Serikali mnataka tufanye kazi gani?

Serikali mnataka tufanye kazi gani?

Salamu wakuu.

Kwanza kabla ya yote napenda kusema samahani sana kwa wale ambao nilikua nawaona hawana akili timamu wanapo iponda serikali yetu.

Ni kweli kabisa kwa mambo yanayofanyika ni too sad.

KiJana anapambana kujiajili. Anajinyima kula sometimes anakula.hata mlo mara mbili ili awekeze katika mambo yake.

Ila serikali yetu imekua ni sehemu moja wapo ya kurudisha maendeleo ya vijana hapa nchini...

Hivi kweli mnakuta mtu anapambana na kibiashara chake ana unga unga lakini from no where wanakuja watu wanajiita sijui nani wanataka vibari vya nini sjui...

Alafu wanakutoza pesa ambayo ukipiga maesabu mtaji wa kazi yako hata haufukii faini ya pesa waliyokutoza..

Sasa nauliza hivi tukiingia mtaani na kuanza kuiba , kukaba au kufanya mambo ya hovyo mtatufanya nini...

Kuna mambo mengine yanafanyika yanaumiza sana sana
Huku ni kurudisha a nyuma kimaendeleo wakuu

Nimeumia sana mpaka sasa pesa niliyoitafuta zaidi ya miaka mitatu imekuja kutolewa ndani ya dakika 5 tuu...
Inauma sana wakuu...
Ili kuepuka majanga kama haya unatakiwa kujua ni vibali gani vinahitajika na ni utaratibu gani unatumika katika kulipa kodi. Hii inasaidia sana kwenye kujipanga kimkakati.

Mdogo wangu, hakuna hata nchi moja watakuachia ufanye vile unavyopenda bila ya kufuata sheria, wala wasikudanganye maana huko maulaya ndiyo masheria magumu zaidi kuliko kwetu.

Usivunjike moyo hizo ndiyo changamoto za biashara ambazo wengi huwa wanapitia kimya kimya.
 
huana haja ya kuiba kuona wovu, wala kutamani au kudokoa mali ya wenyewe, watakupoteza bure tu

kilimo, ufugaji na biashara ni ajira za wazi, mtatiji ikiwa ni uthubutu, nguvu na bidii yako tu unatoboa maisha kiulaini sana :NoGodNo:
Unajua naposema biashara ndo hizo hizo tunazofanya mkuu
 
Mnaongea tu , mimi hayo yote nimefanya ,na hakuna kitu zaidi ya kutorekea
🐒 🙈 🙊 🐵 🙉 🐒 🙈 🙊

















nje tu , wengi wanajivunia kutokua raia wa nchi ya kusadikika 🤔🤔🤔 🐒
Mkuu hapa nimechanganyikiwa aiseee
 
Najua ipo mikakati kabambe ya kuwapa uhai chawa hivyo sita shangaa ushirika mpya wa chawa na kunguni kulinda maslahi ya bosi zao dhidi ya binadamu mnyonywa damu.
Mkuu kuna watu wanatufanya tuwe makatili sana aiseee
 
pole Sana - serikali yetu inakosa watu makini wenye kuwa na akili na hisia za kuvaa viatu vya watu wengine.


Japo nimeumia na kukuguswa natafakari njia bora ya kukusaidia katika kile ulichoharibikiwa

Stay calm and positive , hili nalo litapita.
Mkuu acha tuu .
Watu wanakutoa kwenye line..

Assume how mtu umewekeza alafu wanakuja wanakualibia tuu na sio kama wanapata mamilioni ya pesa..

Jua kali bado tunabaniana ridhiki
Sasa naungana na wale wanaoponda siasa za hi nchi aiseee
 
TRA
MUNICIPAL
ZIMAMOTO
AFISA KATA
BWANA AU BIBI AFYA
MIZANI
DIWANI
KITONGOJI
NAWENGINE SIWEZI MALIZA
Mkuu hao hao..
Watu wanapita hawana discussion na mtu hawajari una mda gani katika biashara..
Hawajali your income per day ngapi...
Assume mtu anakuja anakomba kila kitu anakwambia either wabebe vitu au utoe faini au jela au vyote kwa gafula
 
Back
Top Bottom