#COVID19 Serikali isiwaache Wananchi katika mataa kwenye suala la Corona
Tatizo mnaficha vifo hamtaki watu wajue kuwa wanakufa kwa corona. Sasa kama mnaficha na mnasema corona hakuna unategemea ushauti atoe nani wakati hamtaki kukubali kwamba tatizo lipo? Kubalini ukweli na watu watatoa ushauri unaousema
Nakuunga mkono, huo ndio ushauri unaotakiwa.
 
Watanzania wanamuamini kiongozi wao, ndiyo maana hata wasomi kama katibu mkuu kiongozi huku wakijua kabisa kuwa korona ipo ila walisimamia imani ya boss wao.

Uliona jana kijana amesimama mbele ya jeneza la Kijazi pengine ni mwanae, yupo hana barakoa, sasa si muwaambie wavae, au mnapenda kuzika.

Waambieni watu wajikinge wanangojea kauli za nyie mliowaaminisha kuwa korona ni kwa mapapai mbuzi na mafenesi.
Safi sana kwa ushauri mzuri,
Unajua watu wengi bado hawajajua kwamba huu ni ugonjwa mpya hivyo elimu kubwa sana inahitajika kwenda kwa serikali na raia wa kawaida.
Elimu kubwa sana kuhusu Corona inahitajika, hatujui huu ugonjwa utaisha
 
Nimeona watu wengi wanalaumu serikali hasa Rais Magufuli kuhusu vifo hivyo vinavyohusishwa na ugonjwa wa Corona,
Wengine wanakejeli, kutukana, kebehi n.k kuhusu serikali...
Mawazo mazuri sana. Wapo wanaotoa kipaumbele katika kuitukana Serikali, hususan Rais JPM. Wanakazia Rais atangaze kwamba corona ipo nchini wakati watu hao hao hawazingatii mawaidha yanayotolewa ya kutojumuika kwenye mikusanyiko isiyo ya lazima, kuvaa barakoa, n.k. Tumeona ilivyokuwa kwenye mazishi ya Maalim Sef Hamad.

Waombolezaji hawana habari kabisa na kinga zinazohitajika. Inakuwa kama Rais akitangaza tu kwamba corona ipo, ugonjwa ndio utakuwa umekwisha. Watanzania tuweke pembeni hoja za kisiasa. Tufuate mawaidha tupewayo na kuacha mambo ya siasa kwenye nyanja za siasa.
 
Huo ndio ushauri unaohitajika na nakupongeza kwa hilo.
Umetoa ushauri na maoni bila matusi wala kejeli kwa Serikali ni vyema zaidi sababu inapelekea kujenga mshikamano baina ya serikali na wananchi.
Matusi, kejeli, mashinikizo n.k mara nyingi havijengi
Wengi wanaokejeli ni kwakuwa serikali kupitia raisi walisema tz huko hakuna korona wakati si kweli, watu kila siku wanakufa bado serikali wameleta jina jipya changamoto ya upumuaji na si korona
 
Mawazo mazuri sana. Wapo wanaotoa kipaumbele katika kuitukana Serikali, hususan Rais JPM. Wanakazia Rais atangaze kwamba corona ipo nchini wakati watu hao hao hawazingatii mawaidha yanayotolewa ya kutojumuika kwenye mikusanyiko isiyo ya lazima, kuvaa barakoa, n.k. Tumeona ilivyokuwa kwenye mazishi ya Maalim Sef Hamad. Waombolezaji hawana habari kabisa na kinga zinazohitajika. Inakuwa kama Rais akitangaza tu kwamba corona ipo, ugonjwa ndio utakuwa umekwisha. Watanzania tuweke pembeni hoja za kisiasa. Tufuate mawaidha tupewayo na kuacha mambo ya siasa kwenye nyanja za siasa.
Nakupongeza kwa ushirikiano,
ugonjwa wa Corona ni mpya, hivyo elimu kubwa sana inahitajika kwenda Serikalini na wananchi wa kawaida
 
Unadhani kwanini hawakulaumu wewe na familia yako bali Serikali (inayokusanya Kodi) na Kiongozi (aliyejitokeza kuongoza..., by the way sio kwamba alilazimishwa...)
 
