Serikali: Wahanga vyeti feki kulipwa mafao yao

Je Poo makonda na yeye atalipwa stahiki zake??
 
Tupe na ufafanuzi wa kujenge kibanda Cha mlinzi kwa milion 11 halafu ana cheti OG. Mwizi ni mwizi tu.
 
Tupe na ufafanuzi wa kujenge kibanda Cha mlinzi kwa milion 11 halafu ana cheti OG. Mwizi ni mwizi tu.
Halafu jambo jingine, hawa watu walifanya kazi mwaka mmoja wakiwa kwenye uangalizi, wakaonekana kumudu kazi na kuthibitishwa kazini. Kwa maana nyingine, hao watu walimudu kazi zao ndo maana wakathibitishwa kazini. Kwa hiyo hili pia lipo kwa upande wa serikali kuweza kujisahihisha, ndo maana hailazimiki kuchukua hatua kali sana dhidi yao kama wengine wanavyoshawishi.....​
 
hiyo m6 ni nyingi sana bwashe kama waliostaafu kiuhalali na wakiwa wakilipwa 1.3m bado wamepewa m8 tu.hayo matasisi hasa LIPPF lilidhulumu sana pesa ya watumishi.
 
Sazingine unaweza kukosa cha kuandika. Ama unaweza ukatukana ukaonekana mjinga kumbe ni mambo ya kuudhi kwa kiwango Cha juu sana.

Yani mtu ameghushi vyeti badala yakuchukuliwa hatua za kisheria eti analipwa hahahaa.
Labda kama Kuna jambo jingiane ambalo hatulifahamu,vinginevyo kunamtu anatengenezewa jungu alafu alaumiwe baadae naaonekane hafai kwenye nafasiyake.

Haiingii sio akilini tu,haiingii hata kwenye ujinga.
 
Huruma tayari ilisha tolewa baada ya kuamua kutowapeleka kwenye vyombo vya Sheria, "that's more than enough!"
Napia hawakutakiwa kurudisha pesa walizopata kama mishahara kwa njia ya udanganyifu.

Kuanza kuwalipa mafao nikuhalalisha uhalifu wao.
 
Tatizo la watawala wameshindwa kusimamia vitu vya msingi kama kupanda kwa gharama za maisha wamebakiza kuokoteza sifa kwa watu waharifu!
Yaani kwa nchi zingine hii ni jinai kubwa kwa usalama wa nchi na watu wake!
Ila kwa vile alifanya JPM wanataka kufanya tofauti ili aonekane alikuwa wrong!
Mpumbavu huwezi kuacha upumbavu hata umtwange kwenye kinu na baadae upime kiasi cha upumbavu utaukuta ni ule ule!
 
Hatimaye vibaka watanashati kulipwa mafao yao.
Only in Tanzania 🤣🤣🤣🤣
Mimi nashauri kwa kasi anayoenda nayo Mama ya kufungua nchi na HAZINA,sheria ya forgery ifutwe tu,mtu ambaye ata hakukanyaga shuleni,achonge Cheti na apewe ajira na ata ikiwezekana awe Rais au Waziri ili Taifa liendelee kwa kasi chini ya Watumishi mbumbumbu!
 
Lengo ni kuonesha JPM alikosea hakuna kingine!
 
Huruma tayari ilisha tolewa baada ya kuamua kutowapeleka kwenye vyombo vya Sheria, "that's more than enough!"
Napia hawakutakiwa kurudisha pesa walizopata kama mishahara kwa njia ya udanganyifu.

Kuanza kuwalipa mafao nikuhalalisha uhalifu wao.
Hawalipwi mafao, wanapewa makato ile 5% ya mshahara waliyokuwa wanakatwa kwenye mshahara. Serikali imekuwa na msimamo tofauti na hili hitimisho lako.
 
Mbona hili siyo jipya maana maagizo yalihatolewa kitambo kwamba walipwe michango yao?
 
Kumbe hadi leo hawakulipwa ! kwahiyo alichokua anatuambia Mchengerwa ilikuwa porojo siyo ?
 
Namuona anko magu alivyo nuna huko akhera baada ya kupata habari hii. Hee he laiti ningekukuwa hai wangelima kwa meno.
 
Hawalipwi mafao, wanapewa makato ile 5% ya mshahara waliyokuwa wanakatwa kwenye mshahara. Serikali imekuwa na msimamo tofauti na hili hitimisho lako.
Mkuu muhalifu hastahili kulipwa chochote, kitugani ambacho huelewi hapo.
Labda kama tulidanganywa kwamba watu walighushi vyeti na imejulikana waliingia kihalali.

Kwa namna yoyote kama nikweli walighushi vyeti kuwalipa makato sijui mafao vyovyote, kuwalipa niwadekeza wahalifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…