Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Bahati mbaya sana umemuonea Ummy mwalimu kwa kosa ambalo sio lake yeye kama yeye hana mamlaka ya kufunga viwanja vya ndege huyo uliyemsifia kwa kuchukua uamuzi yeye na mwenzake (nadhani unamfahamu) ummy yeye ni mtu wa kutoa ushauri tu wenye maamuzi wapo ndio wa kulaumiwa
una uhakika alitoa huo ushauri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla hujatupia lawama zako ungejiuliza tu huu ugonjwa source yake ni wapi, halafu jiulize hadi sasa umeathiri mataifa mangapi. Unadhani mataifa yote yaliyoathirika na huu ugonjwa hakufikiria hayo mawazo mepesi kama unayoyafikiria wewe? Ingekuwa ni rahisi hivyo basi leo hii usingeona dunia imetaharuki kiasi hiki. Watu wanafikiria vitu vikubwa kuliko hayo mawazo madogo unayoyawaza wewe. Kufunga mipaka ni moja ya option, ila siyo option ya kukimbilia sana kwa sababu ina hasara zake nyingi tu hasa kwa hizi nchi za afrika.
 
Bahati mbaya sana umemuonea Ummy mwalimu kwa kosa ambalo sio lake yeye kama yeye hana mamlaka ya kufunga viwanja vya ndege huyo uliyemsifia kwa kuchukua uamuzi yeye na mwenzake (nadhani unamfahamu) ummy yeye ni mtu wa kutoa ushauri tu wenye maamuzi wapo ndio wa kulaumiwa
Yeye km waziri mwenye dhamana anatakiwa ashauri mamlaka kuwa ugonjwa unapita paleee nashauri pafungwe simple that way, ajitoe kwenye lawama!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mfano kule Chunya kuna kachina kamepatikana na huo ugonjwa kamepelekwa Hospital ya rufaa mbeya sasa sijui kamefikaje

Ni jambo la kawaida hospitali zetu kuwa na taadhali. sio jambo la kushangaza.

hata hapa kanda ya kati ilikuwa hivyo hivyo jana. Lakini tunamshukuru Mungu tumeamka shwari
 
Katika mambo ambayo siamini ni pale mtu anaposhindwa kuiga mambo mazuri. Uganda wamefunga na kuzuia wageni kuingia nchini mwao, kenya wamezuia na mpaka nusura itokee mgogoro baada ya kugundua wagonjwa wanatoka ulaya na marekani. Sasa dada yangu Ummy kama waziri upo kama pazia. Leo hii tuna wagonjwa watatu wotete wamepitia viwanja vya ndege. Hivi mnawafanya watanzania wajinga na wasio na akili?

Hata hivyo nakupongeza Waziri Mkuu. Naona kama umechukua majukumu kushughulika na ugonjwa huu. Tafadhali funga mipaka na funga viwanja vya ndege hasa kwa nchi zilizo na shida kubwa hasa Ulaya, Asia na Marekani.

Ebu fikirini tunawaelekeza kama hawajui kazi yao.

Mtatuelewa mamii wakianza kufariki, ndipo hapo tukapopima uthabiti wa uwezo wa serikali yetu kupambana na majanga.

Waziri wa Afya atumbuliwe please.
Boss wake ndio anapaswa kutumbuliwa October 2020.
 
Ukiangalia waliokua na covid-19 wote wametokea ulaya kwanin serekali isisitishe Safari zote za ndege kuingia Tanzania angalau kwa mwezi mmoja

Kufunga shule ni hatua nzuri Ila sio ku-deal na chanzo
Magu kakimbilia chato ila hili dude litamfuata huko huko
 
Uwezo wangu wa kuwajibisha ni huyu waziri. Kwa sababu ilikuwaje mashine au watu aliowaweka Airport KIA hawakuweza kumtambua mkonjwa? Wsngapi wamepita bila kugundulika? Na hao wazungu wa leo waliogundulika wamepita wapi? Maafisa wa afya walikuwa wapi?
Sio rahisi kama unavyofikiria hata huko ulaya hakuna kupimo cha Corona moja kwa moja airport ingekuwa hivyo hiyo corona ingeishia china tu pale airport
 
Katika mambo ambayo siamini ni pale mtu anaposhindwa kuiga mambo mazuri. Uganda wamefunga na kuzuia wageni kuingia nchini mwao, kenya wamezuia na mpaka nusura itokee mgogoro baada ya kugundua wagonjwa wanatoka ulaya na marekani. Sasa dada yangu Ummy kama waziri upo kama pazia. Leo hii tuna wagonjwa watatu wotete wamepitia viwanja vya ndege. Hivi mnawafanya watanzania wajinga na wasio na akili?

Hata hivyo nakupongeza Waziri Mkuu. Naona kama umechukua majukumu kushughulika na ugonjwa huu. Tafadhali funga mipaka na funga viwanja vya ndege hasa kwa nchi zilizo na shida kubwa hasa Ulaya, Asia na Marekani.

Ebu fikirini tunawaelekeza kama hawajui kazi yao.

Mtatuelewa mamii wakianza kufariki, ndipo hapo tukapopima uthabiti wa uwezo wa serikali yetu kupambana na majanga.

Waziri wa Afya atumbuliwe please.
Usichokijua ni kwamba serekali hii huwa inaongozwa na mtu mmoja! Yaani mtu mmoja ndiye rais na ndiye waziri wa kila wizara!!
 
Ni wazi serikali hii ilidhamiria kabisa Corona iingie Tanzania kwa sababu hakukuwa na jitihada zozote za kuzuia huu ugonjwa kama kufunga mipaka yote na kuzuia International flights kutoka maeneo yaliyokuwa affected zisiingie Tanzania.

Tulishangaa kuona Waziri akitetea ujio wa Wachina ambao dhahiri kabisa walikimbia outbreak ya Corona kwao, eti waziri anadai "Wachina ni rafiki zetu hatuwezi kuwazuia kuja Tanzania ".

Hivi hizi ni akili za kawaida kweli?
Covid -19 has come to slam the slammers including those who slammed Ben Saanane, Aquilina, Mawazo, Kanguye Azori Gwanda, Mwangosi and many more victims of the deadly green [emoji216]!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom