Habari watanzania wote mliopo Tanzania.
Napenda niwaambie Kama korona itakua na athar kwetu Kama ilivyo Iran China Italy na Americans Basi mjue hatutaweza kupambana nayo hata kidogo na hata tukijaribu tutakua tumeshachelewa Kama tulivyoanza kuonesha dalil za uchelewaji.
Tanzania Sasa hivi Kuna wagonjwa watatu wote ni wagen kutoka nje. Hii inamaanisha kwamba Srikali ilipaswa kuliona ili tatizo mapema.
Sawa wote tunajua labda ilishindwa kufanya hivyo kwa sababu za kiuchumi lakin ilikua Bora nch ishuke kiuchumi Ila watanzania wabaki katika Amani na kuishi bila hofu hii ingesaidia Watanzania wote kuendelea kufanya shughuli zao ndan tu ya nchi na Wala asingetokea mtu kufa kwa njaa sababu tungekuwa na uwezo wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na maisha yangeendelea Safi tu mpaka dawa itakapopatikana.
Ila serikali imeshafanya kosa imeruhusu mipaka kuwa wazi na ugonjwa kuingia kwa inshu Kama io tujue kabisa hatuwezi kujilinda na huu ugonjwa ukiwa ndani Tena ndio maisha yatakuwa mabaya kushinda hata Yale ambayo tungekuwa nayo Kama tungefunga mipaka mapema.
Sababu Kama ugonjwa upo ndani tayari shule zingefungwa mahospitali yamefungwa bank zitafungwa na huduma nyingi za kijamii zitafungwa kama ugonjwa utakuwa hatari sana kama Italy watu italazimika wajifungie ndani wafe njaa au waende wakatafute riziki wafe kwa Corona kitu ambacho kingeweza kuziwilika Kama mipaka ingefungwa ndio maisha yangekua magum Ila watu wangepata Uhuru wa kujichanganya Kwani ambae angekuwa hana angeweza kumuamba mwenye anacho Ila ngoma iko humu humu watu tutakimbiana
Pia ningependa niishauri serikali kwanini haitaki kufunga mipaka badala yake inafunga shule na baadhi ya taasisi.
Tuombe Mungu atulinde tu basi ila ngoma ikiwa kama Italian Iran dah hatutaweza kabisa tusidanganyane tena dawa yenyewe Marekani anasema itaanza kupatikana ndani ya mieizi 18 unafikiri tutaweza? Kusubiri muda wote huo?
Sent using
Jamii Forums mobile app