zege la nyasi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2018
- 938
- 1,255
Kinga ni bora kuliko tiba......
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walisema waungwana: "Mwenyezi Mungu si Athumani.
Nimependa ufafanuzi wako wa takwimu kuhusu athari za gonjwa (morbidity) kwa kuzingatia demografia.Inawezekana kabisa nia ya Magufuli ya kufungua uchumi pamoja na kuwa na Corona ni uamuzi mzuri lakini makosa yanayofanywa ni kijiaminisha kwamba huu ugojwa haupo na hauwezi kuingia Tanzania kwasababu huu sio ukweli.
Kuuwaambia Watanzania wanawe mikono, wasishikane mikono ovyo na kuwa mita moja wakati wa kuongea ni muhimu sana. Watanzania ni lazima tujue huu ugojwa ni mbaya zaidi kwa watu wenye kisukari, pumu na wazee wote wenye umri zaidi ya miaka 60. Kibaya zaidi mwezi wa kumi na mbili walikuwa diaspora na wenzetu wengine walisafiri na wakaleta hii Corona inayo enea haraka. Tusifanye hili swala la kisiasa maana hawa wazee ni wetu wote. Imekuwa kisirisiri lakini Agha khan hospital pekee ndiyo wana dawa za majaribio pale oxygen za kutosha na habari nazopata kwa marafiki Madaktari wa pale wagojwa wameongezeka sana hasa wazee na kwa siku kuna wanaolipa milioni mbili kwa kulazwa. Ndugu yangu mmoja wazazi wake wawili walilazwa mama pekee alidaiwa milioni 36 na mzee wake bado yupo kwenye oxygen na inaweza kuwa milioni 40 nyingine na nilijua kwasababu wanapitisha bakuli la kuomba pesa.
Sababu moja wapo tuna wagojwa wacheche wanaojulikana kwetu ni umri Tanzania umri wa kati ni miaka 17-18 wakati US kwa mfano ni karibu miaka 43-44. Huu ugojwa kwa vijana wadogo wanaweza kuumwa mpaka kupona bila hata ya mtu kujua. Watanzania wenye umri wa miaka zaidi ya 64 ni asilimia 3 tu!! hivyo tusishangae wagojwa wanaozidiwa kuwa wachache. Asilimia zaidi ya 80 ya Watanzania ni chini ya miaka 30 na hawa wengi watakuwa sawa hata kama wakipata Corona. Lakini wito wangu ni kulinda wazee wetu.
Kuna jamaa huwa wamebalikiwa kwenye matusi hawajui ya kuwa ustaarabu hauna gharama.Jibu kwa hoja, mimi nimeuliza maswali wewe unatoa matusi. Mtu katoa maoni yake hadharani hutaki aulizwe? Basi angebaki nayo mwenyewe kama hataki maswali au mitazamo tofauti na yake.
Huo sio ukweli,ni kwamba toka mwanzo watanzania hawakuwa serious kujikinga na corona. Wakati ule ndio serikali bado inatangaza kuwepo corona Tz na takwimu zilikuwa zinaonesha maambukizi yanazidi mitandaoni kulikuwa na video za watu kuzikwa usiku,ila pamoja na yote hayo kitu ambacho watanzania walikuwa wanafanya sana ni kunawa mikono mpaka wengine wakawa wanabeza suala hilo,watu wakawa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida nyumba za ibada watu walikuwa wanajaa kama kawaida huko kariakoo ilikuwa kama kawaida.Hasara iliyokuja baada ya Magufuli kudanganya umma kuwa maombi ya siku tatu yameifuta Corona Tanzania ni kwamba watu hawajikingi tena wala kuchukua tahadhari!
Utapata faida gani? Corona itapotea?Jf tunaomba mreport huyu jamaa TCRA
Hata wewe unaleta siasa kwenye corona na ndio maana kipindi cha kampeni mwaka jana ulikuwa bize na kumuelezea Lissu na jinsi alivyojaza watu kwenye mikutano yake ya kampeni,wakati huo hukuona kwamba ile mikusanyiko itaongeza maambukizi ya corona hasa ukizingatia watu hawakuwa wakivaa hata barakoa ila hatukuona ukitoa tahadhari zozote hakuna hata uzi mmoja uliyotoa wa kuhusu corona katika kipindi chote cha uchaguzi.Kwa kusema haya umetimiza wajibu wako kama binadamu.
