#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Kilichomuondoa Trump sio issue ya korona pekee ni mjumuiko wa mambo mengi sana.
 
Naam!
Assalamu alaikum.

Moja ya sababu kubwa kabisa zilizomfanya Donald Trump asiendelee kuwa rais wa Marekani ni namna mbovu alizotumia kukabiliana na janga la korona.

Ni wazi sasa hata rais wa Tanzania, mheshimiwa John Magufuli anatakiwa ajitathmini kama anastahili kuendelea kuwa rais.
Asubuhi njema.
Kwa hiyo wewe unasemaje? Unataka raisi atangaze lockdown nchi nzima

Kama tungekaa lockdown ya covid-19 ina maana sasa hivi tungekuwa tunajiandaa tena kuanza Lockdown ya virusi vipya kama ambavyo Kenya wanajiandaa hivi sasa kuanza tena lockdown
 
Wapiga kura wa tz sio sawa na wamarekani mkuu ... tofauti yao ni kama mbingu na ardhi...
Wapiga kura unawaonea tu. Katiba mbovu ya mwaka 1977 ya chama kimoja ndiyo mzizi wa haya matatizo yote.

Wenzetu wanatanguliza maslahi ya Nchi na mtu au chama hufuata! Ila sisi ni Chama cha Mapinduzi kwanza halafu Nchi na watu ndiyo hufuatia.
 
Kwani katiba inatungwa na akina nani? My point is still valid.
 
Au mnataka mpaka watu waanze kufa na corona kwenye ma bus ndio mstuke. Why isiwe level sit hata kwa mwezi mmoja.
 
Huyu mgeni kutoka china yuko nchini na anapiga kazi kimya kimya.

USHUHUDA.

Nina rafiki yangu anakaa mikocheni hii ni wiki ya pili sasa hali yake angalau imeanza kutengama.
Alianza kujihisi uchovu kupumua shida na mwili kuuma, akaenda hospital wakapima damu na mfumo wa upumuaji wakamwambia ana virus katika mfumo wa upumuaji.

Mwishowe wakamwambia wazi kuwa usiwe na hofu utapona wakampa dawa pamoja na kumwambia atumie tangawizi achanganye na chai. Ametumia Tiba hiyo leo ijumaa ndiyo ameaanza kwenda kazini na walimwambia wazi ni corona.

USHUHUDA WA PILI.

Ndugu yake pia na huyo huyo yeye hali ilikuwa mbaya zaidi kalazwa hospital wiki mbili naye pia ilifikia hatua wakamwambia wazi kuwa ni corona, lakini Mungu ni mwema wote wanaendelea vizuri.

USHAURI.

Corona ipo ila inamuathiri mtu kutegemeana na kiwango cha kinga ya mwili wake,,wapo wanaougua kidogo na wapo wanaozidiwa zaidi, na kwa kuwa tumeshaaminishwa haipo basi hatulipi kipaumbele tena na kuonesha kuwa ni tishio.

Hivo tuendelee tu kujifukiza na ukiumwa nenda hospital mapema, wengi wao wanapona bila shida.
 
kuna jirani yangu hapa Mbezi alianza kuumwa wiki iliyopita akapelekwa Massana hospital, akawekewa Oxygen wiki nzima, juzi kaambiwa Oxygen ya Massana haitoshi kwa hatua aliyofikia, akahamishiwa Lugalo na jana alfajiri amefariki.
Corona ipo tena ya kipindi hiki ni hatari.

Afya yako siyo mali ya serikali, chukua tahadhari.
 
Mtaani kuna wazee watatu wamedanja wamepishana siku 2 mbili, chanzo ni vifua kubana, nilikuwa nachukulia poa ila hivi vifo vya hawa wazee vimenifanya niamini
 
Hamna kitu kinaniuma Kama Raisi wa nchi kufanyia hili janga mzaha na kuwa na kebehi.

Asiweke lockdown ila asisitize watu kujikinga na huu ugonjwa. Ata Kama watu wanakufa wachache, uhai wa mtu mmoja unathamani Sana.

CHUKUA TAHADHARI CORONA IPO NA INAUA KWELI KWELI.
 
Mtaani kuna wazee watatu wamedanja wamepishana siku 2 mbili, chanzo ni vifua kubana, nilikuwa nachukulia poa ila hivi vifo vya hawa wazee vimenifanya niamini
Ukweli ni huo tuendelee kujifukiza tu
 
Ukweli,ni huo kama hujapata ushuhuda kwa mgonjwa unaweza sema haipo ila kiukweli ipo
kuna jirani yangu hapa Mbezi alianza kuumwa wiki iliyopita akapelekwa Massana hospital, akawekewa Oxygen wiki nzima, juzi kaambiwa Oxygen ya Massana haitoshi kwa hatua aliyofikia, akahamishiwa Lugalo na jana alfajiri amefariki.
Corona ipo tena ya kipindi hiki ni hatari.

Afya yako siyo mali ya serikali, chukua tahadhari.
 
Ukienda hospitali unakuta kuna vifaa vya kunawia, wanakuambia magonjwa ya kuambukiza ni mengi hakikisha unanawa.
 
Back
Top Bottom