Afya sio mali ya serikali,usisubiri mpaka ikuambie kwamba ipo ndio uanzae kuchukua hatua, umeanza vizuri, corona ipo duniani na TZ ni sehemu ya dunia. Chukua tahadhari DIPOTIVO ipo.
 
Kuna rafiki yangu yupo morogoro amenipigia simu Leo kuniambia kuwa Corona ipo nichukue tahadhari

Mtaani kwao modeko wamezika mtu alikuwa na dalili zote za Corona alipokuwa hai.
Pana watu yafaa washatakiwe kwa kumisslead watu Ili wapotee Hali wao wamejificha majumbani kwao kukimbia corona,nani alikuambia sisi ni kisiwa.
 
Ninapowapendea WaTZ ni hapa tu, ubishi na ukweli anaujua!!

Tanzania si kisiwa kwamba usiingie, kasema alikuwa na dalili kama....!! Mtu anauliza hakuna magonjwa mengine!! [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Kuanzia Desemba 29 nilianza kupatwa natatizo la kuhara na homa kali sana, nilipokwenda kupata vipimo sikukutwa na chochote, sikuridhika nikaanza kutumia mseto na flagili, hali haikutengaa sana kidooogo kuhara kukawa kumepungua.

Nikaenda duka la dawa za binadamu, nikajaribu kutoa maelezo yangu kwa jinsi ninavyosikia, mhudumu aidha ukapime ujue nini kinakusumbua au utumie dawa za typhoid, nikachukua cipro - hali ya kuahirisha ikawa imekata japo homa ikifika jioni inakuwa kali sana na kukohoa.

Nikatumiatumia tangawizi na limao hali ya kukohoa ikapungua kwa asilimia karibu 90.

Nikapata tena vipimo sehemu nyingine nikakutwa na viral blood infection/mchafuko wa damu, nikaanza dozi hata sijaimaliza hadi sasa na ninajihisi kupona kabisa huku nikiendelea na tangawizi sometimes.

NOTE: BAADHI YA MARADHI YANA DALILI ZA KUFANANA.
 
Kilichonifurahisha kwenye story yako ni kuwa ukimuona ameenda Chato, basi, corona ipo. Huwezi kutafuta ka fomyula kentine⁉️⁉️⁉️⁉️🤓🤓🤓🤓🤓
 
Tunataka serikali itupe majibu, tunataka kujua status ya hali ya Corona nchini, maana baadhi ya watu wanaoaga dunia kuna watu mitaani wamekuwa wakinong'ona kuwa Korona ipo na inang'ata

Wananchi tunataka majibu, tena majibu sahihi ya hili suala!
Majibu haya hapa toka kwa wazungu wanafurika nchini wakijua corona hamna.cheki mandege yanavyoshusha watalii hawana cha barakoa wala nini. Mleta mada una matatizo ya akili wahi mirembe haraka.

 
Jan 1 2021: Kifo cha baba mdogo, upumuaji.

Jan 14 2021 Kifo cha babu, upumuaji.

Wote walisaidiwa na mashine kupumua nyakati za mwisho za uhai wao.

ALLAH awarehemu.
HAWANA MAJINA NI WASIOJULIKANA?
 
Kuna Daktari Mmoja Rafiki yangu nilimuuliza kwanini kuanzia Mwezi Desemba 2020 hadi Januari 2021 Vifo ni vingi akajibu tu niwaulize Wachina.
Mkuu umehesabu hadi vifo vya ajali nini?maana mwisho mwa mwaka ajali nyingi.
 
Kwani kuna tamko la serikali lilishawahi kutolewa rasmi kuwaambia wananchi wake wasichukue tahadhari?wewe kama una mashaka vaa tu barakoa au tumia sanitizer pale inapobidi,pia jaribu kiasi unachoweza kuepuka mikusanyiko isiyo na msingi au keep distance popote unapokuwa kwenye mkusanyiko,hilo sio kosa la jinai,swala la afya ya mtu binafsi liko mikononi mwako mwenyewe.Unajua kabisa gears zote zinazotumika kujikinga ili usipate maambukizi halafu unalalamika eti unasubiri serikali ikwambie,hata kama itakwambia juwa kuwa haitakununulia vifaa kinga au wewe kupata unafuu wowote wa hivyo vifaa....
 
