#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Tatizo tumemuamini Mtanzania mmoja na kumuona ana Akili kuliko wengine wote....

Tumemfanya yeye kuwa mungu-mtu na kuwasemea watanzania wengine wote na sisi tunamuamini....

Yeye naye ameota pembe na kuwa na kiburi na dharau zaidi ya Herode!
Iko Siku tutaja kumbuka shuka kumekucha...
Wewe ni mpumbavu sana! Unataka huyo mtu akufanyieje?

Sema wazi kwamba huyo mtu nataka afanye hivi na vile ili watu wasife, na unaposema wafanye hivi na vile useme ni taifa lipi limefanya na kuzuia vifo?
 
JPM hawezi kusema chochote mpaka dakika hii kwasabb so far ameshaaibika...japo hanaga aibu!.
Kaaibikaje sasa? Au ulitaka Magufuli akwambieje?

We unapoona mataifa makubwa tajiri kama USA wanavifo mpaka 2000 kwa siku utajilinganisha na sisi huku?
 
Nauli ya nn mkuu, nikiona ndugu yangu au rafiki zangu wa karibu wameugua nitaamini ila bado siamin hii kitu we endelea kujifukiza mkuu piga nyungu
Wewe ndugu zako wa karibu au rafiki zako wameugua UKIMWI ???
 
ASIE AMINI KAMA Uviko aka Covid-19 au almaarufu korona, atembelee hospitali ya agakan hapa dar,aone wenye hela wanavyohangaika na mapaipu ya puwani.
Ipo ile nyimbo inasema ....Nenda kaone mwenyewe utakuja kuwseemaa... sijui muimbaji ni King kikii au Abdallah Mwinshee sidhani kama ni Remi au ni Nuta jazz band. usifananishe na nyimbo za hawa wakata mauno wa siku hizi zinazovuma siku moja.
Haa haa "mtoto acha kupiga mayoe.. Acha watu waone wenyewe" umenikumbusha mbali sana.
 
Tatizo tumemuamini Mtanzania mmoja na kumuona ana Akili kuliko wengine wote....

Tumemfanya yeye kuwa mungu-mtu na kuwasemea watanzania wengine wote na sisi tunamuamini....

Yeye naye ameota pembe na kuwa na kiburi na dharau zaidi ya Herode!
Iko Siku tutaja kumbuka shuka kumekucha...
Hivi unaamini kama leo Magufuli akisema kuna Korona wale wote waliokuwa wanapambana kusema hakuna watabadili kauli na kusema IPO? . Hakuna Mtanzania anaweza kupigania haki yake SASA hivi hata wapinzani nawashauri wafanye kazi nyingine hii ming'ombe ni ya kuiacha mpaka ishike adabu.
 
Dodoma kuna MTU na dada yake wameongozana alitangulia mkubwa mdogo kakaa kwenye oxygen wiki mbili Jana kaondoka. Kikwete tunakushukuru Sana tena Sana, kweli we mswahili umejua kutushikisha adabu.
Nimezika Shangazi yangu na mumewe hapo Kitunda lerini, na nikaumwa mbaya mpaka leo sipo sawa kabisa.
Mwendawazimu mmoja linafungua domo lake chafu linatoa riha chafu Eti hamna Corona.
 
Kwani tupo milioni ngapi ? Ukichukua idadi ya waliofariki USA unaweza kuwafuta waZanzibari wote na bado ,inawezekana serikali inamkakati wa siri.ya kwamba hata na wao wapo tayri kujipunguzisha katika population yetu.
 
Ndugu zangu Watanzania, wasomi na wasio wasomi, Wenye uwezo na wasio na uwezo, ni kweli Corona ipo

Mwaka uliopita kuna namna Mungu alitupitisha, ilipoingia karibu Kila mwananchi alitaharuki, hofu ilitawala Kwa kila mtu, hii ilimaanisha kwamba, kufa kupo na kila mtu lazima apitie umauti Ila ni nani aliye tayari?? Hapo ndipo kwenye shida

Binafsi Naamini, Kwa maombi na kuvunja hofu mioyoni mwa Watanzania ilitusaidia kuvuka,

Dunia ipo katika wimbi la pili la maambukizi ya Corona na Tanzania ni sehemu ya Dunia, wanasayansi na watalamu mbalimbali hawalali usiku na mchana kutafuta walau tiba ya gonjwa hili la hatari

Awali watu walihoji juu ya uhalali wa Tanzania kubaki salama bila maambukizi kwamba, Kwani Mungu ni wawatanzania pekee?

Kule kulikoanzia dini mbona wanalia? Iweje Tanzania Tu? Ndugu zangu, Mungu amewaumba wanadamu Kwa kusudi lake yeye, Muda unapofika wa yeye kuvuna, huamua ni wapi atavuna Kwa Wakati upi na Mahali gani ataacha, hii yote ni Kwa ajili yake

Sasa Corona ipo Kwetu Tanzania, watu wanahangaika kujua ni wapi ulipo msaada, wengine wakidhani labda serikali Yao itasaidi, wengine wanamlaumu kiongozi mkuu wa nchi, hapa ukiniuliza Mimi sielewi ni Kwa mini analaumiwa, Kwa sababu, kuna serikali bhana hapa duniani, kuna viongozi ambao kila kukicha wamekuwa wakiweka na kubuni mipango mipya ya kupambana na Corona, lakini wapi, ndio kwaanza watu wanaangamia maelfu Kwa maelfu

Swali langu ni....ndio Corona Ipo Tanzani lakini Je, Tufanye nini ili tunusurike? Je ni kweli chanjo zinazolazimishwa mataifa wanunue zimewasaidia wenzetu ambao tayari wamejichanja? Mbona hayo mataifa wanazidi kuweka masharti mapya ya kuingiliana na mataifa mengine mbali na kwamba wanachanjo?

Huko tunakodhani wanafanya kitu, lakini ndio kabisaa!

Je, njia ipi Bora itakayo tunusuru Watanzania?

Nakuuliza wewe unayedhani Una njia Bora ya Sisi Taifa kunusurika na maambukizi ya Corona

Wanasansi wakinyoosha mikono juu, Mungu atatukuzwa

Stachanjwa chanjo ya Corona Licha ya kwamba hayo mafua yamenisumbua wiki mbili sasa
 
Sawa chukua tahadhari jikingine na kujiweka lockdown kama unauwezo haya yapo sio ni kuzidi kuelimishana
 
Hii ni vita ya kimya kimya, kila mtu apambane kujinusuru kwa kuchukua tahadhari. Ukipuuza shauri yako.
Mkuu, nakuuliza Kwa upole kabisa na Kwa sauti ya kunong'ona, Je unafahamu ni njia ipi nzuri ya kutuvusha juu ya hili gonjwa kaka
 
Tatizo vipimo ni ghali Sana tungepimwa wote ingesaidia Tatizo viongozi wengi walafi wanaacha kujikata mishahara yao tukapimwa corona Angalau
 
This is the most realistic comment I have read so far and I concur with you sir/madam
 
Leo nyuzi za corona zimeshamiri nasubr serikali ipige marufuku mazungumzo yoyote ya Corona
 
Back
Top Bottom