Nimependa ufafanuzi wako wa takwimu kuhusu athari za gonjwa (morbidity) kwa kuzingatia demografia.
 
Sijaelewa hicho kikosi kinachopinga mchina hayupo Tanzania wakati ugonjwa unasambaa kwa hewa wakati watu wanasafiri chukueni tahadhari kinga ni bora kuliko Tiba...
 
Jibu kwa hoja, mimi nimeuliza maswali wewe unatoa matusi. Mtu katoa maoni yake hadharani hutaki aulizwe? Basi angebaki nayo mwenyewe kama hataki maswali au mitazamo tofauti na yake.
Kuna jamaa huwa wamebalikiwa kwenye matusi hawajui ya kuwa ustaarabu hauna gharama.
 
Hasara iliyokuja baada ya Magufuli kudanganya umma kuwa maombi ya siku tatu yameifuta Corona Tanzania ni kwamba watu hawajikingi tena wala kuchukua tahadhari!
Huo sio ukweli,ni kwamba toka mwanzo watanzania hawakuwa serious kujikinga na corona. Wakati ule ndio serikali bado inatangaza kuwepo corona Tz na takwimu zilikuwa zinaonesha maambukizi yanazidi mitandaoni kulikuwa na video za watu kuzikwa usiku,ila pamoja na yote hayo kitu ambacho watanzania walikuwa wanafanya sana ni kunawa mikono mpaka wengine wakawa wanabeza suala hilo,watu wakawa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida nyumba za ibada watu walikuwa wanajaa kama kawaida huko kariakoo ilikuwa kama kawaida.

Sasa ukiangalia hayo yote utaona ni jinsi gani watanzania hawakuwa wakizingatia kujikinga na corona toka mwanzo na ndio maana ikawa rahisi kwao kukubali hakuna corona kwa sababu kabla hata ya kutangaziwa hakuna corona wao wenyewe asilimia kubwa walikuwa wanaishi kama hakuna corona. Kwahiyo suala la corona na maombi ni imani ya baadhi ya watu tu na si kwamba watanzania wameacha kujikinga na corona kwa sababu wametangaziwa maombi ndio yameondoa corona.
 
Hata wewe unaleta siasa kwenye corona na ndio maana kipindi cha kampeni mwaka jana ulikuwa bize na kumuelezea Lissu na jinsi alivyojaza watu kwenye mikutano yake ya kampeni,wakati huo hukuona kwamba ile mikusanyiko itaongeza maambukizi ya corona hasa ukizingatia watu hawakuwa wakivaa hata barakoa ila hatukuona ukitoa tahadhari zozote hakuna hata uzi mmoja uliyotoa wa kuhusu corona katika kipindi chote cha uchaguzi.
 
Hasara iliyokuja baada ya Magufuli kudanganya umma kuwa maombi ya siku tatu yameifuta Corona Tanzania ni kwamba watu hawajikingi tena wala kuchukua tahadhari!
Mmeshakufa wangapi baada ya kutochukua tahadhali?
Vipi kuhusu uingeleza kwa Sasa wanakufa wangapi kwa siku?'
 
Hasara iliyokuja baada ya Magufuli kudanganya umma kuwa maombi ya siku tatu yameifuta Corona Tanzania ni kwamba watu hawajikingi tena wala kuchukua tahadhari!
Ndio ujue kuna Mungu na ni suala la imani, wewe inaonyesha huna imani...je unaamini Mungu anaponya? hata wewe hapo unayeongea umeazimwa pumzi tu na Mungu akitaka kuichukua mwenyewe wakati wowote anaichukua..upo..!!
 
ACHA UROONGO! KUDHIBITI AU KUTODHIBITI HAKUHUSIANA NA MUBEZA KWENYE MITANDAO BRO! INDIA, UGANDA NA NCHI KADHAA WATU WAMEPIGWA HADI MIKWAJU KWA KUJARIBU KPUUZIA MARUFUKU ZILIZOTOLEWA! TZ HATUKUTOA MARUFUKU TULIKUWA TUNATOA TAHADHARI NA ANGALIZO.
 
Hivi baba yetu amesharudi toka Chato kuja Dodoma?
 
Ingekuwa vyema ingewaondoa wale wazee ambao hawataki kustaafu kuwaachia vjana bado tu wameshikilia sekta nyeti
 
Kuna jamaa huwa wamebalikiwa kwenye matusi hawajui ya kuwa ustaarabu hauna gharama.
Kumjibu mjinga kutokana na ujinga wake ni baraka. Wapi mleta mada aliposema wazee zamani walikuwa hawafi? Wapi mleta mada aliposema waliochukua tahadhari hawana vifo? Mtu analeta hoja ya maana mnaleta maswali ya kejeli tuwaache tu tunawaogopa?
 
Hivi nauliza nani kazuiwa kuvaa Barakoa?

Nauliza nani kazuiwa kutembea na sanitizer?

Nani kalazimishwa kushikana mikono na mwingine wakati wa kusalimiana?

Nani kazuiwa kunawa mikono kila baada ya muda fulani?

Acheni siasa kwa kutaka kila kitu kisemwe na serikali.

Maisha ni yako wewe kwa manufaa yako, familia yako na wanaokuzunguka ki ukoo.
Kuna shida gani kila mtu kutimiza wajibu wake kwa kuanza kuhimizana kufuata vigezo vya covid19.

Kama ni watu wa chama fulani mnaamini covid19 imelipuka tena nchini kwa jinsi mnavyoonekana kuaminishana basi kwa nini kama taasisi msianze kuhamasishana kuvaa hizo barakoa na kutumia sanitizer?

Corona ipo ndio na Tanzania ni duniani kama nchi zingine zilipo.
Lakini nawauliza...kama ipo na watu wanakufa mbona Maskini hatuwaoni mitaani na mahospitalini wakiwa hoi kwa kushindwa kupumua?
Mmebaki tu kueneza uvumi wa Agha khan kila uchao.

Wengine kazi yenu kueneza ooh mtu wangu wa karibu.....

Mara oh jamaa yangu mmoja?

Acheni UNAFIKIIII!!!@wakaanga sumu!

Hii kitu ikienea hakuna itikadi fulani itakayobaki salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…