#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Usitukane mamba kabla hujavula mto.

Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.

Walishafanya makosa na sasa wanaona aibu kula matapishi[emoji38]
 
Covid is ReAL, Serikali itangaze ili Wananchi wasipuuze. Kama kuna hatua zakuchuliwa kitaifa zitangazwe pia.
 
Vifo hivi viwili hasa siku ya leo, Makamu wa Rais Hamad Sherif na sasa shocker, Katibu Mkuu Eng John Kijazi.

Hii ni dalili tosha kwamba mheshimiwa una msimamo usio na tija kwa afya ya watendaji na wanasiasa wako serikalini au chamani.

Kwa spidi hii ya vifo vya viongozi na hakuna msimamo wenye tija kuepusha janga la corona, basi tutapoteza wengi.

Mheshimiwa Rais badili msimamo sasa, watu/viongozi wavae barakoa, hatua za kujikinga kwa kupunguza mikusanyiko zichukuliwe.

Its now or death looms.
 
La msingi kujihadhari kadri tuwezavo kwasababu hata hayo mataifa yaliondelea Wana kila kitu Ila bado Hali ni tete kwa waliopoteza ndg zao poleni sana maradhi ni sababu tu Ila unapofika muda wa mja kuondoka hakuna kitakachoweza kuzuia Mungu atupe subra katika nyakati hizi ngumu
 
Unafikiria kama wasingekuwa na "kila kitu" hali ingekuaje?
La msingi kujihadhari kadri tuwezavo kwasababu hata hayo mataifa yaliondelea Wana kila kitu Ila bado Hali ni tete kwa waliopoteza ndg zao poleni sana maradhi ni sababu tu Ila unapofika muda wa mja kuondoka hakuna kitakachoweza kuzuia Mungu atupe subra katika nyakati hizi ngumu
 
Kwa wale Wakristu habari za Jumatano ya Majivu, kwa wengine habari za Great Thinkers...
Aya yako ya mwisho (Hitimisho) ndio yenye hoja ya mashiko, kama tu kila mtu atatimiza wajibu wake kama ilivyokuwa wakati UKIMWI ulivyotangazwa. Tulijawa hofu na kunyanyapaana. Je, UKIMWI haupo au hauuwi?
 
Kwanza nitoe pole kwa wote waliofikwa na misiba ya wapendwa wao. Wapumzike kwa amani.

Kwa hakika sasa vifo vimeongezeka, hapa nazungumzia watu wenye nyadhifa mbalimbali serikalini, achilia mbali wananchi wa kawaida ambao habari zao hazitangazwi. Kama hawa viongozi hawafi kwa corona, je ni nini kinachowaua tena kwa mfululizo namna hii?

Kama sio corona basi hali ya hospitali na huduma zetu za afya nchini ni dhaifu mno tofauti kabisa na jinsi hii serikali inavyojinasibu kuboresha miondumbinu ya afya. Kama watu wanaopewa first class treatment on everything wanapoteza maisha hivi basi raia wa kawaida don't stand a chance.

Kama ni corona, serikali ifanye jitihada za makusudi na za haraka za kuongeza vifaa tiba na kuhimiza tahadhari juu ya huu ugonjwa kuokoa maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom