Ndugu zangu Watanzania, wasomi na wasio wasomi, Wenye uwezo na wasio na uwezo, ni kweli Corona ipo
Mwaka uliopita kuna namna Mungu alitupitisha, ilipoingia karibu Kila mwananchi alitaharuki, hofu ilitawala Kwa kila mtu, hii ilimaanisha kwamba, kufa kupo na kila mtu lazima apitie umauti Ila ni nani aliye tayari?? Hapo ndipo kwenye shida
Binafsi Naamini, Kwa maombi na kuvunja hofu mioyoni mwa Watanzania ilitusaidia kuvuka,
Dunia ipo katika wimbi la pili la maambukizi ya Corona na Tanzania ni sehemu ya Dunia, wanasayansi na watalamu mbalimbali hawalali usiku na mchana kutafuta walau tiba ya gonjwa hili la hatari
Awali watu walihoji juu ya uhalali wa Tanzania kubaki salama bila maambukizi kwamba, Kwani Mungu ni wawatanzania pekee?
Kule kulikoanzia dini mbona wanalia? Iweje Tanzania Tu? Ndugu zangu, Mungu amewaumba wanadamu Kwa kusudi lake yeye, Muda unapofika wa yeye kuvuna, huamua ni wapi atavuna Kwa Wakati upi na Mahali gani ataacha, hii yote ni Kwa ajili yake
Sasa Corona ipo Kwetu Tanzania, watu wanahangaika kujua ni wapi ulipo msaada, wengine wakidhani labda serikali Yao itasaidi, wengine wanamlaumu kiongozi mkuu wa nchi, hapa ukiniuliza Mimi sielewi ni Kwa mini analaumiwa, Kwa sababu, kuna serikali bhana hapa duniani, kuna viongozi ambao kila kukicha wamekuwa wakiweka na kubuni mipango mipya ya kupambana na Corona, lakini wapi, ndio kwaanza watu wanaangamia maelfu Kwa maelfu
Swali langu ni....ndio Corona Ipo Tanzani lakini Je, Tufanye nini ili tunusurike? Je ni kweli chanjo zinazolazimishwa mataifa wanunue zimewasaidia wenzetu ambao tayari wamejichanja? Mbona hayo mataifa wanazidi kuweka masharti mapya ya kuingiliana na mataifa mengine mbali na kwamba wanachanjo?
Huko tunakodhani wanafanya kitu, lakini ndio kabisaa!
Je, njia ipi Bora itakayo tunusuru Watanzania?
Nakuuliza wewe unayedhani Una njia Bora ya Sisi Taifa kunusurika na maambukizi ya Corona
Wanasansi wakinyoosha mikono juu, Mungu atatukuzwa
Stachanjwa chanjo ya Corona Licha ya kwamba hayo mafua yamenisumbua wiki mbili sasa