Wakati nchi mbali mbali duniani wana jihami na ugonjwa wa Corona ulioanzia China na kusambaa kwa kasi nchi mbali mbali jitihada zinafanyika kuzuia kusambaa zaidi ikiwemo kutopokea wageni kutoka China.
Nimeshangaa kuona afisa pale Kilimanjaro Inter. Airport ana furahia kupokea eti wageni wengi wanaotoka China kuja pumzika kutokana na kwao kusambaa corona.
Tuwe makini pesa ya utalii isije angamiza taifa. Nchi tajiri duniani zime kumbwa na huu ugonjwa na hawajaweza kuudhatiti sembuse sisi masikini tunao jazana kenye matatu na dala dala.
Rais toa neno taifa lisijeangamia. Kenya rais wao ameshapiga marufuku ndege toka China kutua tena baada ya waliopewa dhamana kushindwa kuweka zuio. Hali inajulikana haitavunja uhusiano wetu na China.
Mtu mmoja toka Italy kesha peleka ugonjwa Nigeria, hili ni somo.