askari hawezi kuomba rushwa wala kumbambikizia dereva kosa kwa sababu kila kitu kinakuwa na ushahidi wa video na sauti. Hii inaleta uwazi na haki kwa pande zote mbili.

Wito wangu kwa Serikali:
Kaeni chonjo na shinikizo la mgomo huu. Tukirudi nyuma sasa hivi, tutakuwa tumefungulia milango ya ajali zaidi, vifo, na ulemavu usio na lazima barabarani. Sheria ikazie hapo hapo, na yeyote anayeona hawezi kufuata sheria, aachie usukani akafanye kazi nyingine.

 Usalama wa abiria na mali zao kwanza!
Itapendeza zaidi huu mfumo wa points ukiwa kwenye kada zote.usiishie tu kada usalama barabarani.

Ikipendeza hata jeshi la polisi kwa mfano,kila askari akifanya kosa naye akatwe points kwenye kazi yake.ili points zikiisha automatically anakua amejifukuza kazi.

Kila kada ikiwekewa mfumo huu itakua safi sana.

Maana ni kweli madereva wanahatarisha maisha ya watu barabarani na ajali zinakua nyingi.

Lakini twende mbali zaidi hadi kwa askari wanaokula rushwa,kusingizia watu kesi na kuwakamata bila utaratibu.

Na mfumo huu wa points twende nao hadi kwa madaktari wasioshinda kwenye vituo vyao vya kazi na kufanya kazi kufanya kazi kwenye vituo vya watu binafsi,wanaoficha na kuiba dawa muhimu na kuuza kwenye famasi zao.

Naungana na mfumo wa points lakini usiishie kwenye kada moja tu.ikiwezekana ufike hadi kwa wanasiasa.
 
Wana-Jamii Forums salamu,

Kama mnavyofahamu, nchi imeshuhudia taharuki na usumbufu mkubwa kufuatia mgomo wa ghafla wa madereva wa mabasi ya mikoani na malori unaopinga utekelezaji wa mfumo mpya wa Jeshi la Polisi wa kukata pointi kwenye leseni za udereva kila wanapofanya makosa.

Binafsi nasema, Serikali isitii kabisa matakwa ya mgomo huu na isirudi nyuma kwenye msimamo wake. Kufanya hivyo ni kuzidi kuhalalisha uzembe na kuhatarisha maisha ya abiria na mali zao barabarani.
Hebu tuangalie ukweli bila kumung'unya maneno:

1. Uzembe uliokithiri na "Kamari" ya Ligi za Barabarani

Madereva wa mabasi ya mikoani wanaongoza kwa kufanya makosa ya kijinga na ya kizembe barabarani. Wengi wao wanafanya overtake za hovyo kwenye milima, kona, na maeneo yenye mstari mmoja ulionyooka bila kuzingatia sheria wala kanuni zozote za usalama.

Inasikitisha sana kuona pindi mabasi yanapotoka stendi kuu ya Mbezi Magufuli kwenda mikoani, au kutoka mikoani kuja Dar es Salaam, madereva hawa na wadau wao wanageuza maisha ya watu kuwa kamari. Kuna ujinga wa hovyo unaoitwa "Ligi za Barabarani / Ligi za wanazi " ambapo wanashindana mbele ya abiria kuona basi gani linakimbia zaidi au gari gani litawahi kufika. Huu ni upumbavu uliopitiliza na watanzania tumechoka kuzika ndugu zetu kila siku kwa sababu ya sifa za kijinga za watu wachache. Faini ya fedha pekee imeonekana kutofua dafu kwa sababu wamiliki wanazilipa, lakini mfumo huu wa pointi unamwajibisha dereva mmoja mmoja binafsi ili anyooshe nidhamu yake.

