#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Watanzania jitahidini kufanya mazoezi hasa push ups ili kuongeza uwezo wa ufanyaji kazi wa mapafu,
Hasa watu wazima na watu wenye miili mikubwa
 
Kwa wale wanaotumia vilevi kama pombe na sigara, mjitahidi kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya hivyo vilevi kwa kipindi hiki cha huu ugonjwa ili kuongeza ufanisi wa mfumo wa upumuaji
 
Watanzania jitahidini kuongeza matumizi ya vyakula vya asili kama mboga mboga, matunda, mafuta ya mimea, vitunguu swaumu, limao, tangawizi n.k
Ili kuongeza kinga ya mwili
 
Jitahidi sana kukaa mazingira safi yasiyokua na vumbi, moshi na harufu kali hii inaenda sambamba na usafi wa mashuka na blanket za kulalia ili kufanya upumuaji wako uwe mzuri, pia hakikisha mazingira ya nyumba au ofisi ni masafi
 
Watanzania punguzeni safari zisizo na lazima ili kupunguza athari za maambukizi ya huu ugonjwa, kwani huu ni ugonjwa usioonekana kwa macho, haijulikani nani anao na nani hana.
Hivyo tujitahidi kutofanya safari zisizo na lazima.
Katika hili pia ikiwezekana ni vyema watoto wakabaki nyumbani badala ya kwenda shule, kwani uhai ni muhimu zaidi kuliko pesa na elimu ya duniani.
Pia katika hili ninashauri serikali iangalie namna ya kuwalinda watoto mashuleni na vyuoni
 
Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali.

Ila ni wachache sana wanakuja na ushauri au solution kutokana na wingi wa vifo hivyo.

Inajulikana Corona ipo nchi nyingi, imeua na inaendelea kuua watu duniani kote.

Hivyo kama watanzania wenye akili timamu bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa, kidini, kikabila n.k ni vizuri tukawekeza nguvu kubwa katika kutoa mawazo ya kujenga kuhusu namna ya kupambana na huu ugonjwa.

Hivyo kwa yeyote mwenye mawazo mazuri ya namna ya kupambana na huu ugonjwa ni vizuri akashauri vyema sababu Corona haichagui mtu wa kumuondoa, pia ugonjwa wa Corona haujaletwa na serikali au Raisi Magufuli hivyo matusi, kejeli, dharau na vitu vya namna hiyo kwa serikali sio sawa.
Huu ni UTOPOLO, ukifiwa na ndugu yako wa karibu, hutoandika ungedere huu
 
Huu ni UTOPOLO, ukifiwa na ndugu yako wa karibu, hutoandika ungedere huu
Acha kukalili wewe Buji,
Kwa hiyo unataka nilaumu au kumtukana Magufuli na serikali kuhusu Corona ndio uone nimeweka mada nzuri.
Kuna mda wa propaganda za siasa na kuna mda wa kutoa mawazo mbadala
 
Serikali kama serikali, haijatangaza rasmi uwepo wa ugonjwa wa Covid 19 hapa nchini. Kinachotokea ni watu waliopaswa kutoa hizo taarifa, kuzitoa kwa mafumbo na kukwepa kabisa kuutaja ugonjwa huu kwa jina lake kama lilivyo.

Wanaotaka serikali itoke hadharani kutamka wazi uwepo wa Covid wanachukuliwa kama wapinzani, wakiambiwa na wale wanaounga mkono ukimya wa serikali kuwa wajilinde wenyewe maadam wanajua ugonjwa huu upo.

Ni sawa kwamba watu wajilinde wenyewe, wachukue tahadhari wenyewe kwa sababu uhai ni wao. Lakini kwa nini ninadhani ni muhimu serikali itangaze uwepo wa ugonjwa huu hapa nchni?

Huu ni ugonjwa wa maambukizi, unasambaa kwa kasi na unaua kwa haraka. Unapaswa kupigwa vita na wote kwa pamoja. Kushoto wanashambulia, kulia wanashambulia, mbele na nyuma wanashambulia.

Mwenye uwezo wa kuwaingiza watanzania wote vitani dhidi ya ugonjwa huu ni serikali peke yake. Serikali itaagiza tahadhari ziwe ni lazima na siyo hiyari. Leo hii watu wanajazana kama kawaida kwenye daladala. Gari haiachi mtu njiani.

Kwa kutaka kila mmoja ajilinde mwenyewe maana yake hili ni suala la utashi. Huyu anajali yule hajali. Tukumbuke ugonjwa ukija hauchagui kama huyu anajali au hajali, kwani hatujaona madaktari wanaowatibu wagonjwa wa Covid wakifa?

Hakuna aibu kwa taifa letu kuwa na Covid, kwani sisi nani katika hii dunia?

Hatuna shida na takwimu, tunahitaji nguvu ya pamoja kupambana na kiongozi hapa ni serikali.

Nimeikopi kama ilivyo toka Facebook
 
Acha kukalili wewe Buji,
Kwa hiyo unataka nilaumu au kumtukana Magufuli na serikali kuhusu Corona ndio uone nimeweka mada nzuri.
Kuna mda wa propaganda za siasa na kuna mda wa kutoa mawazo mbadala
Sasa huyo Magufuli nimemtukana tusi gani?
Ninachosema Magufuli atimize wajibu. Kimya ni jawabu la mpumbavu.
Atoe amri, vyombo vya usafiri wa umma, turudi kwenye level seats.
Kinyume na hapo atakuwa anafanya genocide
IMG-20210218-WA0075.jpg
 
Hayo ni mawazo yako,
Ila kuna mada za kuweka masihara.
Kama wewe haujafa leo basi mshukuru Mungu, ila inawezekana kesho ukafa wewe au mtu wako wa karibu.
'Mamlaka' inasema hiyo kitu haipo macho makavuuuu,
mimi ni nani niseme vinginevyo?
wewe nani unipinge?
Sikuelewi ujue.
 
Sasa huyo Magufuli nimemtukana tusi gani?
Ninachosema Magufuli atimize wajibu. Kimya ni jawabu la mpumbavu.
Atoe amri, vyombo vya usafiri wa umma, turudi kwenye level seats.
Kinyume na hapo atakuwa anafanya genocideView attachment 1705913
Katika hizo hoja zako naungana nawe kabisa, kuna haja serikali kutoa kauli kuhusu mustakabali wa wananchi na huu ugonjwa
 
'Mamlaka' inasema hiyo kitu haipo macho makavuuuu,
mimi ni nani niseme vinginevyo?
wewe nani unipinge?
Sikuelewi ujue.
Kuna kujikinga kwa mtu binafsi na Kitaifa,
Kwa sasa kila mtu binafsi ajikinge, huku tukiendelea kusubiri tamko la Kitaifa toka serikalini
 
Back
Top Bottom