#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Hii ngoma ni balaah hakuna kwenda kutibiwa ulaya wala nini, masikini na tajiri wote tunachangamana hapa hapa Bongo, kwel tumepatikana.
 
Unajua nini? Trump alifanya ujinga huu huu wa kutotoa mwongozo kuhusu juhudi za kujikinga mpaka mambo yakaharibika sana. Serikali ikiri kuwa Korona ipo na itamke wazi kuanzia sasa:

1. Kila mtu avae barakoa

2. Asichangamane na watu kila inapowezekana. Ikibidi kuchangamana basi kuwe na umbali angalau wa futi sita kati ya mtu na mtu kila inapowezekana.

3. Sanitizer kila mahali.

4. Watu wahimizwe kuwa waangalifu mf. kuacha kushikana mikono hovyo hovyo, kutorundikana kwenye mazishi na ikiwezekana wazee wajitenge na wasichangamane na vijana na watoto.

Na juhudi zingine za kawaida kama hayo malimau, tangawizi na nyungu kama zinasaidia kuwaondolea watu hofu hata kama ni placebo effects tu.

Barakoa na hatua zingine zinasaidia na kufanya kazi vizuri kama kila mtu atazifuata; na hili haliwezekani bila mwongozo wa serikali.

Inasemekana Trump angetoa mwongozo kama huu mapema angeweza kuokoa zaidi ya nusu ya watu waliofariki na Korona ambao wanakaribia laki 5 mpaka sasa.

Hata sisi hatujachelewa. Bado tunaweza kuzuia baadhi ya vifo kwa watu wetu vinginevyo tunakoenda hali itakuwa mbaya sana na tutachekwa na dunia nzima.

Na tuchague chanjo moja tuifanyie majaribio haraka tukijiridhisha basi watu wetu wachanjwe mara moja. This is ridiculous [emoji51][emoji51][emoji51]
 
Mkuu umemaliza kila kitu.
 
Baada ya kifo cha Nkurunzizah, rais wa sasa wa Burundi anachukua tahadhari zote kwa raia wake.
 
Hali ni mbaya kwa sasa hilo halina ubishi.

Cha kushangaza serikali bado iko na msimamo wake kwamba nchi haina korona, lengo ni nini hasa kuhusu huu msimamo wa serikali wakati hili ni janga la dunia nzima?

Kuna ubaya na madhara gani kutoa tahadhari kwa watu ili wajikinge?

Sasa hivi hakuna anaejali tena au kuchukua tahadhari, ni wachache sana wanaofanya hivyo.
 
Toka tu huko Machimboni mwaya...

Mtu aliyewaaminisha watanzania Corona haipo...

Juzi kati akawavimbia wazungu kuhusu chanjo...

Tusiangalie tutaonekaje mbele ya jumuia ya mataifa, bali tuangalie maisha ya Watanzania yanavyowekwa rehani na mtu mmoja.

Lets face it, statement za mkuu Rais zinafanya more damage, sio kwenye image yetu wa Tanzania bali kwetu sisi wenyewe kwa wenyewe maambukizi ya covid-19.

Yeye ni msomi wa kiwango cha uprofesa; tafiti hupingwa na tafiti. Sio unaamka asubuhi na kuropoka.

Anyway tuwache hayo, Janga ndio limeshatukuta.

What is the way foward? (michango yenu hapa inahitajika).

I just think president Magufuli atoke huko aliko auhudhurie mazishi ya makamu wa kwanza wa Rais Seif Hamad aliyefariki kwa Covid

Aseme Tanzania kuna Corona, tujikinge na atoe guidelines.

Just to honour him, kifo chake ki-save maisha ya Watanzania wengine..

Au mnasemaje?

Becky
 
Atleast hata kipindi kile walikataza mikusanyiko,kuvaa barakoa,kunawa kila mahali,kwenye madaladala level seat hahaha saivi ndo hawasemi kitu wataanzia wapi wakati walisema hamna corona aiseee na wakapaaaamba kuwa wameweza wanaonaa aibuuuu. Huuu sio muda wa kuona aibu hali ishakua mbaya
 
yani kujikinga na korona hadi uambiwe na rais hayo machanjo tunasikilizia kwanza waliojichanja yamewapalua ama la sio sisi tuwe wa kufanyiwa experiment mbona huko ulaya wamechanjwa na bado wanavaa barakoa tumsapoti rais move anayofanya ni nzuri au nasema uongo ndugu zanguuuuu
Tokkujikingao Machimboni mwaya....

Mtu aliyewaaminisha watanzania Corona haipo...

Juzi kati akawavimbia wazungu kuhusu chanjo....

Tusiangalie tutaonekaje mbele ya jumuia ya mataifa..

Bali tuangalie maisha ya watanzania yanavyowekwa rehani na mtu mmoja,

Lets face it, statement za mkuu Rais zinafanya more damage,sio kwenye image yetu wa tanzania bali kwetu sisi wenyewe kwa wenyewe maambukizi ya covid-19

Yeye ni msomi wa kiwango cha uprofesa; tafiti hupingwa na tafiti

Sio unaamka asubuhi na kuropoka,

Anyway tuwache hayo,

Janga ndio limeshatukuta,

What is the way foward? (michango yenuhapa inahitajika).

i just think president Magufuli atoke huko aliko auhudhurie mazishi ya makamu wa kwanza wa Rais Seif Hamad aliyefariki kwa Covid

Aseme Tanzania kuna Corona,tujikinge na atoe guidelines

Just to honour him, kifo chake ki save maisha ya watanzania wengine........

Au mnasemaje?

Becky
 
Wacheni Kutegemea mtu nae ni mtu kama Nyie
Hata akitoka aseme haitasaidia kwani hamuoni hatari hii ni kubwa?? Tujisaidie wenyewe akitoka pengine ndio aseme Mungu ametenda muujiza utafanyaje??
 
Tunataka kutatua tatizo la Corona Tanzania kwa kujidanganya kuwa Tanzania hakuna Corona!
2825585655.jpg
 
Kutoka 14:8

Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu zaidi.
Kutoka 14:8-9,13-14
[8]Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri.
[9]Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni.
[13]Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.
[14]BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
 
Back
Top Bottom