2. Kulinda Maisha ya Wananchi vs Maslahi ya Madereva
Kugoma kisa tu unalazimishwa kufuata sheria ni utovu wa nidhamu. Dereva anayejiamini kuwa anafuata sheria na kuheshimu alama za barabarani anaogopa nini kukatwa pointi? Ni wazi kuwa wanaogopa kwa sababu wanajua hawana nidhamu barabarani. Serikali isikubali kuwekwa mtu kati na kikundi cha watu wanaotaka kupewa leseni ya kuendelea kuua raia wetu kwa uzembe.

3. Mfumo wa Pointi ni Suluhisho la Kimataifa (Mifano ya Nchi Zilizofanikiwa)

Mifumo hii ya point-deduction inatumika duniani kote na imethibitika kisayansi kupunguza ajali kwa zaidi ya 21% na vifo kwa 10%.

Uingereza na Ujerumani: Zina mifumo madhubuti ya pointi ambapo dereva akifikisha kiwango fulani cha makosa, leseni inafungiwa kiotomatiki na anarudishwa chuo kusomea upya udereva. Hii imesaidia kuwa na madereva wenye nidhamu ya hali ya juu barabarani.

Italia

(Ukanda wa Veneto): Utafiti unaonyesha tangu kuanzishwa kwa mfumo huu, zaidi ya vifo 1,500 na majeraha ya barabarani zaidi ya 91,000 yaliepukwa kwa sababu madereva walianza kuogopa kupoteza leseni zao.

Ushauri wangu kwa Serikali: Leteni Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kwa Askari
Ili kuondoa malalamiko ya madereva kudai kuwa wanaonewa au kubambikiziwa makosa, na ili kudhibiti mianya ya rushwa barabarani, nashauri serikali iweke utaratibu wa askari wa usalama barabarani kuwa na Kamera za Vifuani (Body-Worn Cameras) kama wanavyofanya mataifa makubwa.

Teknolojia hii itarekodi mazungumzo na matukio yote kati ya askari na dereva papo hapo:

Mataifa kama Marekani na Uingereza: Matumizi ya kamera hizi yamesaidia kupunguza malalamiko dhidi ya askari kwa takriban 16% hadi 17%. Kamera iko wazi, hivyo dereva hawezi kutoa rushwa na askari hawezi kuomba rushwa wala kumbambikizia dereva kosa kwa sababu kila kitu kinakuwa na ushahidi wa video na sauti. Hii inaleta uwazi na haki kwa pande zote mbili.

Wito wangu kwa Serikali:
Kaeni chonjo na shinikizo la mgomo huu. Tukirudi nyuma sasa hivi, tutakuwa tumefungulia milango ya ajali zaidi, vifo, na ulemavu usio na lazima barabarani. Sheria ikazie hapo hapo, na yeyote anayeona hawezi kufuata sheria, aachie usukani akafanye kazi nyingine.

 Usalama wa abiria na mali zao kwanza!
Ni kweli mkuu zina hiyo mifumo ila hata moundombinu yao ni bora. Sisi leo unapita mwenge mataa yanawaka, unakuja pita baadaye hayawaki... Harabara ya dar dodoma from moro to dodoma full mashimo unahama hama barabara.
Ila pia madereva wa mabasi wanazingua barabarani. Yani dereva anaocertake bila kujali kama kuna gari dogo linakuja wewe utajua mwenyewe uingie mtaroni au vichakani. Sometimes inabidi wavundishwe
 
Siku ukipoteza mtu wako wa karibu kwa ajili ya ligi ya za kina katarama na ally star huko barabara,akili yako ndio itakaa sawa
Zile bus zinakimbia sana aisee nadhani wangepunguza muda wa kutoka na kufika huko maana sioni sababu ya wao kushindana kufika huku wakisababisha ajali..
Mimi nimeshuhudia ajali nyingi za kizembe sana.
 
