#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Kweli mdau...covid 19 ipo..ila kuna watu wanajitoa ufahamu humu....kwamba hakuna...mpaka jamaa zao wafariki ndio wataamini hii kitu ipo.
Tatizo tumemuamini Mtanzania mmoja na kumuona ana Akili kuliko wengine wote....

Tumemfanya yeye kuwa mungu-mtu na kuwasemea watanzania wengine wote na sisi tunamuamini....

Yeye naye ameota pembe na kuwa na kiburi na dharau zaidi ya Herode!
Iko Siku tutaja kumbuka shuka kumekucha...
 
Wakuu me mbona nashinda kariakoo daily na sipati corona?? Au askari wenu wapo weak?? Kuna watu wanaumwa mafua wanasema corona[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
Watu tuko tofauti sana unaweza kuwa umepata lakini usiumwe kabisa wala kuhisi na hao ni wengi sana na uhakika watu wakienda kupima wengi watakutwa na antibodies kuashiria wamepata na wamepoma bila kujuwa. Kukujibu yes, watu hawafanani wako inawachukuwa vibaya na wako ndio wengi wanapata bila kujuwa. Muhimu ni kuwa makini maana hatujui kesho yetu au ya ndugu zetu.
 
Mzee amefariki kwa kovid leo.....tunamsika saa 10.....alifikia hatua ya kukohoa damu nyeusi na alikuwa hawezi kupumua,huku mapafu yakikaza sana,tuwashauri wazee wetu wenye umri 70+ wakae home tu kama hakuna umuhimu wa kutoka
Watu wanakufa kila kuchwao na ina sikitisha Tanzania limekuwa ni Taifa la wasioweza kuhoji,

Kuna suala limetokea Jana Kibaha Kongowe ni hatari sana , watu sita wamekufa kwa sababu ya Corona

Watu wanakufa wanakufa wanakufa nasema wanakufa
 
Mzee amefariki kwa kovid leo.....tunamsika saa 10.....alifikia hatua ya kukohoa damu nyeusi na alikuwa hawezi kupumua,huku mapafu yakikaza sana,tuwashauri wazee wetu wenye umri 70+ wakae home tu kama hakuna umuhimu wa kutoka
Pole sana mkuu
 
Wakuu me mbona nashinda kariakoo daily na sipati corona?? Au askari wenu wapo weak?? Kuna watu wanaumwa mafua wanasema corona[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
Asilimia kubwa wenye umri mkubwa ndiyo wameathirika.....kariakoo ipo vizuri tu,mtaa niliopo kuna mtu amepoteza baba yake,baba mdogo na baba mkubwa last week,aliugua mmoja
........wakaenda kumjulia hali bila tahadhari,wameachiana siku 3 tu....kuna bank siitaji amekufa mmoja watatu wapo mahututi akiwepo collegemate wangu mmoja.....
 
Lets do the math Wataalamu wanasema 5% ya wanaopata Corona wanakufa..., hivyo kwenye watu mia watano watakufa....

Na inavyoambukiza na Chanjo hatutaki wala sidhani kama tuna mpango wa kutengeneza ya kwetu..., hivyo basi graph ya vifo itaongezeka mpaka ifikie peak (hopefully tumeshafika kwenye peak) yaani it will get worse before it gets better..., Na hii herd immunity (watu wote lazima tutapata tu kama ipo) kwahio mwisho wa siku wa kufa wakishakufa vifo vitapungua na hapo tutasema Corona tumeifukuza, kumbe waliobaki wana immunity...

Na tutaendelea hivyo mpaka ikibadilika tena tunaanza tena Mwanzo..., kwahio inabidi wataalamu washirikiane pande zote kuutokomeza huu ugonjwa na sio kubezana..., unless otherwise huenda mimi au wewe tukawa katika hao 5% soon or later..., au mbaya zaidi ika-mutate na kuua sana kuliko sasa....
 
