Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Serikali kutodhibiti idadi ya wageni wanaoingia nchini kwa kisingizio cha Utalii, inahatarisha Usalama wa Taifa dhidi ya virusi vya Corona

Nimeangalia hii video nasikitika namna tulivyo na ujinga wa kupindukia. Dunia nzima inahaha na huu ugonjwa na wanajitahidi kuzuia wasafiri kutoka China.

Sisi kwa ujinga wetu tunajisifu kupokea wachina wengi. Let not be fooled by prosperous tourism industry citzens first.

Ugonjwa ukilipuka hapo hautachagua chama. let work together, raise voice.

Serikali kama haioni umuhimu wa maisha yetu basi tunafaa kuikumbusha kutumia akili. Yaani polepole ndo wakuja kuzungumzia masuala sensitive kama coronavirus kweli.

Halafu tunajisifu eti watalii wameongezeka. Gharama za huu ujinga zitakuwa kubwa sana tusipo zuia leo. Mark my word.

Swali ni kuwa huyu jamaa hajasikia kabisa hatari ya huu ugonjwa kweli?. Poor Africa, poor Tanzania.

View attachment 1371697
Mkuu punguza jazba ugonjwa huu nimpango mkakati wa kupunguza idadi kubwa ya watu kama ilivyo UKIMWI na MARALIA na mengine so tulia watupange watakavyo atakayenasa anaondoka atakayebaki atasimulia. Ili swala la serkali kutumia watu wapumbavu kuzungumzia mambo makubwa ya kitaifa tumelilea wenyewe kwa kuongoza nchi kwa matamko badala ya sheria na katiba. Nadhani ni muda muafaka kutenganisha shughli za vyama na Serkali ili kutoa nafasi kwa wataalamu wetu kutumia taaluma zao kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora slay Queen nitafikisha hata siku 14, wewe Marioo siku 3 tu tushakula ubwabwa ya nne tumekusahau umekua chakula cha funza.
Afu kumbe we kilaza eeh? Dalili zinachukua 14 days kuonekana we unasema siku tatu? Nyie ndo maana hamna mnachojua zaidi ya kudanga tu na kula bata...

Muone kwanza lisura lakee libayaa had apake mekap[emoji57]
 
Afu kumbe we kilaza eeh? Dalili zinachukua 14 days kuonekana we unasema siku tatu? Nyie ndo maana hamna mnachojua zaidi ya kudanga tu na kula bata...

Muone kwanza lisura lakee libayaa had apake mekap[emoji57]
Dalili zinaonekana kuanzia siku 14 kwa binadaam ila kwa nyie masokwe ni siku 3 tu ya nne ushatangulia kuzimu,
Hata hiyo ilikupita? Kweli porini ndio makazi yako.
 
Dalili zinaonekana kuanzia siku 14 kwa binadaam ila kwa nyie masokwe ni siku 3 tu ya nne ushatangulia kuzimu,
Hata hiyo ilikupita? Kweli porini ndio makazi yako.
Mimi sio sokwe,ni binadam
 
Ila jamani kuweni serious, inamaana hii serikali wizara ya afya ndio kumejaa mataahira namna hii??? Hata siamini kama kweli waChina wanaruhusiwa kuingia bila quarantine yeyote ile, au serikali imetuchoka inataka watz wote tufe?
 
Hapana hatupaswi kufanya unyanyapaa kwa mtindo wa kutenga kwa hili "isolation" haipaswi kueleweka kama "discrinination".Zipo njia nyingi za kuhakikisha tunajilinda lakini siyo kwa kuwanyanyapaa wengine.
Wachina hawakuomba kupatwa na Corona "wakati na bahati huwapata wote".Hatuwezi kuwazuia Wachina wote hata ambao wapo salama wasiingie Nchini kwa kigezo cha "Corona".
Tunafahamu tutakufa pia lakini tusikwepe kusaidia wenzetu kwa kiasingizio cha kufa.."what saves life is life".
Kipindi west Africa kuna ebola unajua walichotufanyia hao waChina?
 
Aah wapi. Sisi waafrika hasa watanzania tunaishukuru serikali ya dakta magufuri kwa usugu mkubwa wa gonjwa corona. Ikija watakao kufa ni chadema ila wale wa mashati ya mboga mboga utadunda. Wacha wachina waingie ili kudhibitisha hili. Asante sana dakta magufur.

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂😂😂😂😅😅😅😅😅😅😄😄😁😁😁😁😁😁😁😁😁😁😂😂😂😂😂😂😂😂😂 daaaah..., sijawahi cheka kiasi hiki....agghhh!!!
 
Rais Magufuli kuna clip ambayo imesambaa sana ikionyesha kujiwa na watalii wengi uwanja wa ndege wa kimataifa KIA kutoka China na mtendaji wa mamlaka wa uwanja wa ndege huo akitoa comments na kuthibitisha kuhusu ujio huo wa watalii.

Swali langu kwako Rais Magufuli, ina maana wewe na watendaji wa serikali yako mnajiona kama ni binadam wenye akili kubwa sana duniani kuliko binadam wengine wote? Au ndiyo ina maanisha kuwa watanzania wana njaa kubwa sana kiasi mbacho ikakufanya wewe na watendaji wako wa serikali yako mkakubali kuwaingiza watanzania kwenye riski kubwa ya kujipatia maradhi ambayo ulimwengu wote unatetemeka?

