Ndugu zangu Watanzania,
Serikali yetu kupitia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kupitia idara zake zote za usalama.ziwe macho na kuwa karibu sana na lissu na kumfuatilia nyendo zake pamoja na Mambo yake yote.
Kwa kuwa ni wazi lissu anatambua na kufahamu wazi kabisa hawezi kupita na kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA.hivyo lissu anaweza kutumia wakati na kipindi hiki cha uchaguzi kupitishia pesa chafu pamoja na kufanya utakatishaji wa pesa kutoka nje ya Nchi,.ambazo atazitumia kuvuruga amani ,utulivu na usalama wa Taifa letu.
Anaweza kufadhiliwa na wenye nia mbaya na chuki binafsi na serikali yetu kumpatia mapesa Mengi wakati huu halafu aje asitumie baada ya kumalizika kwa uchaguzi wao wa ndani kuleta uchochezi na kuhamasisha vurugu,ubaguzi ,chuki na mgawanyiko miongoni mwa watanzania.
Ikumbukwe ya kuwa Lissu hana uchungu na Taifa hili maana hata familia yake upo nje ya Nchi ambako hata yeye mwenyewe huenda na kushinda huko wakati wote.nawakumbusheni pia ya kuwa Watoto wa lissu wana uraia wa nje.kwa hiyo lissu hawezi kuumia wala kusikitika wala kuwa na uchungu machafuko yakitokea katika Taifa letu.maana hiyo ndio kiu yake kubwa inayochochewa na uchu,uroho na tamaa ya madaraka iliyo mjaa kifuani pake.
Kwa hiyo ni muhimu kwa idara zetu kutupia jicho kwake ili asije ingiza mapesa machafu na utakatishaji wa pesa zitakazotumika kuunda magenge na vikundi vya kujifanya vya kiharakati ambavyo vitaleta uchochezi hapa Nchini.
ikumbukwe kuwa hiki ni kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu ambapo siyo wote wanaofurahia kuona Taifa letu likiendelea kutamalaki kwa amani na kuwa kisiwa cha amani Barani Afrika na Duniani kote kwa ujumla wake.
wengine hatuna kwa kukimbilia yakitokea ya kutokea kama ilivyo akina lissu ambao wao huhamasisha vurugu huku wakiwa na tiketi ya ndege mifukoni kwa ajili ya kukwea ndege na kwenda ulaya huko kutumbua Maisha. Sasa wewe mtanzania mwenzangu ni vyema ukalijua hili mapema na kuwa mzalendo kwa Taifa hili.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
##
Lucas Mwashambwa mbona una hofu sana na Tundu Lissu kiasi cha kuwa na mawazo ya kijinga na kipumbavu hivi kwa Mwenyekiti wetu wa CHADEMA Taifa...?
## Tundu Lissu amejaliwa na Mungu silaha moja tu kubwa ambayo ndiyo anayoitumia kiasi cha watu kumwelewa na kumfuata kirahisi tu...
##Amejaliwa hili➡➡➡
UWEZO WAKE WA KUJENGA HOJA ZA KUSHAWISHI na KUELEWEKA KIRAHISI HATA KWA MAMA ASIYEKWENDA SHULE KULE KIJIJINI...
=====Hiki☝🏻☝🏻☝🏻ndicho watawala wanachokiogopa, basiiiiii=====
##Ukitaka kuthibitisha hili nenda kule kijijini (jimboni kwake Singida Mashariki) ambako amewahi kuwa mbunge kwa mihula miwili. Kila mtu kwenye jimbo hilo anazitambua haki zake na CCM na ulaghai na dhuluma zake, ilishakataliwa huko, haina chake 100%...!!
##KWA HIYO, BINAFSI, naelewa msingi wa hofu yako. Kwamba huyu mtu akipata platform pana ya kusemea (uenyekiti wa CHADEMA) nchi yote itawekwa kwenye darasa lake la kuwafanya wananchi wajitambue na watambue haki na wajibu wao wa kulinda haki zao dhidi viongozi mahayawani wa CCM na serikali yao....
Kwenu ninyi hayawani wachache wa CCM, akitokea mtu mwenye authority ya kuwaamusha watu toka kwenye usingizi wa UJINGA na KUTOJITAMBUA na kutotambua HAKI na WAJIBU wao kiasi cha kuonewa na kunyanyaswa na watawala makatili na hayawani wa CCM, mnamwita huyo mchochezi, mleta fujo na vurugu na kila jina lenye sifa mbaya kinyume na uhalisia wake....
Huyu ndiye tunamtaka sisi wananchi....!!
NAKUJULISHA TU KUWA, MAMBO YAKO HIVI:
1. Tundu Lissu pesa zake tunazo sisi wanachama, mashabiki na wafuasi wa CHADEMA. Atatembea nchi nzima kujenga POLITICAL AWARENESS kwa wananchi wote kwa gharama ya fedha toka kwa wananchi wakiwemo wana CCM wasio machawa ambao nao wamepigika tokana uchafu na ufisadi wa serikali ya CCM wa miaka karibu 65 sasa...
2. Tundu Lissu NDIYE MWENYEKITI WA CHADEMA (2025 - 2029) iwe CCM na "wasiojulikana" wanataka au hawataki...
3. Mambo ya utakatishaji pesa, yako huko CCM. Au hujui kuwa mtakatishaji fedha mkuu nchi hii kwa sasa ni Samia Suluhu Hassan na mwanae Abdul? Hujui kuwa ni mawaziri wote wakiongozwa na Mwigulu Nchemba...?
Mnafikiri watu hawajui, au siyo....?
Unadhani hatujui ni kwanini mfumo wa serikali hii ya kishetani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan haingependa kumuona mtu safi & mwadilifu, jasiri, msemakweli, mwenye maarifa na ufahamu, mwenye internal & international influence ya kutisha Tundu Lissu awe kiongozi mkuu wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani..?
Ni kwa sababu TUNDU LISSU ni NURU ya taifa na nchi hii. Na NURU inapoingia mahali, GIZA huogopa na kukimbia..!!
KWA HIYO NURU (HAKI) na GIZA (USHETANI WA CCM na SERIKALI YAKE) unajaribu kupingana na nuru, unajaribu kuizima Nuru....
Historia iko very clear, kwamba, GIZA HALIJAWAHI KUISHINDA NURU. Yesu Kristo (Nuru ya Ulimwengu) hakushindwa na GIZA (shetani)...
Hata SHETANI alipojaribu kutumia silaha yake ya mwisho, inayoogopwa sana na watu wote yaani KIFO na MAUTI, navyo havikumshinda Mwamba YESU KRISTO. Alikufa na siku ya tatu alifufuka na YU HAI LEO NA HATA MILELE...
Vivyo hivyo Tundu Lissu. Risasi 16 ndani ya mwili wake hazikuweza kuchukua uhai wake ili apate kutimiza kusudi aliloletwa kulifanya hapa duniani na specific hapa Tanganyika...
Hivyo,
Lucas Mwashambwa mnatwanga maji kwenye kinu kupambana na mkono wa Mungu...!!