Mimi sihofii hizo mambo na pia udereva wangu ni wa kutoa gari SA na kuleta Tanzania hapa nasukuma mashine ambayo sio ya mambo ya points wala leseni..
Basi ukiingia ndani ya mipaka ya Tanzania ni sharti ufuate sheria za barabarani za Tanzania
 
Hii sheria iende mpaka kwa madereva wanaoendesha magari ya serikali..wengi wanaendesha ovyo sana bila ya kuzingatia sheria zozote za barabarani wakitegemea kings ya serikali.
Commissioner wa police Nottinghamshire UK tena Mwanamke alikamatwa mara Sita kwa speed alipigwa faini na Mwisho akafungiwa license yake kwa miezi sita
Wenzetu hawana rushwa Ndio maana hata uwe Nani ni lazima ufuate sheria

Je sisi tutaweza maana hata ukiwa na shangingi jeupe na wewe ni raia wa kawaida upite speed zote basi polisi anadhani ni serikali na kupisha uende

Je nani katoa amri hizo gari zivunje sheria?
Siku Mbunge au mkurugenzi akipigwa faini ndio nitajua sheria zipo
 
Ni kweli mkuu zina hiyo mifumo ila hata moundombinu yao ni bora. Sisi leo unapita mwenge mataa yanawaka, unakuja pita baadaye hayawaki... Harabara ya dar dodoma from moro to dodoma full mashimo unahama hama barabara.
Ila pia madereva wa mabasi wanazingua barabarani. Yani dereva anaocertake bila kujali kama kuna gari dogo linakuja wewe utajua mwenyewe uingie mtaroni au vichakani. Sometimes inabidi wavundishwe
miundombinu inamzuia vp dereva makini kufuata sheria na kanuni za barabarani?
 
Ulicho kusema ni sahihi serikali haitakiwi kulegeza kamba kwenye hili, ila tatizo lake ni kuwa madireva wanakatwa point hata kwenye makosa yanayo husiana na gari Moja Kwa Moja hali ya kuwa sio jukumu la dreva kutengeneza gari bali ni mwenye gari.
Mm nadhani ingekuwa poa iwapo kukatwa point kungehusisha makosa ya uzembe tu.
 
hicho ni kisingizio tu cha madereva kutaka huu mfumo utolewe
 
Commissioner wa police Nottinghamshire UK tena Mwanamke alikamatwa mara Sita kwa speed alipigwa faini na Mwisho akafungiwa license yake kwa miezi sita
Wenzetu hawana rushwa Ndio maana hata uwe Nani ni lazima ufuate sheria

Je sisi tutaweza maana hata ukiwa na shangingi jeupe na wewe ni raia wa kawaida upite speed zote basi polisi anadhani ni serikali na kupisha uende

Je nani katoa amri hizo gari zivunje sheria?
Siku Mbunge au mkurugenzi akipigwa faini ndio nitajua sheria zipo
Sasa Mkuu, si unabidi tuanze na sisi mdogo mdogo? Unadhani wao waliamka tu overnight wakajikita hawana rushwa? Initiatives kama hizi zikianza huwa zinapunguza rushwa taratibu with time, mifumo, transparency nk nk
 
Commissioner wa police Nottinghamshire UK tena Mwanamke alikamatwa mara Sita kwa speed alipigwa faini na Mwisho akafungiwa license yake kwa miezi sita
Wenzetu hawana rushwa Ndio maana hata uwe Nani ni lazima ufuate sheria

Je sisi tutaweza maana hata ukiwa na shangingi jeupe na wewe ni raia wa kawaida upite speed zote basi polisi anadhani ni serikali na kupisha uende

Je nani katoa amri hizo gari zivunje sheria?
Siku Mbunge au mkurugenzi akipigwa faini ndio nitajua sheria zipo
Hata wao walitokea mbali mpka kujenga hiyo nidhamu. Si vibaya nasi tukapitia katika michakato hiyohiyo..nina imani miaka 30 ijayo tutakuwa na taifa lenye madereva makini wanaofuata sheria na kanuni za usalama wa barabarani bila ya shuruti. Ifike mahali mtu akiona chombo cha moto ajue kabisa sio cha kufanyia mchezo
 
Back
Top Bottom