Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Viongozi wetu wengi wamevembewa hawana uwezo tena wa kufikiria
 
Only in Tanzania

Kwani wao wanajali awafahamu zama hizi za globalisation kuna mtu huko South Afrika au Nigeria anafyonza keshaweka hela yake anasubiri matokeo halafu wao wanamuwekea usiku.

Akija kusikia sababu zenyewe sasa za mechi kucheleweshwa, we Tanzanians are not serious people.
 
Haya sasa waangalie huo uzinduzi wenyewe na ndugu zao sasa... this is stupid kabisa.
 
Hakika na bado mtajionea mengi nyie endeleeni kuipamba serikali ya mama yenu na kuidharau serikali ya hawamu ya tano.
 


Umesema kweli kabisa mkuu.

Nyongeza ni kuwa kuna watu wizarani wanaingilia masuala ya soccer.

Ni kosa kubwa sana kufanya au kusababisha mashabiki kusafiri kutoka kona zote za nchi, wengine kutoka nchi jirani, wasafiri kwa usafiri wa nchi kavu, majini na angani, walipe malazi, chakula, usafiri wa ndani ya jiji, acha kiingilio walicholipa na kuingia uwanjani kabisa!!!

Then MTU mmoja kutoka wizarani anatoa amri mchezo sio saa 11 jioni ni mpaka saa moja jioni kinyume kabisa na taratibu za muda halali unaopaswa kutolewa taarifa ya kuahirisha mchezo.

Hatujakaa sawa mpira umeahirishwa hauchezwi leo!!

Vipi kuhusu gharama za hao mashabiki?

Vipi wale waliocheza michezo ya
online betting ?

Serikali ituambie vizuri gharama hizo zitalipikaje????
 
You have a point.

Ila serikali nayo wana sababu na nafikiri kikubwa ni kwamba Mzee Mwinyi pamoja na kuzndua kitabu chake leo pia ni siku yake ya kuzaliwa yaani ametimiza miaka 96.

Hivyo serikali imeonyesha udhaifu wake kiutendaji kwa kushindwa kupanga uzuri siku ya leo ili isiingiliane na mechi ya mpira wa Simba na Yanga.

Walipaswa kuliona hilo kitambo na kujipanga uzuri.

Haya masuala ya kudarizi shughuli kama hizi "in last minutes" ni kasoro kubwa za kiufundi ambazo zahitaji marekebisho ya haraka.
 
Nilidhan huu uzwazwa umekwenda na mwendazake kumbe bdo upo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…