Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Ina uma Sana ndugu Zanguni

Imagine Mwanao yupo China amekataliwa kuja Tanzania Wakati huo huo Nchi inapokea Watalii kutoka kutoka huko huko China

Mbona Mnatufanyia hivi Serikali ya Awamu ya Tano ??

Mnataka tufe Kama kuku waliovamiwa na Mdondo ??

Mkuu umeniwahi, nimeshangaa sana serikali kugomea ndugu zetu kurudi kwa kigezo cha kukwepa maambukizo, lakini inawapokea wachina watalii kisa pesa! Ni kweli tunahitaji pesa, je pesa hizo ni hizi za hatari kiasi hiki ambacho tumefikia mahali pake kujitoa utu?
 
Mbona Kenya nao wameruhusu ndege iliyojaa watalii toka huko China; kwani si mnasemaga tuwaige wakenya, au?
 
Mkuu Sukaredi Woli, ucha dharau, usiwadharau kabisa darasa la saba, kuwaita wajinga na mazuzu, hivi kabla ya kuja wakoloni na kuleta elimu hii ya Wazungu, mababu zetu wote walikuwa wajinga na mazuzu?. Hivi unamjua Tajiri bilionea No. 1 TZ ni nani na inaijua elimu yake?.

Jee unajua kuna ma geniuses kibao ambao hawakwenda shule?. Hii elimu ya darasani na vidato, isitupe kiburi na dharau ya kutukana watu wajinga na mazuzu bila sababu. Heshima kitu cha bure.

P.
 
Yaani huyu msemaji wa serikali ni mpuuzi kabisa. Mataifa makubwa, yenye teknolojia ya hali ya juu katika tiba, wameona janga la huu ugonjwa na ugumu wa kuudhibiti, wamepiga marufuku wasafiri toka China, sisi tunawakaribisha.

Kweli sisi ni vichwa vya panzi!

Hivi tunaamini kuwa hela ya watalii kutoka China inazidi thamani ya uhai na afya za Watanzania? Kama tunawapenda sana Wachina na tumeamua kufa nao, nashauri wakifika tu airport wapokelewe kwa tahadhari maalum, wasafiri kwa magari maalum, kisha wakafungiwe ikulu, wakae siku 14, ikiwa wapo salama, ndiyo waruhusiwe kwenda sehemu yoyote ndani ya nchi.
 
Kwan huo ugonjwa upo china nzima au whuhan?
Kupokea watalii toka china sio lazima watoke china mainland,kuna hong kong na macau zote china
Lete details za hao watalii kwanza kabla ya kuja kulia humu
Jielemishe kuweza kujua jinsi ugonjwa huo ulivyoenea China nzima licha ya kwamba ulianzia jimbo moja.
 
Huu ugonjwa Inavyosemakana ngoz nyeusi hautupati,had sasa haluna report inayoonyesha mwafrica ngoz nyeus amefariki au kuambukizwa...kuna jambo lakujifunza hapa
Upo mbali na Dunia. Wapo walioambukizwa, na wakalazwa.
 
hatujitambui
Hao siyo watalii, ni wakimbizi wa Corona huko kwao, wanakuja huku kutulia mpaka huko kwao hali iwe shwari, Na you never know wengine wwnaweza kuwa na virusi vya ugonjwa huo
Wanashuka Kia tunawapakia kwenye mabus Hadi Gurmet hotels hukohuko Serengeti Wala hamna shida
 
Mzee wa magogoni anakucheki tu bagosha anasema hi hiiiii usinijaribu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda serikali haina fedha so fedha yoyote itakayopatikana vyovyote vile kwa gharama yoyote ni sawa tu, hatuiachii. Ila msisahau hawa wachina ndio marafiki wetu wa kweli , wana hela nyingi mpaka za kukopesha marekani, tukijifanya kuwazuia, wanaweza kutunyima misaada sisi donor country.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…