Na hili ndio tatizo yani wanasema hakuna corona hawapimi watu corona hakuna takwimu na wanaosema watu wanakufa kwa corona hawana ushahidi wowote wao hujiamulia tu kuhusisha vifo vya watu na corona wamejipa haki ya kuongea pasina ushahidi ukawabishia wanakwamnia Tz sio kisiwa. Kuwepo na wenye kuamnisha watu kuwa hakuna corona sio sababu ya wewe kuaminisha watu corona ipo kwa kueleza yale usio na uhakika nayo. Kuna watu walikuwa wameshikilia kabisa kuwa Magufuli kakimbilia chato kwa kutuaminisha kuwa ni sababu ya kuepuka na mlipuko mpya wa corona.
 
Wakuu me mbona nashinda kariakoo daily na sipati corona?? Au askari wenu wapo weak?? Kuna watu wanaumwa mafua wanasema corona[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]
Naona unaibeep,ikukupigia usiaanze kulia
 
Nakubaliana na Askofu Bagonza kwamba maisha ni mali ya mtu binafsi. Jukumu la kwanza la kila mtu kuhusu kuchunga usalama wa afya na uhai wake ni lake mwenyewe na kamwe hawajibiki kufuata amri, ushauri, maelekezo au fikra za mtu mwingine wakati anaona kwa kufanya hivyo anahatarisha maisha yake. Tuchukue tahadhari
 
Sawa pia Maoni ya mtu mmoja Magufuli hayaondoi haki yangu ya msingi ya kupata chanjo
 
Huku nilipo naona watu wanaendelea na maisha kama kawaida sijasikia vifo ila tahadhari ni muhimu siwezi sema chochote sababu data za wanaoumwa au kufa na corona sizijui
 
Asilimia kubwa wenye umri mkubwa ndiyo wameathirika.....kariakoo ipo vizuri tu,mtaa niliopo kuna mtu amepoteza baba yake,baba mdogo na baba mkubwa last week,aliugua mmoja
........wakaenda kumjulia hali bila tahadhari,wameachiana siku 3 tu....kuna bank siitaji amekufa mmoja watatu wapo mahututi akiwepo collegemate wangu mmoja.....
Unadhani hivyo vifo vya kufuatana hivyo havikuwepo before corona? binafsi mwaka juzi nimefiwa na watu wangu wa karibu ndani ya wiki moja na wote walikuwa wanaishi eneo moja ilikuwa mshangao kwa majirani ingekuwa kipindi basi bila ya shaka hivyo vifo vingehusishwa na corona.
 
Watu wanakufa kila kuchwao na ina sikitisha Tanzania limekuwa ni Taifa la wasioweza kuhoji,

Kuna suala limetokea Jana Kibaha Kongowe ni hatari sana , watu sita wamekufa kwa sababu ya Corona mi familia ya Mr Gaudence, na nyingine ya Mzee John Chillo,

Watu wanakufa wanakufa wanakufa nasema wanakufa

Naona Melo na Mods wakitaka kuufuta Uzi huu plz msiufute Corona ipo watu wawe aware
Wewe ni msemaji wa hizo familia au mna hisia ni corona? Weka ushahidi wako hapa kama wamefari kwa covid-19 wa vyeti vya vifo vyao.
 
Corona ipo jamani. Yani wikii hiii baba yangu kapoteza marafiki wanne kwa covid. Na wote hawajaugua sana ndani ya masaa 24 mtu anaishia. Tuchukue tahadhari zote. Na ya safari hii haingalii umri ikikushika sana yoyote unaenda
 
Watu tuko tofauti sana unaweza kuwa umepata lakini usiumwe kabisa wala kuhisi na hao ni wengi sana na uhakika watu wakienda kupima wengi watakutwa na antibodies kuashiria wamepata na wamepoma bila kujuwa. Kukujibu yes, watu hawafanani wako inawachukuwa vibaya na wako ndio wengi wanapata bila kujuwa. Muhimu ni kuwa makini maana hatujui kesho yetu au ya ndugu zetu.

Point mkuu tuendelee kupiga nyungu
 
Back
Top Bottom