Serikali kuwajadili waliokataa Ukuu wa Wilaya

WAtu mbina wanagomea hata kuwa Mwalimu Mkuu, Mganga Mkuu, Muuguzi Mkuu n.k.
Hilo wala halina uajabu wowote ule
 
Kwanini hawakuoni wewe mpaka wawape wenye ajira zao?, Kuna vijana wengi mtaani hawana ajira kwanini wasipewe....
 
wale walimu hawana jeuri ya kugomea teuzi za muajiri wao. Haingii akilini kugomea promosheni kwa mwalimu. Watakubali tu la sivyo waache kazi kitu ambacho ni ujuha kuacha kazi kwa kugomea uteuzi wa mkuu wa nchi aliyekutunuku heshima
 
hata mm nimemsikia Jenista mhagama akiliongelea jambo hilo na nimeshindwa kuelewa.kwani ni lazima ukiteuliwa na rais nafasi fulani ukubali hata kama unaona huwezi kuimudu nafasi hiyo?si wawateue wengine kwani wenye sifa hizo ndani ya ccm wameisha mpaka wawang'ang'anie hao hao tu?hawataki kwani ni lazima.
 
Kuna protocol mkuu athari kwa mtumishi wa umma kukata alikotumwa na bosi wake ni kubwa.Sahau nchi nyingine wanafanyake deal mifumo ya utawala wetu na sheria za utumishi zekoje kwetu.
mbona wakati wa Magu kuna mtu alikataa uteuzi wake na akaachwa kwa nn huyu jenister analeta kiherehere.elimu yake yenyewe ni kidato cha nne na nusu kombi ya HL lkn ujuaji mwingiiii.
 
Huo ni mtego,unaweza ukateuliwa huo ukuu wa wilaya na ukatenguliwa na huko ushaaga kwa mbwembwe.Watu wanaogopa kuumbuka mjini.Kila mwezi ni kuteua na kutumbua
 
Nchi ina watu kama mil 60 ivi, wasomi wapoooo pengine wangefanya vizuri zaid ya hao basi izo nafasi wapewe wengine
 
Sheria za kazi zinasemaje endapo mtu amekataa uteuzi? Mimi nafikiri mtu aandaliwe kwanza kisakolojia, kwanza kwa kumuhoji kuhusu utayari wake endapo atateuliwa kufanya kazi fulani kupitia teuzi zinazofanywa na taasisi nyeti ya urais.

Ili kuepuka suala kama hili lisijirudie, wateule watarajiwa wapimwe kwanza kuhusu utayari wao wa kuweza kutumikia majukumu mapya na kuyaacha yale ambayo wanayatumikia kwa wakati uliopo. Wengine hukwepa kufanya hivyo ili kukwepa mgongano wa maslahi.
 
Wanaona Raisi wao kazarauliwa , ifikie hatua wajue tuu kuwa Raisi ni binadamu Tu na yeye , madaraka hayo amepewa Tu na Mungu kwa Mda , na hawezi nyenyekewa na kila mtu , watu sio waoga wa maisha Yao , wengine wanajitambua bhana ..... Kama vip waueni sasa si mamlaka mnayo , sio kila sku kubwabwaja tuu na kulazimisha kitu ambacho wenyewe hawataki hyo kazi
 
Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.

Kwanini hajataja kipengele!!!
Kumtoa mtu kwenye kazi yake je, hakuna utaratibu? Wanapewa siku ngapi wakipokea ofa na kutakiwa kujibu? Kazi za CWT hazina utaratibu wake wa mtu anatokaje na inakuwaje? Na contract zao walipo zinasemaje?

Imekaa kama kuwaondoa watu waweka wanaowataka.. michezo hii ya kufukuza mtu kazi alipo? Je, akimaliza kuwa DC wanaweza kurudi?

Why ni lazima mtu akubali uteuzi kama anajijua hataki kazi hiyo?

Serikali na Rais kweli wanataka watumishi ambao wanajiona kazi hawawezi au kuzitaka?

Hii ya kulazimisha sio habari nzuri..
 
ni bora nikaachishwa kazi kuliko kuingia kwenye mifumo ya hovyo ya nchi hii.kama rais analalamika kuhusu pesa za plea bargaining wakati yeye alikuwa makamu wa rais na makamu wake wa sasa alikuwa waziri wa fedha sasa hayo si maajabu ya dunia?kama watashughurikiwa itakuwa ni uonevu wa hali juu na tutakuwa tunarudi kwenye mambo ya hovyo ya awamu ya tano.
 
Hzi ni taratibu za hovyo , na matokeo Yake ni kutengeneza Taifa la hovyo tuu, hakuna umhimu wwte wa kuwa na taratibu mbovu kama Hz , ndo mana tunasema Raisi apunguziwe mamlaka ya kuteua badala yake watu waombe kazi , Ila awe na mamlaka ya kutengua , kung'ang'ania taratibu kama hzi matokeo Yake ndo haya kulazimisha watu wa kutii , na wakizingua unaona kama umedharauliwa , majamaa wamekataa hyo kazi hawataki , ya nini kuanza kuwatisha tisha, chawa wote sa hv fyoko fyoko , kila Kona utasikia mama mama .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…