Sasa huyo Magufuli nimemtukana tusi gani?
Ninachosema Magufuli atimize wajibu. Kimya ni jawabu la mpumbavu.
Atoe amri, vyombo vya usafiri wa umma, turudi kwenye level seats.
Kinyume na hapo atakuwa anafanya genocideView attachment 1705913
Kwani wewe huwezi kuona kama gari limejaa ukaacha kupanda???Hadi uamrimshwe???? Hiyo ni akili ya kitumwa
 
Kwani wewe huwezi kuona kama gari limejaa ukaacha kupanda???Hadi uamrimshwe???? Hiyo ni akili ya kitumwa
CCM Chama Cha Mazezeta. Mmeshindwa kufikiria, hata kuwaza pia?

Sio kila mtu anapandia mwanzo wa safari, kiasi kwamba ubahatike kukuta gari haijajaza.

Pili, unaweza kupata siti, umevaa na barakoa. Barakoa inakuziba pua na mdomo, si macho. Muathirika aliyesimama anapiga chafya, wadudu wanakurukia machoni.

Hebu acheni uzezeta wenu, hata Kama mna mtindio wa ubongo anzeni kujitoa huko sasa
 
Ushauri unatakiwa kuwa mwingi kadiri iwezekananyo, na ushauri isiwe kwenda serikali tu bali iwe hata kwa wananchi wenzetu wa kawaida kwa kuelimishina nini cha kufanya na nini cha kuacha ili kujikinga.
Izingatiwe huu ni ugonjwa mpya hivyo elimu yake inahitajika sana
Huu ugonjwa siyo mpya. Una upya gani na ugonjwa ulianza tangu mwezi March mwaka jana?
 
Pombe zipi mkuu wakati tunaziita sanitizer huku
Kwa wale wanaotumia vilevi kama pombe na sigara, mjitahidi kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya hivyo vilevi kwa kipindi hiki cha huu ugonjwa ili kuongeza ufanisi wa mfumo wa upumuaji
 
Uko sahihi kwa namna moja,
ila kwa namna nyingine unaweza ukawa sio mtalam wa fani yeyote ila kwa uzoefu kutokana na kuona, kusikia au kusoma kuhusu Corona ukawa na mawazo ya kushauri serikali, ijulikane huu ni ugonjwa mpya hivyo tukiwa na mawazo mengi toka kwa watu tofauti tunaweza tukafanikiwa.
Asante. ila narudia: Sisi raia tumemwajir rais. Anawatendaji na vitendeakazi vyote vinavyohitajika.
 
Naona Serikali inakwepa jukumu lake la msingi hasa kwenye janga hili la CORONA la kuhakikisha ustawi wa Wananchi wake na imeegemea zaidi kwenye jukumu la viongozi wa dini la kuhubiri imani.
 
Kuna kujikinga kwa mtu binafsi na Kitaifa,
Kwa sasa kila mtu binafsi ajikinge, huku tukiendelea kusubiri tamko la Kitaifa toka serikalini
Huko ni kuenda kinyume na mamlaka,
Rejea hadhara ya kumuaga 'Mhandisi' leo.

Viongozi wajuu wote waliokuwepo kwenye Hadhara hakuna aliethubutu kuvaa hiyo kitu,
Nani hajipendi?

Au unadhani hawajitambui wale?
 
Nimepitia video ya YouTube ya Magufuli



Anasema hakutakuwa na lockdown, lakin the way anavyoongea anaonekana ku surender fulani ametambua alikosea kutoa tamko kwamba Tanzania Hakuna Corona, na ikamuumbua ikagonga juu kabisa,

Kuhusu meseji alosema kutumiwa na Prof Mpango tutaiamini vipi kama ameweza kuudanganya Umma kuwa hatuna corona?

Tujihadhari Corona ipo

Big UP Jakaya Umeonesha Mfano

Britannica
 
Back
Top Bottom