Jana uzi wangu ulipigwa pini! Nilikuwa nahusisha uhusika wa vifo na viongozi wanatuhamasisha hakuna korona ilihali wao wanajificha na wengi tuna taarifa wamepokea chanjo! . Mod aliogopa lakini ukweli ndio huo. Hii ni masacre! tupende tusipende. Nimezika kaka yangu! Mimi na familia yangu yote ni wagonjwa tumeenda hospitali tumerudishwa nyumbani! Tuende wapi??
 
Mimi huwa nawaza watoto wa shule ingawa wao "changamoto" haiwasumbui sana.
 
Pole sana ndugu yangu. Mzee laizer amazika ndugu watatu ndani ya juma lilopita, alianza mkewe, akafuata mamamkwe, akifuatiwa na shemejiye mjane wa marehemu kakaye.
 
Pole sana ndugu yangu. Mzee laizer amazika ndugu watatu ndani ya juma lilopita, alianza mkewe, akafuata mamamkwe, akifuatiwa na shemejiye mjane wa marehemu kakaye.
Umeipata hii ya wahadhiri wa SUA?
Dr Delphina-7/2/2021
Dr Mamiro Mume wa Delphina- 9/2/2021
Mama yake Delphina- 14th January 2021
Shangazi yake Delphina16 Jan 2021
Baba yake Delphina 23 Jan 2021
Shemegi yake Delphina- 16/1/2021
Dereva wake Delphina-10/2/2021
Wote walifariki katika kipindi kifupi.
Hizi Mbwa zinazojiita wanasiasa hawaniambii lolote sasa hivi. The suffering is beyond repair.
 
Pole sana ndugu, tuna ombwe la uongozi, mbaya zaidi wanaiona hali na vifo vya watu ila hawajali! Huwa naangalia wakienda kuwazika wabunge na wengine wenye vyadhifa, ndipo napokumbuka machoni kama watu.. . ila mioyo yao ni bora Simba mwenye njaa[emoji706]
 
Ndio maana nasema nijuu yake na serikali kwa ujumla kubadilika haraka au watatuingiza katika doa jeusi katika history ya nchi kuja kujisafisha tena itachukuwa miaka. sisi tuna history nzuri miaka yote hatujawahi kuwa hivi tulivyo sasa.

Kama nilivyosema Corona sio ugonjwa wa Tanzania tu huu ni ugonjwa wa dunia na ukishakuwa wa dunia maamuzi ni ya dunia sio ya mtu au nchi moja moja.

Kama kuna kipindupindu basi usafi ni lazima kwa kila mtu sio unasema mimi kwangu kusafi ila jirani hakufai kawaida anapigwa fine na kushtakiwa kwa kuwa unahatarisha mtaa mzima na wakazi wote sio wewe tu na ndivyo ilivyo corona.

issue yake ya kuponda chanjo sasa kwa data watu wamethibitisha kuna mafanikio yanaonekana. hatuwezi kudharau science ndio msingi wa kila kitu hata Mungu alisema soma, na science iko katika dini.
 
Senseless opinion
 
Nimeona matamko ya Wamarekani, Waingereza na sasa wajapan. Juzi waangola wametuonesha kuwa na afrika siye hatukaribishwi na yeyote.

Isipokuwa Tanzania na Burundi nchi zote zimekubali kupokea chanjo ya Covid19.

Ni Tanzania tu ambapo takwimu za vifo na wagonjwa wa covid19 haziwekwi wazi.

Ni Tanzania tu ambapo Rais anasimama majukwaani na kutangaza kuwa hakuna corona.

Ni Tanzania tu ambapo taarifa kuhusu korona ni classified!

Ni Tanzania tu ambapo raia wanakufa kwa korona lakini hakuna anayeruhusiwa kusema.

Ndugu wamekufa, watu ni wagonjwa, maisha ni jehanam tuende wapi?

Tujadili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…