Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Serikali ya CCM mmeamua kutusaliti wananchi, Tunaenda kukumbwa na njaa kubwa hali ni mbaya

Wakulima wakubwa wa mpunga ifakara ni waganda ambao hukodi mashamba, na kuanza kulima baadae husafirisha mchele kuelekea kahama kwenda uganda ukitoa wasukuma hao wandamba na waluguru huko hawana kitu, inabidi tuwaeleze muelewe mavuno ni machache funga mipaka wanyarwanda na warundi wanaolima hadi binti manyanga kwenda kambi katoto chunya huko watauza chakula ndani hawatosafirisha kwenda kwao
Ifakar ipi hiyo?
 
Mimi ni mkulima na biashara ya mazao naijui kuliko wewe, mwaka huu mavuno ni machache soko la ndani pekee halina mazao, siwezi kufurahia kuuza sudani kusini au Rwanda wao wapate chakula huku nchini kuna njaa, tungekua tumevuna sana ruksa kuuza nje lakini hali ya mvua uliiona ilivo leo hii tunapoongea mimi na wewe kigoma, rukwa, katavi, mbeya, morogoro hakuna tena mazao sasa mikoa ya uzalishaji kama hiyo ikikosa chakula unategemea nini? Hii ni mwezi wa saba ukumbuke usifurahie bei kupanda angalia mateso ya maskini huko vijijini kwetu ambao kula yao hadi sasa ni shida, MAVUNO NI KIDOGO MWAKA HUU SOKO LA NDANI TU HALINA KITU HAKUNA SABABU YA KUFUNGUA MIPAKA.
Morogoro ipi ambayo chakula hamna
 
Mimi naona ni Sawa tuu kwakuwa asilimia 75 ya watanzania wanategemea shughuli za kilimo kuendesha maisha yao.

Kama unataka kujua anaefurahia bei ya mazao kupanda nenda ifakara mashambani huko ndo utajua sio kuleta propaganda hapa jukwaani.

Acha soko liongee tumechoka kuwa wanyonge
 
Huna tu akili na hujui unachozungumza!
Muda kama huu hakuna mkulima mwenye Mahindi, ama kama wapo ni wachache sana!
Mahindi yapo sasa hivi mikononi mwa WALANGUZI wachache walio ya langua kwa bei ya chini kwa Wakulima na sasa wanayauza ili kupata faida ya juu kupita kiasi.
Wewe endelea kushangilia Simba au Yanga na Kubet ndizo kazi unazoweza kuzifanya hapa Duniani!
Hili watu hawalioni wala kulielewa kabisa.
Mkulima gani wa hekari 5 ghalani mwake anakuwa na gunia 2000!!???
 
Tulishauri mwaka huu mavuno ni kidogo wafunge mipaka kwani hata soko la ndani tu linatosha wakashupaza vichwa vyao.

Mavuno yakiwa mengi watu wauze nje ni sawa lakini mwaka wenye mavuno kidogo nao wauze nje kipindi chote hapana,

Burundi kuuza mahindi, maharage, mtama na muhogo ni uhujumu uchumi kwa sasa, Uganda kazuia hakuna kuuza chochote nje isipokua ni ruhusa kununua, na kuingiza ndani,

Rwanda kazuia kabisa hakuna kutoa hata kiazi, wizara ya kilimo ipo ipo tu imekalia siasa, hakuna usalama kama nchi haina chakula cha kutosha na mkumbuke dunia nzima mavuno kwa mwaka ulioisha yalikua hafifu sana, viongozi hawachukui maamuzi simply sababu wao na familia zao njaa haitowakumba.
Badala la kushinda Jf tumia uhaba wa chakula kama fursa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kakwambia mkulima ndiye anayenufaika na biashara hii ya chakula kupelekwa nnje ya nchi?

Njoo huku Kusini (Mtwara na Lindi) uone jinsi tunavyonunua ufuta kilo moja tsh 1100 - 2000 kutoka kwa mkulima na sisi tunauza tsh 3190 kwa kilo.

Mkulima ananufaikaje na bei hiyo ya 3190 kwa kilo!!??
Mnapenda kuongea vitu ambavyo hamvifahamu.
Wakulima wanaonufaika na bei kubwa ya mazao ni wakulima wakubwa tuu.

Wanufaika wakubwa wa kupanda kwa bei ya mazao ni watu wa kati (madalali) ma wafanyabiashara wa mazao.
Nikupe mfano mmoja,kuna kijiji ambacho wakazi wake walilima ufuta na kupata mavuno mazuri lakini changamoto yao ni kuwa umbali wa kutoka hapo kijijini mpaka kwenye mnada wa ufuta ni km 29.

Hakuna usafiri wa mabasi.
Mimi nimeenda huko nikawaambia nanunua ufuta kwa tsh 1200 kwa kilo,wamekubali kuliko kusubiri kwenda mnada ambao watauza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani itakayowachukua wiki kupata fedha yao.

Umeona mkulima anavyoteseka hapo sasa!?
Nenda wewe kanunue kwaiyo Bei rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakulima wakubwa wa mpunga ifakara ni waganda ambao hukodi mashamba, na kuanza kulima baadae husafirisha mchele kuelekea kahama kwenda uganda ukitoa wasukuma hao wandamba na waluguru huko hawana kitu, inabidi tuwaeleze muelewe mavuno ni machache funga mipaka wanyarwanda na warundi wanaolima hadi binti manyanga kwenda kambi katoto chunya huko watauza chakula ndani hawatosafirisha kwenda kwao
Umekatazwa kwenda kuweka Kambi huko ifakara mpaka waganda wakupige bao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, si hivyo.

Nadhani hukuelewa alichomaanisha yeye. Hajakataa wakulima kuuza kwa faida kwa yeyote yule iwe ndani au nje ya nchi. Lakini hili halifanyiki holela tu. Hakuna serikali popote duniani inayoruhusu namna hiyo ya ufanya biashara.

Kama wakulima wenyewe wanaouza mazao yote, hata akiba ya chakula chao, njaa ikiingia nchini, hilo siyo janga?
Wazembe wafe maana ni mzigo kwa jamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom