Kwa wale Wakristu habari za Jumatano ya Majivu, kwa wengine habari za Great Thinkers
Niende kwenye mada yangu. Msingi wa hoja yangu unajikita katika mapambano ya ugonjwa wa covid 19.
1: Hatua za Kijamii
Kwa kweli hapa JF tumejitahidi kuishauri serikali kwa wazi kuwa itamke wazi kuwa Covid 19 imerudi, na hatua za kujikinga zakuvaa barakoa kwenye maofisi, taasisi za umma zitiliwe mkazo km kwanzia, kwenye mwendo kasi watu level sit na hivyo hivyo kwenye daladala, vitakasa mikono pamoja na kunawa mikono.
2: Maziko
Kwenye maziko km mhusika kafa kwa Covid 19 pia kuna hata ya familia yake ameambukiza hivyo kuwe nakutoshikana mikono pia kuwe na umbali katika misiba(social distance)
Nimehudhuria kanisa la Roma leo jtano ya majivu getini huingii km hauna barakoa pia lazima unawe na mnakaa umbali kati ya mtu na mtu binafsi naipongeza kanisa la Roma kuweka utaratibu kitaasisi.
3: Nashauri Serikali kuwa iwalinde Majenerali(Wababe wa vita na mbinu za medani wanazifahamu)
Hii kipengele cha tatu naiweka kwa upekee kabisa maana kwa sasa hivi vifo vya Mabrigedia zimekuwa kwa wingi na nimepenyezewa na watu wa ndani kuwa, taratibu za maziko yaani paredi zao zinaenda kwa rank (Mwili utabebwa na warank yako, sasa km amekufa kwa Covid na familia yake imeathirika ni wazi kuwa hawa wakuu wetu km wafariji wakwanza watachangamana, hivyo ni rahisi kupata maambukizi)...Vita hupiganwa kwanza mezani kabla ya medani sasa tuwalinde hawa majenerali ni lulu jeshini)
Hitimisho
Serikali kupitia waziri wa afya ituongoze kwenye hii vita, tuchukua hatua za kisayansi zaidi tuwape nafasi wataalam wa afya