Watanzania wengi ndani na nje ya nchi yetu wamelalamika sana kuhusiana na uamuzi huo ambao wewe na watendaji wako mmeamua kuufanikisha. Watanzania wengi hasa walio nje ya nchi hawaelewi kwa nini serikali hiyo hiyo iliyokataa kuwarudisha vijana wetu wanaosoma huko kwenye mji wa mlipuko wa ugonjwa unaosababishwa na CORONA VIRUS, lakini hawa ma-tourist kutoka CHINA tunawapokea kwa mikono miwili? Ina maana wewe Rais Magufuli unajiamini kiasi hicho cha kuitumbukiza nchi yako kwenya janga kama hili ili mradi upate hela za miradi yako ya maendeleo?

Rais Magufuli mimi binafsi nilikuona ni mtu mwenye akili sana kuliko watanzania wote wengine, lakini kwa tukio hili inabidi niingie wasi wasi kuamini kuwa uwezo wako wa kufikiri mambo kama unalingana na yote uliyo tuuzia mpaka sasa. Usifikiri kuwa ni sifa kufanya vitendo vya namna hiyo, huko ni kujitengenezea kaburi letu wenyewe.

Usifikiri kuwa wewe na watendaji wako mna uwezo wowote ule wa kuweza kutibu ugonjwa huu kama utatokea Tanzania. Na hii nakuambia Rais wangu kuwa hata kama ungekuwa na hospitali ngapi na hata kama ungeangiza vifaa vya kisasa vya haina gani, nchi yako na watanzania kwa ujumla hawana uwezo wowote ule wa kutibu ugonjwa huu.

Pamoja na kuwa watanzania wamekuamini na kukusifu kwa matendo yako, lakini nakuomba kwa hili usimkufuru Mungu wako. Usijikute ukateketeza yote uliyoyafanikisha mpaka sasa. Kukiwa na Outbreack ya huu ugonjwa nchini, elewa kuwa Tanzania itateketea moja kwa moja. Tutaokota mizoga mpaka hapata kuwa na mtu tena wa kuokota mizoga hiyo.

Zaidi ya hapo naomba zingatia kuwa nchi yako haina wataalam wa kimaabara na wala hatuna research Institute yenye wataalam mbao wanatambulika kimataifa kuwa wana uwezo wa kufikiri beyond the horizone. Hao ma PHD holders wako wasikuzingue akili kiasi kwamba ukapoteza fahamu. Hao ni matheoretician tu na holders wa vyeti kwa ajili ya mishahara. Sio great thinkers hao. Waangalie wasije wakakuponza ukaharibu kila kitu.

Serikali ya nchi kama Ujerumani ina haha na kujaribu kuchukua njia zote zinazo wezekana kuzuia usambazaji wa huo ugonjwa wameshindwa sembuse serikali ya kitanzania ndiyo iweze?

Jumatatu iliyopita wajerumani walisheherekea Carnival, wenyewe wanaiita "Rosenmontag Zug" kwenye miji yao ya Duesseldorf, Cologne na Mainz. Mpaka kufikia asubuhi ya jumanne watu wawili walikuwa wamelazwa kwenye Hospitali yao ya jimbo la Nord Rhein Westfallia mjini Duesseldolf na mpaka leo tarehe 29.02 2020 tayari idadi ya watu zaidi ya 60 wamesha kuwa infected.

Ilianza na mtu mmoja kwenye Carnival yao Duesseldorf na hivi sasa majimbo manne yamekwisha kumbwa na ugonjwa huo, Hamburg, Hessen, North Rhine Westphalia na Baden Weurttenberg.

Inawezekekana nyie watanzania wa nyumbani mnachukulia kitu kimzaa mzaa sana. Lakini watanzania wengi ambao wako ughaibuni wana wasi wasi mkubwa sana na ndugu zao nyumbani na nchi yao pia. Hiki sio kitu cha kukichezea. Ni kitu hatari sana!

Nakuomba chonde chonde Rais wangu kuchukua hatua mara moja za kuzuia kumiminika kwa watu kutoka China. Maisha ya watanzania hata kama ni ya kisokwe, yanathamani kubwa sana kuliko hayo mabilion ya fedha yanayoingizwa na watalii. Hao watu wanao jiita watalii naomba wasubiri. Mali asili yetu na Mbuga za wanyama ziko na zitaendelea kuweko, lakini ndugu zetu kwa upande mwingine kama mlipuko.utatokea hawata kuwepo tena.

Rais Magufuli sisi masokwe hatuna uwezo hata mara moja wa kuzuia kuenea kwa ugonjwa unaosababishwa na CORONA VIRUS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania ni wajuaji msio na maarifa, kwa sasa Italy na uarabuni ni sehemu hatari zaidi ya China. Jimbo lenye mlipuko China ni Hubei ambalo lipo chini ya “lock down “. Hakuna mchina ambaye ni mkazi wa Hubei anaruhusiwa kutoka Hubei, hivyo wachina wa majimbo mengine ni salama.

Italy, South Korea na uarabuni ndio kwenye epidermic kwa sasa, kesi mpya kutoka nchi hizo kwa sasa zinaongezeka kuzidi China, maambukizi mapya kwenda zaidi ya nchi 10 duniani sasa yanatokea Italy na Iran, anza kulia kuzuia watalii wa Italy, South Korea na uarabuni ila sio China.
 
Back
Top Bottom