Ni bahati mbaya kuwa ugonjwa huu hatari kama ulivyo, umefanywa kuwa ni mtaji wa siasa na mijamaa ya chama fulani pasipo na kujali maisha yanayopotea.
Mijamaa hiyo imejikita katika kuhalalisha hata watu kufa ili tu kumpendezesha bwana mkubwa wao.
Utu umeyatoka kiasi kuwa hawajali maisha ya watu kabisa.
Hadi pale gonjwa hili litakapo mtembelea bwana yule vilivyo kila mwenye domo ana lake la kusema.
Walisema waungwana: "Mwenyezi Mungu si Athumani."
Yetu yanabakia kuwa ni macho hadi siku muafaka itakapofika.
Mmeshakufa wangapi baada ya kutochukua tahadhali?Hasara iliyokuja baada ya Magufuli kudanganya umma kuwa maombi ya siku tatu yameifuta Corona Tanzania ni kwamba watu hawajikingi tena wala kuchukua tahadhari!
Ndio ujue kuna Mungu na ni suala la imani, wewe inaonyesha huna imani...je unaamini Mungu anaponya? hata wewe hapo unayeongea umeazimwa pumzi tu na Mungu akitaka kuichukua mwenyewe wakati wowote anaichukua..upo..!!Hasara iliyokuja baada ya Magufuli kudanganya umma kuwa maombi ya siku tatu yameifuta Corona Tanzania ni kwamba watu hawajikingi tena wala kuchukua tahadhari!
Ila malaika mkuu anaishi hapa!Bagonza kalikawe alisema "Tanzania siyo Makao Makuu ya Mungu"
Ntafuta maana yake mpaka leo sijapata
ACHA UROONGO! KUDHIBITI AU KUTODHIBITI HAKUHUSIANA NA MUBEZA KWENYE MITANDAO BRO! INDIA, UGANDA NA NCHI KADHAA WATU WAMEPIGWA HADI MIKWAJU KWA KUJARIBU KPUUZIA MARUFUKU ZILIZOTOLEWA! TZ HATUKUTOA MARUFUKU TULIKUWA TUNATOA TAHADHARI NA ANGALIZO.Huo sio ukweli,ni kwamba toka mwanzo watanzania hawakuwa serious kujikinga na corona. Wakati ule ndio serikali bado inatangaza kuwepo corona Tz na takwimu zilikuwa zinaonesha maambukizi yanazidi mitandaoni kulikuwa na video za watu kuzikwa usiku,ila pamoja na yote hayo kitu ambacho watanzania walikuwa wanafanya sana ni kunawa mpaka wengine wakawa wanabeza suala hilo,watu wakawa wanaendelea na shughuli zao kama kawaida nyumba za ibada watu walikuwa wanajaa kama kawaida huko kariakoo ilikuwa kama kawaida.
Sasa ukiangalia hayo yote utaona ni jinsi gani watanzania hawakuwa wakizingatia kujikinga na corona toka mwanzo na ndio maana ikawa rahisi kwao kukubali hakuna corona kwa sababu kabla hata ya kutangaziwa hakuna corona wao wenyewe asilimia kubwa walikuwa wanaishi kama hakuna corona. Kwahiyo suala la corona na maombi ni imani ya baadhi ya watu tu na si kwamba watanzania wameacha kujikinga na corona kwa sababu wametangaziwa maombi ndio yameondoa corona.
Kumjibu mjinga kutokana na ujinga wake ni baraka. Wapi mleta mada aliposema wazee zamani walikuwa hawafi? Wapi mleta mada aliposema waliochukua tahadhari hawana vifo? Mtu analeta hoja ya maana mnaleta maswali ya kejeli tuwaache tu tunawaogopa?Kuna jamaa huwa wamebalikiwa kwenye matusi hawajui ya kuwa ustaarabu hauna gharama.