Kwenye suala la Ulinzi wa mwili hapo Mungu sidhani kama ataweza maana kama ingewezekana najua kwa imani aliyo nayo Rais angesema hata walinzi hataki amemwachia Mungu. Maana atakaye ikoa nafsi yake ataipoteza.
Kwani Corona inaingia kwenye mwili au kwenye nini?
 
Pamoja na kuonfoa hofu katika jamii, suala la maambukizi mapya, 2nd wave ya covid 19 bado limekuwa tishio kubwa.

Madaktari bingwa na wanasayansi waliobobea wameluwa kimya utafikiri wamewekewa maji baridi.
Kama kuna kada itaokoa wananchi na janga hili ni utaalam wa kidaktari na afya ya jamii.

Cha ajabu sasa hivi waongeleaji wakubwa wa ugonjwa utokanso na maambukizi ya covid19 ni wanasiasa na watu wa dini, makasisi, maaskofu na mashekhe.
Mara tusivae barakoa, mara tumepona Mungu ameponya, mara tuvae tena barakoa!
Hii ni ajabu sana kwa Tanzania.
Hivi hatuna Dkt Fauci wa Tanzania?
 
Kama kweli nyie ni wapenda ukweli amkeni usiku wa manane muone buguruni palivyojaa watu wakihangaika, huyu anaemda Kariakoo,huyu Ubungo ,yule G mboto. Kwa ujumla ni mshikemshike. Watu wako busy kusaka maisha yao.

Ninyi mpo mitandaoni, mnakesha kueneza kile ambacho hakipo. Maana hata kama kuna uwepo wa Covid 19 sio kwa kiasi mnachokieneza kwenye mitandao.

Mbaya zaidi wengine mpo Usa,Uk na Sweden. Mnaishi kwa migongo ya kodi za wazungu. Lakini kila siku ni kueneza uongo kuhusu Tanzania. Kama hali ni mbaya kiasi hiki, hivi hapa bongo tutaishi?

Huko mikoani watu wako busy wanalima,wanafanya biashara. Ninyi mmebakiza kupiga propaganda za uongo kama kwamba sasa watu wanadondoka kama mdondo.

Kweli tatizo lipo maana Tanzania sio kisiwa, lakini mnaeneza uongo mwingi kuliko uhalisia.

Kumbukeni Mungu ni muweza, na anawalinda Watanzania. Hata kama mlitaka kushudia maelfu wanakufa kwa siku,Mungu atawalinda.
 
Nadhani kuna kitu hakipo sawa, ingawa changamoto ya ukimya iliyopo itawamaliza kimya kimya.

Tumeusiwa kutokuongea bila data, ila hii kada ya afya pia wanaondoka mno kutokana na covid. Nadhani hawachukui tahadhali za kutosha wanapowahudumia wagonjwa wao.
 
Pamoja na kuonfoa hofu katika jamii, suala la maambukizi mapya, 2nd wave ya covid 19 bado limekuwa tishio kubwa...
Kwa hiyo wewe unataka waseme nini? Madaktrai unawategemea wako chini ya mkono wa Mungu unayemdharau. Na usipotubu upumbavu wako wa kumdharau Mungu, shauri lako. Endelea kukufuru. Sisi tunajua wave ya kwanza ya COVID 19 Mungu alituponya na madaktari walishuhudia hili. Leo wewe unajifanya mungu mpumbavu.

Ni mpumbavu kwa kuwa hata maelekezo ya rais huwezi ku yelewa. Wapi amesema usivae barakoa? Mbona wewe juha sana? Kama hrauwezi kuelewa ama kwa ushetani wako unabadilsha statement za Magufuli ili kumfurahisha shetani, huwezi kumwelewa Fauci na ndiyo sababu unamshangilia.
 
Kwa hiyo wewe unataka waseme nini? Madaktrai unawategemea wako chini ya mkono wa Mungu unayemdharau. Na usipotubu upumbavu wako wa kumdharau Mungu, shauri lako. Endelea kukufuru...
Utanisamehe ndugu yangu.

Unachosema ndio upotoshaji wa hali ya juu katika gonjwa hili.

