Ndugu zangu,
Wahenga walisema hivi "Mficha maradhi kifo humuumbua" Amiri Jeshi mkuu wangu Magufuli Kifo kinakuumbua
Sioni tatzio kama ukikubali kwamba Korona Ipo na ukachukua hatua za lazima kuhangaika suala hili.Mbona watanzania watakupa ushirikiano tu. Si uliona mara ya kwanza walivonunua ndoo wakanawa mikono na dala dala zikawa level siti na barakoa wakavaa na kujifukiza majani ya ajabu wakajifukiza?Kwani unaona aibu ya nini?
Hizi siasa na maisha ya watu zinakusaidia nini?ZInakupa faida gani?Au mpaka afe mtu wako wa karibu sana kama mkeo/mtoto wako ndo utaelewa kwamba siada katika maswal aya afya ni marufuku?
Mheshimiwa Raisi,Watu wanakufa kama nzi,Waziri wako wa Afya anamsifia mume wako na kutoa matamko ya taarabu.Hivi mantuaonaje watanzania?Mnatuona sisi ni Mbuzi sana na tunafaa kufa tu maana hatuna umuhimu.
Haya umekataa habari ya chanjo,umekataa kufanya vipimo na kutoa takwimu hata kuhamasisha watu wajikinge nako pia hutaki.Tunajua ulikaa kupima kwa sababu hakuna pesa ya kununua vipimo na tunajua umekataa kuchukua chanjo kwa sababu ya ukata lakini kwani kunawa mikono na kuvaa barako nako kunahitaji PESA yako.Si useme tu.
Ona sasa jinsi kifo kinavyotuumbua.Watu wanakufa kama kumbikumbi unataka tuwale nyama?Unafikiri utakuwa huna hatia kama kiongozi mkuu wa nchi?Unafikiri wewe upo salama?
Mheshimiwa chukua hatua.Fanya uamuzi kama rais anayejali watu.hata kama ni kuwafungia watu ndani wafungieni ila jamani watu wanadanja kama mzaa vile.
Hii kitu sasa haichagua,inazoa tu watu.
Hii kweli ni CORONA sasa sijui Ndo tunakufa wote?