#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Kwamba dunia nzima wajinga ila sisi ndo werevu? Kuna watu hapa hawaamini kama ipo na hawachukui tahadhari yoyote. Hawajui second wave siku zote ni mbaya zaidi. I just lost a mtu wa karibu leo kwa changamoto hii, saaa kama hakuna isemwe basi hii changamoto ndo mlipuko mpya wa gonjwa ama? Linaitwaje?
 
Unataka Yohana ajidhalilishe kuwa maombi yake hayakufanya kazi?
Suala la maombi si Yohana tu hata ule waraka wa maaskofu katoliki pia nao ulisema kwamba mwaka jana tulifanikiwa mapambano dhidi ya corona kwa kufuata ushauri wa wataalamu pamoja maombi.
 
Mtaani watu wanaugua corona; wapo wanaofariki kwa corona. Watanzania, hasa wa mkoa wa Dar es Salaam na mipakani, wanaathiriwa pakubwa na ugonjwa huu wa corona. Katika hospitali zetu (hata viongozi wetu wanajua), wagonjwa wa corona wapo wa kutosha na kutisha.

Serikali yetu imeamua kufanya kazi sirini. Hadharani wananchi wanaambiwa hakuna corona. Sirini, kunatolewa maelekezo hata kwa wanafunzi wa Shule za Msingi kujifukiza na kuchukua tahadhari. Sirini ni tofauti na hadharani. Kwanini?

Hii ni nchi yetu. Afya na uhai wetu ndivyo vya thamani kwetu. Kuna haja gani kudanganyana kuhusu afya na uhai wetu sisi kwa sisi watanzania? Mheshimiwa Rais, Waziri wa Afya na viongozi wengine, taarifa zetu ni za muhimu kwetu kuliko mnavyodhani.

Corona ipo na inaua kila uchao, tuambiane ukweli ili tujiponye na kujihadhari!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Sasa hao viongozi mbona hawaonekani kujali afya zao kwa maana nao hawazingatii taratibu za kujikinga na huu ugonjwa,kuanzia rais mwenyewe hadi mawaziri wake wote sikumbuki hata mara ya mwisho lini kuwaona kuvaa hata barakoa tu. Hii ina maana gani hasa ukizingatia kama ulivyosema kwamba hao viongozi wanajua kabisa kuwa corona ipo na inaondoa watu?
 
Kwamba serikali ituambie naweni mikono kila wakati.

Kwamba serikali ituambie vaeni barakoa.

Kwamba serikali ituambie epukeni misongamano.

Wananchi ni vema kujiongeza wenyewe, afya yako binafsi ndio uhai wako chukua tahadhari.

Na nyie wenye mafua jitahidini kutulia majumbani kwenu kuepusha kupigia chafya raia wasio na hatia.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwamba serikali ituambie naweni mikono kila wakati.

Kwamba serikali ituambie vaeni barakoa.

Kwamba serikali ituambie epukeni misongamano.

Wananchi ni vema kujiongeza wenyewe, afya yako binafsi ndio uhai wako chukua tahadhari.

Na nyie wenye mafua jitahidini kutulia majumbani kwenu kuepusha kupigia chafya raia wasio na hatia.

Maendeleo hayana vyama!
It seems hujui hata wajibu wa viongozi uliowachagua.

Idiot.
 
Mtu wa kwanza kabisa anauetakiwa kutunza afya yako ni wewe mwenyewe
 
Ni kweli tusisubiri waziri ndio aseme tuchukue tahadhari za kujikinga na covid19.
 
... kwa hiyo serikali imejiondoa kwenye suala la korona? Kwamba haihusiki na lolote as far as COVID-19 is concerned?
Ndicho anachotaka kutuambia. Serikali ambayo ukitaja ugonjwa unafukuzwa kazi na kuitwa mhujumu uchumi
 
Back
Top Bottom