#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Inaonesha hali ni mbaya ndio mana kajisogeza Dar mwenyewe ili awe karibu na hospital
 

Yehoshafati Anamtumaini Yehova​

Yehoshafati ni mfalme wa ufalme wa makabila mawili ya Israeli. Anakaa wakati mmoja na Mfalme Ahabu na Yezebeli wa ufalme wa makabila 10. Lakini Yehoshafati ni mfalme mzuri, na Asa baba yake alikuwa mfalme mzuri pia. Basi watu wa Ufalme wa makabila mawili wanafurahia maisha mema kwa miaka mingi.

Lakini sasa kunatokea jambo la kuogopesha watu. Wajumbe wanamjulisha Yehoshafati hivi: ‘Jeshi kubwa kutoka nchi za Moabu, Amoni na Mlima Seiri linakuja kukushambulia wewe.’ Waisraeli wengi wanakusanyika Yerusalemu wamwombe Yehova msaada. Wanakwenda katika hekalu, na huko Yehoshafati anasali hivi: ‘Ee Yehova Mungu wetu, hatujui la kufanya. Hatuna msaada juu ya jeshi hili kubwa. Twakutumaini utusaidie.’

Yehova anasikiliza, anamtuma mtumishi wake awaambie watu hivi: ‘Vita si yenu, bali ya Mungu. Ninyi hamtapigana. Tazameni tu, mwone jinsi Yehova atakavyowaokoa ninyi.’

Basi kesho yake Yehoshafati anawaambia watu hivi: ‘Mtumainini Yehova!’ Kisha anaweka waimbaji mbele ya askari zake, wakimsifu Yehova wanapotembea. Unajua linalotokea wanapokaribia vita? Yehova anafanya askari maadui wapigane wao kwa wao. Na Waisraeli wanapofika, kila askari adui amekufa!

Je! Yehoshafati hakuwa na akili kwa kumtumaini Yehova? Sisi pia tukimtumaini Yeye, tutakuwa na akili.1 Wafalme 22:41-53.

Haya ndio tunayopaswa kuyafanya kipindi hiki,ni kumtanguliza Mungu ili atupiganie na kutuvusha kwenye kipindi hiki kigumu.
 
Nitawalaumu waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari maana wameshindwa elimisha jamii.
Ni kweli mkuu, lakini wangeweza kweli kuwa na ujasiri wa kumpinga mkuu Rais anachosema?
 
Serikali inagwaya kukiri kwa Covid 19 ni kujishusha kisiasa, huku wapinzani wakiitumia COVID kujipandisha kisiasa. Shida inaanzia hapo.
 
Ndugu zangu kulalamika hakujawahi kutatua tatizo kama una jipu tumbua na sio kulalamika jipu linauma,huku huchukui juhudi zozote kuliondoa...
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Waalimu na baadhi ya watoto wa shule ya kulelea watoto yatima kituo cha Mashima Usseri Wilayani Rombo wamelazwa katika Kituo Cha Afya Karume kwa changamoto ya mafua makali, vikohozi na kuumwa kichwa.

Ni taarifa tu.

USHAURI: Usisubiri kuambiwa na mwanasiasa kwamba kuna korona, chukua tahadhari.
  • Nawa kwa sabuni na maji tiririka kila Mara.
  • Vaa barakoa
  • Epuka maeneo ya misongamano na usitembee hovyo km huna sababu ya kufanya hivyo.
  • Epuka kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana. Nk
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo poleni kwa misiba inayotokea ila ndio mwisho wa binadamu lazima tukubali ila ningependa kushauri kwa sasa watu wenye umri kuanzia 55 nakuendelea walazimeshwe kuvaa barakoa baada ya hapo serikali iweke utaratibu maalum wa mazoezi kwa wenye kuweza huku tukiebdelea kuchukua tahadhari.

Nawaambia watanzania wenzangu huu sio mda wakutafuta watu wakuwalaumu huu mda wakusaidiana na serikali ili sote tuwe salama naona kuna watu wanashindwa elewa maana ya upinzani matokeo yake wanatandaza chuki kipumbavu kama kweli ipo corona tuchukue tahadhari na habat soda
 
Tatizo la kila mtu anataka kumuaminisha mwenzake badala ya kujadiliana kwa hoja. Mtu anataka kukuaminisha hakuna corona hali ya kuwa hatupimi corona na kutoa takwimu ili kuthibitisha kweli hakuna,mwengine nae anakwambia corona ipo na watu wanakufa halafu ushahidi hana anabaki kusema Tz sio kisiwa.
Wewe umetoa hoja ipi hasa?
 
Hii ya kudiscourage watu kujikinga, kufanyia mizaha barakoa, kila mara kutangaza kuwa korona haipo iliwafanya wananchi wengi washushe guard zao na wengine waamini moja kwa moja korona haipo!. Sasa ikipiga tena inawakuta wananchi wamerelax hawana habari!..
Ndugu Missile uko sahihi kabisa!
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo poleni kwa misiba inayotokea ila ndio mwisho wa binadamu lazima tukubali ila ningependa kushauri kwa sasa watu wenye umri kuanzia 55 nakuendelea walazimeshwe kuvaa barakoa baada ya hapo serikali iweke utaratibu maalum wa mazoezi kwa wenye kuweza huku tukiebdelea kuchukua tahadhari nawaambia watanzania wenzangu huu sio mda wakutafuta watu wakuwalaumu huu mda wakusaidiana na serikali ili sote tuwe salama naona kuna watu wanashindwa elewa maana ya upinzani matokeo yake wanatandaza chuki kipumbavu kama kweli ipo corona tuchukue tahadhari na habat soda
Serikali imeshajitoa kwenye huu msala imekuachia wewe mwenyewe uhangaike nao. Yenyewe inaendelea tu kuingiza watalii nchini bila kujali kuna uwezekano mkubwa wao ndo wametuletea msala huu kwa kiwango kikubwa
 
BVICHA ...mnalalamika afu hamtuletei dawa ....[emoji1][emoji1][emoji23][emoji23]
nadhani huu si wkt wa kuweka siasa kwenye mambo ya muhimu.
kazi ya serikali ni nini kama hata wataalam wetu wameshindwa tu kutengeneza dawa licha la kuwapeleka nje kusoma?

si kazi ya chama cha siasa kuleta dawa
 
Huyu naye, ukibishana na watu wa aina yako kwanza unaweza jikuta hata wamekuambukiza 'viakili vyao'..!
Hey, bado hujapona tu🤔! Pole, usijali Mungu akusaidie utimamu wa akili ukurudie!
 
Back
Top Bottom