COVID ipo na uzuri haichagui, hata hao wanaosema haipo inaendelea kuwafyeka tu Jamaa zao na wao hawana kinga wala exception kusema COVID haiwezi kuwafikia.
Ndio Maana wame ji isolate, Mbochi Tocha
jikinge Mwenyewe usiwangoje wakwambie
Mkuu kama kweli ipo na inauwa sana watu kwanini sasa tuwe tunabishana humu? yani mie nifiwe na ndugu na jamaa zangu huku nikijua kwa sababu ya corona halafu nije humu kabisa niseme hakuna corona? au naona kabisa eneo nalokaa watu wanaugua isivyo kawaida na wengine wanakufa halafu nije nipinge humu mashaka ya uwepo wa corona?

Hivi kweli nikifanya nakuwa na akili ya aina gani au kwa kumfaidisha nani?
 
ushirikina huu
 
Corona ipo tena umepamba moto, watu wanakufa sana sisi tumeamua kuendekeza siasa. Uliza madaktari wa Muhimbili na Mloganzila wakupe picha kamili
Kwahiyo wagonjwa wakifikishwa hospitali hupimwa hadi corona na ndio hao madktari wanajua kuwa watu wanakufa sana kwa corona?
 
Ni maranyingi sana serikali hata Rais ameshasema kuhusu kuishi kwa tahadhari.
Wanaoongoza kusema hali ya maisha ni mbaya ndo hao wanatamani lock down,nchi tajiri zilitepeta kwenye lock down wakaamua kuachia.
Kikubwa ni kuishi kwa taahadhari na namna ya kujikinga imeshaelezwa na watu wote wanajua.
Tanzania kama taifa serikali imeruhusu njia za ziada za kujikinga na Covid kwa kujifukiza na kutumia dawa zingine za asili kama za NiMR.
 
Nilienda kuangalia mechi ya simba na platnum kwa makusudi walifunga baadhi ya mageti yakabaki machache matokeo yake kukawa na msongamano mkubwa wa watu kuingia tukawa tunajiuliza kama serikali ipo makini kuzuia Corona kama inatengeneza mrundikano wa makusudi
 
Kuna watu wanasema kuwa ishu ya Afya ni personal issue, kwamba wewe raia wewe mwenyewe chukua tahadhari!, ni sahihi kwa upande mmoja lakini siyo sahihi kwa upande mwingine kwa sababu kazi mojawapo ya serikali ni kuwa wakweli na kuupa umma information sahihi kuhusu hali ya situation ili hao raia wachukue tahadhari husika.

Ukisema korona ipo chukua tahari wewe mwenyewe ni sahihi, LAKINI SWALI LA MSINGI NI JE, WATANZANIA WANGAPI LEO HII WANAJUA, AU WANAAMINI KUWA KORONA IPO TANZANIA?

Serikali ilishatangaza ushindi dhidi ya Korona kitambo sana na ikaacha kutoa information zozote juu ya hali ya korona nchini na raia wengi wanaimini serikali yao kuwa korona haipo na hawachukui tahadhari yoyote.

Hapa ndo tunaitaka serikali itoke mafichoni iseme, Hapa Tanzania hii kitu ipo au haipo ili wale raia wanaoamini Tumeishinda Korona wasijiachie sana!
 
Jan 1 2021: Kifo cha baba mdogo, upumuaji.

Jan 14 2021 Kifo cha babu, upumuaji.

Wote walisaidiwa na mashine kupumua nyakati za mwisho za uhai wao.

ALLAH awarehemu.
Kama kusingekuwa na kinachoitwa corona basi pengine hivyo vifo hata usingekuja kuvizungumzia hapa ila kwa sababu kuna corona basi hayo matatizo ya kupumua na kuwekewa mashine za kuwasaidia kupumua yanaonekana kama ni mambo mapya yaliyokuja kipindi hiki cha corona.
 
Personally najua wawili Nancy kafiwa na mama mdogo wake na Witness mzee wake yuko hoi anajitibu hiyo Covid kwa mitishamba ingawa ana hali mbaya sana.

Hyo ni mifano miwili nayoweza thibitisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…