Serikali Toeni Elimu Visiwani waache Tabia ya kuzuia watoto wachanga Wasipate VISOGO!

Serikali Toeni Elimu Visiwani waache Tabia ya kuzuia watoto wachanga Wasipate VISOGO!

Kwan vp kiafya kuna tatiz loloto mtot kulazwa kisogo kikiwa chini?

Sio kosa mtoto kuwa na kisogo mkuu
Hahaha, hacheni tamaduni za hovyo, watafutieni WATOTO Wenu mahitaji muhimu na ya kisasa
 
Kitendo cha kuvibonyeza, kuvikandamiza vichwa vya watoto wachanga ili kuzuia kichogo, bila kutumia wataalamu wa afya, hii inaweza kusababisha hitilafu ya ubongo Kwa Mtoto. Na Kwanza kitabibu hairuhusiwi kufanya kitendo kama hicho.

Serikali kupitia wizara ya AFYA, toeni elimu ya kutosha, hasa visiwani Zanzibar (Pemba, Unguja).

Hospitali ya Muhimbili kitengo cha watoto na kitengo cha ubongo, inawapasa kutoa elimu ya AFYA ya Mtoto hasa huko visiwani Zanzibar.

Wizara ya ustawi ya jamii jinsi na watoto, elimisheni jamii, kwamba Mtoto kuwa na kichogo sio ukilema. Bali ni maumbile ya kawaida Kwa ukuaji wa mtoto pamoja na afya yake.

Maana wana wanyanyasa watoto vichanga, haya yote ni matokeo ya ukosefu wa elimu na Imani potofu huko visiwani Zanzibar.

Mtoto kuwa na kichogo Sio Kwamba atakuwa na muonekano mbaya AU Kwamba atachekwa na wenziwe shuleni, lahasha Bali, ni maumbile halisi ya kibinaadamu.

Wenyeji wa huko visiwani, heshimuni haki za watoto.
Habari bila picha hainogi. Kibaragashia kitakaaje vizuri?
 
Kwahiyo unataka kusema wazanzibari wote watakuwa na hitilafu ya ubongo,maana hiyo mila ina miaka mingi sana...
Kama wanachapa wasio wa imani yao wakila mchana basi jibu ni ndio. Mbona wabara huku hawako hivyo.
 
Wala hakandamizwi mtoto.

Mtoto anafungwa fungwa asijigeuze kulalia ubavu wa kichwa.

Hiyo watu wa Pwani tunafanya sana, siyo Zanzibar tu.

Mtoto atavaaje baraghashia akiwa na chogo kama isuzu za zamani?
Yaani kumbe yote haya for the sake of Baraghashia? Oya So Poa.
 
Kitendo cha kuvibonyeza, kuvikandamiza vichwa vya watoto wachanga ili kuzuia kichogo, bila kutumia wataalamu wa afya, hii inaweza kusababisha hitilafu ya ubongo Kwa Mtoto. Na Kwanza kitabibu hairuhusiwi kufanya kitendo kama hicho.

Serikali kupitia wizara ya AFYA, toeni elimu ya kutosha, hasa visiwani Zanzibar (Pemba, Unguja).

Hospitali ya Muhimbili kitengo cha watoto na kitengo cha ubongo, inawapasa kutoa elimu ya AFYA ya Mtoto hasa huko visiwani Zanzibar.

Wizara ya ustawi ya jamii jinsi na watoto, elimisheni jamii, kwamba Mtoto kuwa na kichogo sio ukilema. Bali ni maumbile ya kawaida Kwa ukuaji wa mtoto pamoja na afya yake.

Maana wana wanyanyasa watoto vichanga, haya yote ni matokeo ya ukosefu wa elimu na Imani potofu huko visiwani Zanzibar.

Mtoto kuwa na kichogo Sio Kwamba atakuwa na muonekano mbaya AU Kwamba atachekwa na wenziwe shuleni, lahasha Bali, ni maumbile halisi ya kibinaadamu.

Wenyeji wa huko visiwani, heshimuni haki za watoto.
Mkuu kama utawawekea hapa hiyo taarifa ya hospital ya muhimbili nadhani itawaonesha uhalisia na madhara ya tatizo hili

Vinginevyo nawe utakua na dhana potofu kwamba "Kila mtu lazima awe na chogo, Na ikiwa hana basi ameponndwa kichwa utotoni"

Pia kumbuka kua huo ni urithi. IKIWA UPO KWENU HAUKIMBILIKI
NA
IKIWA HAUPO HUNA PAKUUPATA
 
Kibagharashia kama ganda la chungwa
 
Dunia ina mambo hii
Wengine hawataki vichogo
Ila wengine wanawatengenezea kabisa watoto chogo refu kwa kuona kuwa ni urembo wao, unaitwa kilugha Elongeted head
Mtoto akizaliwa anafungwa manguo kichwani na kukazwa haswa mpaka kunaanza kuchongoka

Na hawa wenzetu pia wanahitaji kuelumishwa waondokane na mila hizo
Mbona wengi hatuna chogo na hatukukandwa?

Angalia sasa hawa
Screenshot_20240813_192334_Chrome~2.png
Screenshot_20240813_192206_Google~2.png
 
Back
Top Bottom