#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Mimi nashauri serikali iache kununua madawa yote hospitalini maana ni ya wazungu.

Serikali iache tuombe mungu magonjwa yote yataisha.

Hakuna haja ya kua na wizara ya afya maana magonjwa yote tutaomba mungu atatuponya.
 
Tufate kanuni za afya zilizowekwa na tuache kuupa airtime humu kwenye mitandao ndio tunaongeza hofu na taharuki kwa raia wakati hakuna dawa.
tuache kuupa airtime......... should we conceal true information about the disease?
 
Baba ameshasema
Screenshot_20210127-123736_WhatsApp.jpg
 
Mkuu wewe ndio baradhuli coz umetoa mfano wa kipuuz kwenye ishu sensitive. Malaria iko tofaut na Corona.Ugonjwa unaoambukizwa kwa hewa au kugusa HUITAJI DEBATE kujua upo au haupo...
Punguza upumbavu ufike mbinguni! Umeulizwa swali simpo tu, kwamba malaria ndio ugonjwa unao ongoza kwa kuua hapa tz. Je kwenu au kwa jirani au kijiji au mtaa wa jirani kuna mtu yeyote ushawahi kushuhudia kafa kwa malaria?
 
Hilo la kukimbilia chato unalisema wewe na ndio ungefaa kueleza kwanini umefikiri kakimbilia huko kujificha kwani huko chato ndio corona inaogopa kwenda ama vp? Au akienda Chato ndio hafanyi majukumu yake ya kawaida anajifungia ndani tu haonani na watu kuogopa corona?
Makao ya Rais ni ikulu na sio kijijini kwake. Tuliona mwaka jana alikimbilia huko fukuto lilipokuwa kubwa, mwaka huu nako kakimbia tena. Subiri akishakufa mamako au mumeo ndio utasadiki kuwa hii ngoma ipo
 
Haya sasa ushaambiwa kuwa mdudu hayupo, na hata akiwepo usimuogope na uchukue tahadhari...
 
Yeye anapambana kwa kijificha, sisi tujifiche wapi? Ikipamba mot anajificha machakani, ikipoa anarudi. Analetewa kla kitu kwa fedha zetu, maisha kama kawaida kwake, Sisi tujifiche wapi?
Kajificha wapi?

Umekatazwa kujificha? Au unataka uakajifiche nae?
 
Wariokufa kwa corona nawajua, tena ni ndugu katika familia,,,wewe kaa ukijidanganya corona haipo. Na mtakufa msipojiangalia.
Hafi mtu achaneni na propaganda za wazungu Tz iko salama.
 
Makao ya Rais ni ikulu na sio kijijini kwake. Tuliona mwaka jana alikimbilia huko fukuto lilipokuwa kubwa, mwaka huu nako kakimbia tena. Subiri akishakufa mamako au mumeo ndio utasadiki kuwa hii ngoma ipo
Mbona haina haja ya kuongea maneno makali tunajadiliana tu,hakuna niliposema hakuna corona bali nachokizungumzia hapa ni huko kusema Magufuli kakimbilia Chato kuogopa corona, ndiyo nauliza huko Chato ndio huwa hakuna corona? au kwamba akiwa Chato huwa kinafanyika nini cha tofauti na Dodoma?
 
Nimemsikia rais wetu akisema kuwa Korona haipo Tanzania mara akabadili lugha na kusema haipo nyingi sana kama nchi zingine.

Pia nimemsikia akisema kuwa kuna watu walikimbilia nchi za nje na huko walipewa chanjo ya Korona virus, hao ndio walioleta korona virusi hapa Tanzania.

Kwa kauli hizi za mkuu wa nchi ambaye yeye ndie anayejua kila kitu juu ya taifa letu, nimeishiwa pumzi maana nilikuwa najipa matumaini kuwa tupo salama na hata hii second wave ya korona virus haijatinga Bongo.

Nipo njia panda, maana lockdown kwa maisha ya bongo kama ngoma ikizidi kuenea huenda tukajikuta tunafia majumbani kwetu.
 
Pole na majukumu najua walio wengi mpo kwenye daladala au usafiri binafsi mkielekea nyumbani kwenu.

Bila kupoteza muda ngoja niende mojakwamoja kwenye kwenye topic, ikumbukwe yakua tangu covd 19 imeingia kulikuwepo na jitiada za awali za kuzuia wimbi hili ninakumbuka baada ya sintofahamu kwa kipindi fulani Rais wa jamuhuri alikuja na kauli yakua ambaye anapaswa kutoa taarifa juu ya covid ni wazir mkuu, Rais , makamu wa Rais .

Sasa la kushangaza siku mbili tatu watu wameibuka na uvaaji wa barakoa hii inamana wanataarifa zao juu ya huu ugonjwa na wameamua kuas maagizo ya serikal na kufata yakwao.

Maswali yangu ni je serikal imeshindwa kupata taarifa sahii juu ya huu ugonjwa na kuutangazia uma mpaka raia watafute taarifa zao?

Pia kama kuna kikundi au watu walioeneza taarifa je serikal itawafungulia kesi ya uhujumu uchumi? Karibu kwa mjadala.
 
Mshukuru sana JPM kwa kukuondolea HOFU, vinginevyo hata usingekuwa na nguvu ya kutumia hiyo device yako kuandika. You are such a clueless Behaviourist
Kuna njia sahihi zaidi za kuondoa hofu.Kuondoa hofu siyo kudanganya umma kuwa Tanzania hakuna Corona na matokeo yake watu wanaancha kuchukua tahadhari halafu watu wanaishia kupukutika kama nzige waliopigwa dawa.Alichofanya JPM ni crime against humanity.Anapaswa kushtakiwa kwa makosa ya mauaji ya halaiki.
 
Nashauri Vyombo Vyetu Vitusaidie Kwenye Kuwakamata
Niko Dar es salaam Kituo Cha Fire
Hapa Tutakuwa Tunawazoa Kama Senene
 
Back
Top Bottom