Kwa hiyo mtu akiambukizwa aende kanisani au msikitini kusali na kuswali?
Huu ni ujinga uliopitiliza.

Na hao madktari bingwa tumetumia fedha nyingi za kodi zetu kuwasomesha. Mbona hatuwasikii katika suala la Public Health katika hili, misingi ambayo ni ya kisayansi.
 
Utanisamehe ndugu yangu.
Unachosema ndio upotoshaji wa hali ya juu katika gonjwa hili....
pale politics onapo zidi professiinalsm. ndicho konachotokea sasa. Hata madaktaru bingwa wameshindwa kuwa na msimano kabisa. wote wanasifu na kuabudu.. taaluma wameweka mfuko wa nyuma.

kisa mtu mmoja tu. ambae hana taaluma hiyo. kwa umoja wao MAT wanashindwa nn?
 
and maybe wana uhaba wa vifaa. so wanafanya kazi kwa mazingira yale yale.
ndio maana wanakuwa exposed, lakin wapi watapeleka malalamiko haya? maana kila mahali ni siasa
 
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi mpaka serihakijui mipaka ya kisiasa...
Hivi Ni kweli hujasikia serikali ikihimiza watu kuchukua tahadhari? Hata kule kuambiwa tumia barakoa uliyoshona mwenyewe ni tahadhari kubwa Sana dhidi ya Corona, je hujawahi kusikia?
 
Kama kweli nyie ni wapenda ukweli amkeni usiku wa manane muone buguruni palivyojaa watu wakihangaika, huyu anaemda Kariakoo,huyu Ubungo ,yule G mboto. Kwa ujumla ni mshikemshike. Watu wako busy kusaka maisha yao...
Ni kweli kabisa! Akifariki mtu tu tayari ni kosa kana kwamba kabla ya Corona watu walikuwa hawafi!

Kabla ya Corona changamoto za kupumua zilikuwepo na zilishika nafasi ya pili Tanzania na duniani kwa ujumla kwa kusababisha vifo. Takwimu hizi kazionesha naibu waziri wa afya Jana asubuhi wakati akihojiwa na watangazaji wa Wasafi Redio.

Leo hii mtu akifa kwa changamoto ya upumuaji wahuni akiwemo zytow wanasema Ni corona!! Ili mradi tu mabwaana wao mabeberu wafurahi!!!
 
Lazima tuji ulize maswali. Rais Magufuli pamoja na team yake ikulu lazima wanafahamu vizuri sana kuhusu ugonjwa huu wa corona, athari zake na njia za kuji kinga. Wao kusema kwamba hatuhitaji lockdown wala chanjo zinazo tolewa nchi zingine na ku ongezea haya kwa kusema kwamba tumtegemee Mungu kutusaidia ni njia moja ya kusema kwamba

1. Tuna fahamu kuhusu Janga hili vizuri ila tatizo hili halipo Tanzania

2. Takwimu za waathirika wa ugonjwa huu nchini hazipo

3. Takwimu za waathirika wa ugonjwa huu nchini zipo ila hatutaki kutangaza

4. Waathirika wa Corona wapo nchini ila tatizo limefanyiwa kazi na kwa uhakika watanzania walio wengi wata nusurika..

- Kama kweli kuna waathirika wa Corona Tanzania, ni lazima wahusika serikalini wanafahamu kwamba huwezi kusema Mungu atasaidia bila kuchukua hatua zingine kulinda watanzania wote. Yanayotokea sasa hivi yame kusudiwa
 
Hivi ulimsikia naibu waziri wa afya alipokuwa anazungumza na watangazaji wa Wasafi Redio? Je alikuwa anaongea Siasa au sayansi ya tiba? Hoja zake zimesimama kisayansi na dunia inajifanya kuwa haijamsikia kumbe imekosa namna ya kujibu hoja zake!!
 
and maybe wana uhaba wa vifaa. so wanafanya kazi kwa mazingira yale yale.
ndio maana wanakuwa exposed, lakin wapi watapeleka malalamiko haya? maana kila mahali ni siasa
Exactly, wana vifaa duni vya kujikinga wakati wa kufanya utabibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…